Kutoka Vijibweni Kigamboni, ccm wadaiwa kuingiza wapiga kura 'fake', watu 15 wanaswa

Mwita Maranya

JF-Expert Member
Jul 1, 2008
10,564
7,973
Katika hali inayoashiria hali si shwari kwa upande wa ccm, wameingiza wapiga kura feki katika kata ya vijibweni.
Taarifa za ndani kabisa zimedokeza kuwa kiasi cha kadi 1700 zimetengenezwa kwa ajili ya kuwasaidia kuongeza kura.
Baada ya kupatikana taarifa hizo, Chadema iliwafahamisha mawakala na kuwaelekeza namna ya kuzitambua. Katika zoezi la kutambua kadi feki, watu kumi na tano wamekamatwa wakiwa na kadi feki katika vituo vya Nunge, Shule ya msingi Vijibweni na Ofisi ya mtendaji Vijibweni.
Baada ya kunaswa kwa watu hao kumi na tano inaonekana wameambizana na sasa hakuna kadi feki inayopatikana.
Tunaendelea kufuatilia matukio na tutawajuza kadri yanavyopatikana.
 
hawajama kazi wanayo, mwaka huu wanaweza ila 2015 sijui itakuwaje?
 
Ahsante kwa taarifa mkuu, hizi ndiyo janja za ccm!! Natamani sana wanaofanya huu mchezo siku moja tuunde mahakama ya kushughulikia hii tabia chafu na kujenga taifa lenye watu wanaoheshimu taratibu za nchi bila kujali vyeo, vyama, dini au rangi.
 
Updates wengine watatu wamekamata shule ya msingi vijibweni wakiwa na kadi za kupigia kura walizojiandikishia ilala. Sasahivi wamezuiliwa na vijana wetu ofisini kwa mahojiano zaidi kabla ya kukabidhiwa kwa polisi.
 
More updates taarifa zinanifikia kwamba watu wengine wanane wamenaswa kituo cha nunge wakitaka kupiga kura kwa kadi fake, majina yaliyo kwenye kadi ni sawa na kwenye daftari isipokuwa picha za kwenye kadi zao za kupigia kura ni tofauti na zilizopo katika daftari!

Taarifa za ndani tulizopata awali ni kwamba Nunge ndio kituo muhimu walichopanga ccm kukitumia kuingiza wapiga kura feki kutokana na jiografia yake na pia ndio ngome ya ccm.
Chadema tumeamua kuwakaba hapo hapo ili wasipate fursa ya kuingiza wapiga kura feki ama kuingiza kura feki!
 
Kadi feki!!
Hizi mbinu haziishi?
Hivi kwingine kama mwanza na arusha mawakala wameambiwa hii mbinu?
Utaitambuaje?
Kama walikuwa na datari na paricular zote za watu waliohama, kadi feki unaijuaje?
 
TUPE UPDATES MZEE WA VIJIBWENI,HAWA MAGAMBA TUTAWATAWAZA KWA TINDIPOLE!!.Watajibebaje?
 
Magari yenye namba za DFP, STK na PT zimefurika vijibweni.

Baadhi ya magari hayo yamejaza watu wakishushwa katika vituo mbalimbali vya kupigia kura. Gari moja aina ya land cruiser station wagon imeshusha watu kama 15 hivi katika kituo cha ofisi ya mtendaji na bila kutarajia wakati wanaelekea kuingia kupiga kura tukawasili kituoni hapo tukiwa na campaign manager pamoja na mgombea ghafla wakaanza kuondoka mmoja mmoja wakapanda gari na kuondoka haraka.
Hali ya upigaji kura inaendelea vizuri pamoja na vijikasoro vidogo vidogo ambavyo vimeendelea kutatuliwa.

Polisi ni wengi sana na wanazidi kumiminika vijibweni.
 
Vijana wa green guard a.k.a Janjaweed wameanza kuwasili kwa wingi vijibweni.

Hali ya tension inaanza kujitokeza hapa kutokana wingi wa polisi, usalama wa taifa pamoja na janjaweed.

Lakini niwatahadharishe ccm kwamba chadema tunao vijana wa kutosha kwa siku ya leo kuhakikisha kwamba ulinzi kwa viongozi na wanachama wetu hawadhuriwi na janjaweed!
 
Back
Top Bottom