Tume ya uchaguzi Kenya yafuta majina elfu 88 ya watu waliofariki kwenye daftari la wapiga kura.

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
3,504
2,000
chibuka.jpg

WAFULA CHEBUKATI - Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchini Kenya.

Tume ya Uchaguzi Kenya imeyaondoa zaidi ya majina ya watu elfu themanini na nane waliofariki dunia kutoka kwenye daftari la wapiga kura.

Hatua hiyo ya Tume ya Uchaguzi imefuatia taarifa kuwa zaidi yawatu elfu tisini na mbili walio fariki dunia wa mo katika daftari la usajili.

Mwenyekiti wa tume hiyo, WAFULA CHEBUKATI amesema tume ifahamu kuwa Nusajili ya wapigaji kura hau wezi kukosa majina kadhaa ya wafu, lakini inaamini kuwa teknolojia itathibitisha kwa uhakika na hakutakuwa na udanganyifu siku ya uchaguzi .

Orodha ya wapigaji kura iliyoidhinishwa kutumiwa katika uchaguzi mkuu mwaka huu ina jumla ya wapigaji kura milioni kumi na tisa, laki sita, elfu kumi na moja, mia nne ishirini na watatu wakiwemo watu laki nne, elfu tatu mia tati, tisini na watatu walio katika nchi tano na wengine elfu tano, mia tano ishirini na wanane waliosajiliwa katika magereza mia moja na kumi na manane ya nchini humo.


chanzo; ITV
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom