Kutoka Shinyanga, yanayojiri uchaguzi wa madiwani

n00b

JF-Expert Member
Apr 10, 2008
1,006
2,667
Hapa Kakola:

Mkuu wa Mkoa, RPC na OCD wanaonekana kutumia nafasi zao kushawishi wananchi kuichagua CCM katika kata ya Bugalama. CHADEMA ina nguvu sana katika kata hii.

Katibu wa CCM wilaya ya Kahama - Shinyanga ametinga kwny kituo cha kupigia kura cha Bugalama akiwa na gari lake lenye nembo ya CCM (Jembe na Nyundo); Vincent Nyerere kamtimua!

Mgombea udiwani kata ya Bugalama kwa tiketi ya CHADEMA, Erasmus Malugu ametoweka katika mazingira ya kutatanisha tangu jana saa 2 usiku na hajulikani alipo. Familia yake inadai hata simu zake zote hazipatikani na wanahofia huenda katekwa na makasa wa CCM.

Naelekea Mwawaza
 
Mungu saidia Diwani wetu mtarajiwa apatikane akiwa hai,hawa magamba hawapendi demokrasia hata kidogo hivyo wanaweza kumteka kweli!
 
Wananchi wapo radhi kukichagua hata kinyesi kuliko kuichagua CCM! Wazomeeni hao wezi RPC na OCD.
 
cHaDeMa.......!!

Enyi mnaojiita upinzani, achane siasa za kitoto, mmajificha au kujiteka wenyewe halaf mnaropoka kuwa haonekani....

kwanini asingetekwa wakati wa kampeni, atekwe siku ya kupiga kura!! huo ni ujinga ambao cDm mnataka kutuaminisha.

Mnajificha ili mpewe Publicity, tumeshituka siku hizi, hamtudanganyi tena.

Hizi ni siasa za kitoto sana. Siwezi kutofautisha na mambo wanayoyafanya viongozi wa uWaMsHo......
 
Nipo Kata ya Mwawaza Shinyanga.

Mbunge wa viti maalumu CHADEMA, Rahel Mashishanga amenusurika kufa baada ya kuvamiwa na kushushiwa kipigo na watu wanaodhaniwa kuwa ni wafuasi wa CCM.

Kipigo hicho inadaiwa amekipata asubuhi ya leo wakati alipokuwa akitembelea vituo vya kupigia kura kata ya Mwawaza ili kujionea zoezi hilo linavyoendelea.

Gari lake limepondwa mawe huku vioo vya gari hilo vikiharibiwa.

Amepigwa jiwe na kutenguka bega lake la mkono wa kushoto, na meno mawili inadaiwa huenda yameng'oka baada ya kupigwa jiwe pia. Dah hii ndiyo Tz yetu.

Baadaye nitaenda kumpa pole hospitalitali alipolazwa.
 
Nipo Kata ya Mwawaza Shinyanga.

Mbunge wa viti maalumu CHADEMA, Rahel Mashishanga amenusurika kufa baada ya kuvamiwa na kushushiwa kipigo na watu wanaodhaniwa kuwa ni wafuasi wa CCM.
Kipigo hicho inadaiwa amekipata asubuhi ya leo wakati alipokuwa akitembelea vituo vya kupigia kura kata ya Mwawaza ili kujionea zoezi hilo linavyoendelea.
Gari lake limepondwa mawe huku vioo vya gari hilo vikiharibiwa.

Amepigwa jiwe na kutenguka bega lake la mkono wa kushoto, na meno mawili inadaiwa huenda yameng'oka baada ya kupigwa jiwe pia. Dah hii ndiyo Tz yetu.

Baadaye nitaenda kumpa pole hospitalitali alipolazwa.

what!? Watu wa cdm hawakuwepo? Walikuwa wanaangalia tu? Kwanini hawakumsaidia? Polisi hawakuwepo?
This is too much!
 
Nashukuru kuwa Rachel pamoja na kujeruhiwa ameendelea kupost humu jukwaani na kutoa updates.

Upone haraka Rachel.
 
Last edited by a moderator:
Hivi vurugu zinafanyika hata siku ya uchaguzi? Tena wa madiwani? 2015 tutarajie nini sasa?

Hawana aibu kabisa hawa jamaa wao wanachokwepa ni aibu bila kujali watashinda kwa njia ipi hata kama ni ya aibu kuliko aibu wanayoikwepa.
 
Mkuu n00b, huyo mgombea aliyetoweka amepatikana?
This is scary stuff.
 
Last edited by a moderator:
hata huku Lwenzera...wanachama 2 wa cdm wamekatwa mapanga usiku wa kuamukia leo na hali zo ni mbaya wamelazwa hospitali ya wilaya ya Geita
 
Kuna chama kinaitwa "Chama Cha Magaidi" naamini ndio kinafanya hayo majanga. Kinaendelea kuwa "....Cha Majanga/Majambazi/Majangili..." Hivi ujinga wa kuwa unaweza kulazimisha watu kwa nguvu wachague wasiyemtaka utawaisha lini "HAO WAHUNI"?
Hila zitawatafuna waliozipanga mpaka ziwamalize.
 
Kweli hawa Magamba wamelemewa kazi yao ni kuua wapinzani kwa style kuwatumia Green gurd.
 
Mungu mlinde na kumwokoa Erasmus mikononi mwa watesi wasiopenda kuona mabadiliko ya kitokea kwa njia ya haki na amani
 
Back
Top Bottom