Makamu Mwenyekiti UWT Taifa atembelea mradi wa maji Tinde Shinyanga

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,903
945
MAKAMU MWENYEKITI UWT MNEC. ZAINAB SHOMARI ATEMBELEA MRADI WA MAJI TINDE-SHINYANGA

Makamu Mwenyekiti wa umoja wa wanawake Tanzania UWT Taifa MNEC Zainab Shomari jana Agosti 27.2023 ametembelea mradi wa awamu ya pili wa usambazaji maji katika Kata ya Tinde Wilaya ya Shinyanga unaotarajiwa kuhudumia wananchi 60,000 katika vijiji 22.

Mradi huo uliogharimu Shilingi Bilioni 1.15 unahusisha ulazaji wa Bomba za chuma na za plastiki kwa urefu wa kilomita 7.6,uwekaji wa enka za kushikilia bomba,ujenzi wa chemba na ufungaji wa viungio.

MNEC. Zainab Shomari amesema kuwa Serikali ya awamu ya 6 inayoongozwa na mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. Dokta Samia Suluhu Hassan imeendelea kutekeleza miradi ya kimkakati yenye tija kwa wananchi ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM 2020-2025.

“Rais Dokta Samia amedhamiria kumtua mwanamke ndoo kichwani,tunafahamu eneo ili lilikuwa na changamoto kubwa ya uwepo wa maji safi na salama,hivyo mradi huu umemaliza changamoto hiyo na niwaombe mamlaka ya Majisafi na usafi wa mazingira Shinyanga (SHUWASA) msambaze huduma hii kwenye kila nyumba”Amesema Mama Zainab Shomari.

🗓27/8/2023 📍Tinde-Shinyanga

UWT IMARA. JESHI LA MAMA. KAZI IENDELEE.
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2023-08-28 at 13.27.36.jpeg
    WhatsApp Image 2023-08-28 at 13.27.36.jpeg
    59.4 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2023-08-28 at 13.27.35(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-08-28 at 13.27.35(1).jpeg
    66.1 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2023-08-28 at 13.27.35.jpeg
    WhatsApp Image 2023-08-28 at 13.27.35.jpeg
    100.6 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2023-08-28 at 13.21.14.jpeg
    WhatsApp Image 2023-08-28 at 13.21.14.jpeg
    30 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2023-08-28 at 13.21.13.jpeg
    WhatsApp Image 2023-08-28 at 13.21.13.jpeg
    30.9 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2023-08-28 at 13.21.12(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-08-28 at 13.21.12(1).jpeg
    34.6 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2023-08-28 at 13.21.12.jpeg
    WhatsApp Image 2023-08-28 at 13.21.12.jpeg
    43.2 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2023-08-28 at 13.21.11.jpeg
    WhatsApp Image 2023-08-28 at 13.21.11.jpeg
    31.3 KB · Views: 1
Back
Top Bottom