Wana MMU, Umuofia kwenu!
Kuna kisa kimenikuta nimeona sehemu pekee ya kupata ushauri na mawazo mapana ni kwenu!
Nilikuwa na mchumba ambaye tulikuwa tunapendana sana na muda si muda tungefunga pingu za maisha. Ghafla mwenzangu alipata safari ya kwenda Marekani na kuniomba tuahirishe zoezi mpaka atakaporudi kwani asingechukua muda mrefu.
Nikamkubalia; akakwea zake pipa na alipokuwa huko mawasiliano kwa njia za mtandao yaliendelea. Siku moja akaniambia hawezi tena kuolewa na mimi kwa kuwa alikuwa anataka kufunga ndoa na mtu mwingine. Nilisononeka sana kwa namna nilivyompenda, lakini nikawa sina namna zaidi ya kumtakia kila la heri katika mahusiano yake hayo mapya. Baada ya kuuguza maumivu, nikapata material wife na tukafunga pingu za maisha. Sasa nina miaka kadhaa kwenye ndoa.
Hivi karibuni aliyekuwa mchumba wangu karejea kutoka America na akanitafuta kwa udi na uvumba na akafanikiwa kunipata. Ananiambia bado ananipenda na yuko tayari kutoa gharama yeyote ili nimwache mke wangu.
Kaweka one billion nikamtolea nje! Nikamweleza namna ambavyo tunaishi na mke wangu na watoto kwa amani na kwamba nampenda mke wangu na watoto sana. Hivyo pendo langu kwake limeshapata replacement.
Baada ya majadiliano ya muda mrefu mrefu akarealize kwamba hawezi kunishawishi kwa namna yeyote kumwacha my beloved wife, akaingiza hoja nyingine ya kuwa second wife kwani hawezi kuishi bila mimi.
Na kwamba kama nikimkatalia na hilo basi hana haja ya kuendelea kuishi. Anasema kama pesa anazo lakini kakosa mwanamme aliyemwonyesha mapenzi ya kweli na aliyemfikisha kileleni kama mimi. Hilo ndo linanitisha nikaona niliweke kwenu wadau!
Karibuni kwa ushauri.
ebu mpe kamba tuone kama kweli atajitoa uhai
One billion mnaijua nyie????
Karibuni kwa ushauri.
Haaa best nmekumic
ah sema wewe...umepoteaaaaa. ulikuwa wapi bwana?
Nmekumbatiwa na shemejiyo...
Mpunga huuu ni noumer sana !
kijana ana post tatu tu....hii ni ya kwanza MMU...
AKIJICHANGIA HII MADA....Topic: Swali kwa waliooa/kuolewa
AKAONGEZEA...
ANGALIA MANENO YAKO YASIKUHUKUMU...
HAPA AKIMPIGA MKWARA MLA WAKE ZA WATU...KASAHAU YEYE ''MME WAS MTU''
AKIUNGA MKONO COMMITMENT YA NDOA...
mytake:ndoa na iheshimiwe nawatu wote...
Wana MMU, Umuofia kwenu!
Kuna kisa kimenikuta nimeona sehemu pekee ya kupata ushauri na mawazo mapana ni kwenu!
Nilikuwa na mchumba ambaye tulikuwa tunapendana sana na muda si muda tungefunga pingu za maisha. Ghafla mwenzangu alipata safari ya kwenda Marekani na kuniomba tuahirishe zoezi mpaka atakaporudi kwani asingechukua muda mrefu.
Nikamkubalia; akakwea zake pipa na alipokuwa huko mawasiliano kwa njia za mtandao yaliendelea. Siku moja akaniambia hawezi tena kuolewa na mimi kwa kuwa alikuwa anataka kufunga ndoa na mtu mwingine. Nilisononeka sana kwa namna nilivyompenda, lakini nikawa sina namna zaidi ya kumtakia kila la heri katika mahusiano yake hayo mapya. Baada ya kuuguza maumivu, nikapata material wife na tukafunga pingu za maisha. Sasa nina miaka kadhaa kwenye ndoa.
Hivi karibuni aliyekuwa mchumba wangu karejea kutoka America na akanitafuta kwa udi na uvumba na akafanikiwa kunipata. Ananiambia bado ananipenda na yuko tayari kutoa gharama yeyote ili nimwache mke wangu.
Kaweka one billion nikamtolea nje! Nikamweleza namna ambavyo tunaishi na mke wangu na watoto kwa amani na kwamba nampenda mke wangu na watoto sana. Hivyo pendo langu kwake limeshapata replacement.
Baada ya majadiliano ya muda mrefu mrefu akarealize kwamba hawezi kunishawishi kwa namna yeyote kumwacha my beloved wife, akaingiza hoja nyingine ya kuwa second wife kwani hawezi kuishi bila mimi.
Na kwamba kama nikimkatalia na hilo basi hana haja ya kuendelea kuishi. Anasema kama pesa anazo lakini kakosa mwanamme aliyemwonyesha mapenzi ya kweli na aliyemfikisha kileleni kama mimi. Hilo ndo linanitisha nikaona niliweke kwenu wadau!
Karibuni kwa ushauri.
Hata mimi nashangaa, nahisi kwa mchumba wa America!