Kutoka Mahakamani Kisutu: Kesi 2 dhidi ya Maxence Melo zatajwa na kuahirishwa hadi 26 Januari 2017

JamiiForums

JF Official Account
Nov 9, 2006
6,227
5,278
Ndugu WanaJF,

Kesi inayomkabili Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media (waendeshaji wa mtandao wa JamiiForums na FikraPevu) ndugu Maxence Melo, inatarajiwa kutajwa asubuhi ya leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.

Maxence Melo anashtakiwa kwa makosa matatu ikiwemo kuzuia Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi kwa mujibu wa Sheria ya Makosa ya Mtandao na Kusajili tovuti ya JF kwa kikoa cha .com badala ya .co.tz jambo ambalo Serikali inadai ni kinyume cha sheria.

Zaidi Soma => Maxence Melo ashtakiwa kwa makosa 3, likiwemo la Kumiliki Tovuti ambayo haijasajiliwa Tanzania

=> Mkurugenzi wa Jamii Media akamatwa na Polisi

Kutokana na unyeti wa kesi hii na umuhimu wake ktk kutetea Uhuru wa Maoni, Timu maalumu ya JamiiForums itakuwepo katika viunga vya mahakama ili kukuletea moja kwa moja yanayojiri.

Ungana nasi kwenye uzi huu na kwenye kurasa zetu za Facebook, Twitter na Instagram @ JamiiForums, ili uweze kupata LIVE updates muhimu kutoka mahakamani.

=======

UPDATES;

3:20 ASB
: Shughuli za kawaida za mahakama zinaendelea, kesi mbalimabili zikiitwa. Kesi ya ndugu Maxence bado haijaitwa, inatarajiwa muda wowote itaitwa.

3:29 ASB: Kesi ya kwanza imeitwa mahakama ya Kisutu(Open chamber #2)

9:50 ASB: Mashauri yote yameahirishwa mpaka tarehe 26, January 2017 baada ya upande wa Jamhuri kudai upelelezi haujakamilika.

Kwa shauri la kesi ya tovuti kutosajiliwa kwa kikoi cha .co.tz, mheshimiwa hakimu Simba ameutaka upande wa Jamhuri kufanya upelelezi haraka kwa shauri hilo.

6c59f2e9-cdd2-4f15-83fd-89c541cbe091.jpg
Kutoka kushoto ni Wakili wa kampuni ya Jamii Media Benedict Ishabakaki, Maxence Melo Mkurugenzi mtendaji wa Jamii Media, Mbaraka Islam wa Raia Mwema na Wakili wa kampuni ya Jamii Media Jebra Kambole, wakiwa katika viunga vya Mahakama ya Kisutu.

======

To our English Audience

JamiiForums co-founder’s 2 cases adjourned to Jan 26, 2017

Two among three Cases facing the co-founder of JamiiForums and Managing Director of Jamii Media, Mr Maxence Melo, have been adjourned until January 26.

A fortnight ago, Mr Melo was arraigned at the Kisutu Resident Magistrates’ Court with three charges in three different cases by three different magistrates. In the first case, Mr Melo was charged with managing a website that was not registered in Tanzania in contravention of the Electronic and Postal Communications Act, 2010.

Today, the cases were scheduled for mentioning, but had to be adjourned with the prosecution informing the court that investigations were yet to finalised. Mr Melo is out on bail since Monday last week after spending a week in police custody.

 
Wana JamiiForums tupo hapa kufuatilia kesi yetu ya haki ya kuzungumza ktk baraza letu kwa uhuru na bila woga au hofu.
 
Tuko pamoja wakuu kila baya dhidi ya dhuluma yoyote juu ya haki ya kupata habari itashindwa hatuwezi kuzibwa midomo kwa matakwa yao
 
Wanataka kutuziba midomo ili kila wafanyalo sisi tuwe ni watu wa kuitia ndio pasipo kuhoji chochote hata kama kina manufaaa kwa umma
 
Ndugu WanaJF,

Kesi inayomkabili Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media (waendeshaji wa mtandao wa JamiiForums & FikraPevu) ndugu Maxence Melo, inatarajiwa kutajwa asubuhi ya leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.

Maxence Melo anashtakiwa kwa makosa matatu ikiwemo kuzuia Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi kwa mujibu wa Sheria ya Makosa ya Mtandao na Kusajili tovuti ya JF kwa kikoa cha .com badala ya .co.tz jambo ambalo Serikali inadai ni kinyume cha sheria.

Zaidi Soma => Maxence Melo ashtakiwa kwa makosa 3, likiwemo la Kumiliki Tovuti ambayo haijasajiliwa Tanzania
........

Kutokana na unyeti wa kesi hii na umuhimu wake ktk kutetea Uhuru wa Maoni, Timu maalumu ya JamiiForums itakuwepo katika viunga vya mahakama ili kukuletea moja kwa moja yanayojiri.

Ungana nasi kwenye uzi huu na kwenye kurasa zetu za Facebook, Twitter na Instagram @ JamiiForums, ili uweze kupata LIVE updates muhimu kutoka mahakamani.
=======

Mkurugenzi wa Jamii Media akamatwa na Polisi
Ngoja niwahi kiti cha mbele kabisa
 
Hilo swala la kuregister .co.tz aliyelileta kama bado yupo serikalini wamfukuze

Hii serikali imekosa watu wanaofikiri kichwani hadi kuchagua watu ambao wako tayari kukubana ulipe elfu ishirini badala ya milioni. Hakuna nchi ngumu duniani sasa hivi kuinvest kwenye technology kama bongo, ukifanikiwa kidogo tu, utaletewa sheria nyingine hutoamini kama ni sheria. Hii ya dot tz piga ua, bora nikaishi kenya
 
Back
Top Bottom