Kutoka kwenye maktaba ya jamii 1990 kigamboni harusini

Kutoka kwenye maktaba ya jamii 1990 kigamboni harusini

Umenichekesha sana..walikomajeeee?




Hahahahaha,na mimi nimejikuta nacheka nikikumbuka tukio lile maana jamaa walitazamana kisha wakaulizana huyu Ustaadha wa wapi huyu..?? Mbona hafananii............
 
Hawa jamaa walianza na NYAMA kwanza?hapa sizioni eti

Uswazi kwa uzoefu wangu, hadi sinia hiyo inafika chini huwa tayari REKI zimepita na kutoa MABONGE/VINYANGO vya nyama zote.....Yaani UBWABWA ukifika hapo uuonapo ni wenyewe tuu na NYAMA zinakuwa tayari mikononi mwa wenye SPIDI ya kureki!!!!
 
Mara nyingi nyama huwa zinadakwa juu kwa juu sinia ikifika chini hakuna nyama hata moja

Na sehemu hizo usithubutu kukaa na wazee utakabwa na chakula au kupaliwa
 
Halafu hapo ole wako uonekane unahangaika na nyama tu.
Mkono/kiganja kitakamatwa halafu kitakung'utwa kupukutisha punje za wali, halafu kitalambwa, baadae kitasuguliwa mavumbini....wakishamaliza hivyo wanakuaambia ujikate.
hahahahahahahaaaaaaa mkuu umenikumbusha mbaaali sana kuna siku ilikuwa maulid kwa jiran bwana wee nilikaa na wazee si unajua wanavyoheshimiana hawakuanza na nyama basi mi nikashughulika nazo nilikolewa konzi hilo nilihisi naaga dunia sikurudiaga tena madude yao hayo
 
Back
Top Bottom