Kutoka kuwa kondakta mpaka uwaziri

Kutoka kuwa kondakta mpaka uwaziri

Mbesigwe

Member
Joined
Sep 27, 2016
Posts
51
Reaction score
54
George Boniface Simbachawene amezaliwa tarehe 5 mwezi Julai mwaka 1968, katika wilaya ya Mpwapwa, iliyopo mkoani Dodoma. Ni mwanasiasa kutoka chama cha Mapinduzi CCM, amekuwa mbunge wa Bunge la Tanzania tangu mwaka 2005 hadi sasa. Kwa Sasa ni Waziri wa nchi, ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa umma na Utawala Bora.
.
Alihitimu darasa la saba Shule ya Msingi ya Mahomanyika iliyoko mkoani Dodoma mwaka 1982. 1988 Alihitimu elimu ya sekondari pale Mazengo dodoma. Na mwaka 1993 Alihitimu elimu ya cheti Cha ufundi, Arusha. Mwaka 2001 hadi 2005 aljiunga na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) ambako alitunukiwa shahada ya kwanza ya sheria (LLB).
.
Baada ya kuhitimu na kubobea katika masuala ya ufundi, ilimchukua miaka miwili kabla ya kuajiriwa na kampuni ya mabasi ya Urafiki, tawi la Dodoma mwaka 1995. Alikuwa kondakta, meneja wa kitengo cha ufundi na ofisa usafiri. Mwaka 1997 hadi 1998 aliajiriwa na Kituo cha Mafunzo ya Ufundi cha Future World akiwa mwalimu. Kati ya kipindi hicho hadi mwaka 2000, alifanya kazi kama mkurugenzi mtendaji wa shirika la kiislamu la Muzdalifa linalojishughulisha na masuala ya misaada.
.
Amewahi pia kuwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini na wa Nyumba na Makazi. Januari 2015 alipandishwa na kuwa Waziri wa Nishati na Madini. Hayati Magufuli alipotangaza baraza lake mwaka 2015, Simbachawene alipangwa Tamisemi akiwa waziri.Januari 23, 2020 chini ya uongozi wa Hayati Magufuli, aliteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya ndani akichukua nafasi ya Kangi Lugola. Na baada ya uchaguzi wa 2020 aliendelea hapo hapo mambo ya ndani.
.
Sifa nyingine kubwa ya Simbachawene ni subira. Watendaji ambao wamefanya kazi naye Wizara ya Nishati na Madini , TAMISEMI na Wizara ya Mambo ya ndani wanamsifu kuwa ni mtu mwenye kuuliza kila jambo analotaka kuamua, lakini pia anawasikiliza sana watendaji na wataalamu. Haiba hii huenda ndiyo imesababisha hadi leo hii Simbachawene ameendelea kuwa na ‘namba ya uhakika’ kwenye mabaraza ya mawaziri. Kuna mengi sana ya kujifunza kwake hasa Kwa vijana ambao Bado tunatafuta kutoboa.

Credits TanzaniaWeb
509299799.jpg
 
Ila jamaa Yuki humble Sana ,ni mtu asiye na papala ,huyu jamaa kiti Cha urais hakimpyai .sema ndo hivyo kile chama kina wenyewe!!
 
Lesson.....makondakta msikate tamaa kuna siku mtakua mawaziri.
Tanzania kuna raha.
Nakumbuka wakati nikiwa mwaka wa KWANZA Chuo,...nilipata Bahati ya kujitolea kufanya Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa KITENGO cha Uhasibu/ IDARA ya Fedha.

Tulikua tukienda kukusanya ushuru wa mahoteli, mazao, minada, samaki, etc ( CHAMSISILI, KIBAKWE, MTERA , PWAGA, LUMUMA etc)

Tulivyokua tukifika kwà kina Simbachawene,...wakawa wanatuambia ," Je mnaweza kuzihesabu hizo ng'ombe zote? "

Kiufupi zilikua nyingi sana...jamaa wakawa wanatupa sh. 90k

Afu nilisikia pia, ngo'mbe zao zimewekewa MITISHAMBA,..mtu akiziiba anakua anazunguka pale pale....au anaweza kwenda na akazirudisha tena yeye mwenyewe.
 
Nakumbuka wakati nikiwa mwaka wa KWANZA Chuo,...nilipata Bahati ya kujitolea kufanya Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa KITENGO cha Uhasibu/ IDARA ya Fedha.

Tulikua tukienda kukusanya ushuru wa mahoteli, minada, samaki, etc

Tulivyokua tukifika kwà kina Simbachawene,...wakawa wanatuambia ," Je mnaweza kuzihesabu hizo ng'ombe zote? "

Kiufupi zilikua nyingi sana...jamaa wakawa wanatupa sh. 90k

Afu nilisikia pia, ngo'mbe zao zimewekewa dawa,..mtu akiziiba anakua anazunguka pale pale....au anaweza kwenda na akazirudisha tena yeye mwenyewe.
Motivesheno spika wanatuona sisi watoto....
 
Back
Top Bottom