Kutoka kuwa kondakta mpaka uwaziri

Kutoka kuwa kondakta mpaka uwaziri

George Boniface Simbachawene amezaliwa tarehe 5 mwezi Julai mwaka 1968, katika wilaya ya Mpwapwa, iliyopo mkoani Dodoma. Ni mwanasiasa kutoka chama cha Mapinduzi CCM, amekuwa mbunge wa Bunge la Tanzania tangu mwaka 2005 hadi sasa. Kwa Sasa ni Waziri wa nchi, ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa umma na Utawala Bora.
.
Alihitimu darasa la saba Shule ya Msingi ya Mahomanyika iliyoko mkoani Dodoma mwaka 1982. 1988 Alihitimu elimu ya sekondari pale Mazengo dodoma. Na mwaka 1993 Alihitimu elimu ya cheti Cha ufundi, Arusha. Mwaka 2001 hadi 2005 aljiunga na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) ambako alitunukiwa shahada ya kwanza ya sheria (LLB).
.
Baada ya kuhitimu na kubobea katika masuala ya ufundi, ilimchukua miaka miwili kabla ya kuajiriwa na kampuni ya mabasi ya Urafiki, tawi la Dodoma mwaka 1995. Alikuwa kondakta, meneja wa kitengo cha ufundi na ofisa usafiri. Mwaka 1997 hadi 1998 aliajiriwa na Kituo cha Mafunzo ya Ufundi cha Future World akiwa mwalimu. Kati ya kipindi hicho hadi mwaka 2000, alifanya kazi kama mkurugenzi mtendaji wa shirika la kiislamu la Muzdalifa linalojishughulisha na masuala ya misaada.
.
Amewahi pia kuwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini na wa Nyumba na Makazi. Januari 2015 alipandishwa na kuwa Waziri wa Nishati na Madini. Hayati Magufuli alipotangaza baraza lake mwaka 2015, Simbachawene alipangwa Tamisemi akiwa waziri.Januari 23, 2020 chini ya uongozi wa Hayati Magufuli, aliteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya ndani akichukua nafasi ya Kangi Lugola. Na baada ya uchaguzi wa 2020 aliendelea hapo hapo mambo ya ndani.
.
Sifa nyingine kubwa ya Simbachawene ni subira. Watendaji ambao wamefanya kazi naye Wizara ya Nishati na Madini , TAMISEMI na Wizara ya Mambo ya ndani wanamsifu kuwa ni mtu mwenye kuuliza kila jambo analotaka kuamua, lakini pia anawasikiliza sana watendaji na wataalamu. Haiba hii huenda ndiyo imesababisha hadi leo hii Simbachawene ameendelea kuwa na ‘namba ya uhakika’ kwenye mabaraza ya mawaziri. Kuna mengi sana ya kujifunza kwake hasa Kwa vijana ambao Bado tunatafuta kutoboa.

Credits TanzaniaWeb
​
View attachment 2597037
Haha haha mwambie yeye si kagoma kutoa mkeka wa database, tuna Imani na Mama, atatuletea anae jali maslahi ya vijana
 
Sifa ya Simbachawene ni kukaa kimya wakati wa kula. Pia huwa sio mnoko wengine wakiwa wanakula. Ka-fit vizuri kwenye ile kanuni ya kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake. Ni mtu muhimu sana. Hana mawenge ya kifala. Yeye kaamua tu ku-fit kwenye system hana mambo mengi.
 
Jamaa anautaka URAIS sana.

Lakini anasahau ya kwamba, Watanzania hawapendi viongozi wenye testacles zenye mayai yenye watoto watukutu.

Kama atalingundua hilo mapema, namshauri ajifanye kama Aldof Hitler...( Ajihasi hizo testacles)
Nec kura kaambulia 1 , huo uraisi unaupataj?🤣
 
Kweli Vita vya Urais Tanzania imepambana Moto.

Bado yule aliyeko Jikoni anayelinda Kibubu cha Nchi naye kuja kutueleza namna alivyotoka kuwa Mfugaji wa Ng'ombe hadi kuwa Mtunza Fedha wa Nchi.
Na Sasa anamiliki mabasi , timu ya Mpira wa miguu, endeleea
 
Na Sasa anamiliki mabasi , timu ya Mpira wa miguu, endeleea
Hahahaha.....................mwache mtoto wa Mfugaji aje aupate Urais, huenda mabomba yetu yakawa yanatoa maziwa 🤪
 
Hahahaha.....................mwache mtoto wa Mfugaji aje aupate Urais, huenda mabomba yetu yakawa yanatoa maziwa 🤪
Kwa haki iliyoko Serikalin ss sio shwari kabisaaa, mawaziri wanafanya wanavyotaka
 
Back
Top Bottom