Kutoka kuwa kondakta mpaka uwaziri

Kutoka kuwa kondakta mpaka uwaziri

Hata wewe unaweza zaa mtoto mtukutu.
Mfumo wangu wa Uzazi umeunganishwa na Neno la Mungu.

Watoto wangu sio mali yangu bali ni mali ya Mungu. Nikijidanganya kuwa ni mali yangu...watakua wa Ulimwengu huu ( watukutu a.k.a watoto wasiokua na maadili )
 
George Boniface Simbachawene amezaliwa tarehe 5 mwezi Julai mwaka 1968, katika wilaya ya Mpwapwa, iliyopo mkoani Dodoma. Ni mwanasiasa kutoka chama cha Mapinduzi CCM, amekuwa mbunge wa Bunge la Tanzania tangu mwaka 2005 hadi sasa. Kwa Sasa ni Waziri wa nchi, ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa umma na Utawala Bora.
.
Alihitimu darasa la saba Shule ya Msingi ya Mahomanyika iliyoko mkoani Dodoma mwaka 1982. 1988 Alihitimu elimu ya sekondari pale Mazengo dodoma. Na mwaka 1993 Alihitimu elimu ya cheti Cha ufundi, Arusha. Mwaka 2001 hadi 2005 aljiunga na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) ambako alitunukiwa shahada ya kwanza ya sheria (LLB).
.
Baada ya kuhitimu na kubobea katika masuala ya ufundi, ilimchukua miaka miwili kabla ya kuajiriwa na kampuni ya mabasi ya Urafiki, tawi la Dodoma mwaka 1995. Alikuwa kondakta, meneja wa kitengo cha ufundi na ofisa usafiri. Mwaka 1997 hadi 1998 aliajiriwa na Kituo cha Mafunzo ya Ufundi cha Future World akiwa mwalimu. Kati ya kipindi hicho hadi mwaka 2000, alifanya kazi kama mkurugenzi mtendaji wa shirika la kiislamu la Muzdalifa linalojishughulisha na masuala ya misaada.
.
Amewahi pia kuwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini na wa Nyumba na Makazi. Januari 2015 alipandishwa na kuwa Waziri wa Nishati na Madini. Hayati Magufuli alipotangaza baraza lake mwaka 2015, Simbachawene alipangwa Tamisemi akiwa waziri.Januari 23, 2020 chini ya uongozi wa Hayati Magufuli, aliteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya ndani akichukua nafasi ya Kangi Lugola. Na baada ya uchaguzi wa 2020 aliendelea hapo hapo mambo ya ndani.
.
Sifa nyingine kubwa ya Simbachawene ni subira. Watendaji ambao wamefanya kazi naye Wizara ya Nishati na Madini , TAMISEMI na Wizara ya Mambo ya ndani wanamsifu kuwa ni mtu mwenye kuuliza kila jambo analotaka kuamua, lakini pia anawasikiliza sana watendaji na wataalamu. Haiba hii huenda ndiyo imesababisha hadi leo hii Simbachawene ameendelea kuwa na ‘namba ya uhakika’ kwenye mabaraza ya mawaziri. Kuna mengi sana ya kujifunza kwake hasa Kwa vijana ambao Bado tunatafuta kutoboa.

Credits TanzaniaWeb
View attachment 2597037
So, impressive.
Fupi lakini nzuri.
Inatia sana moyo hasa kwa wanaojitafuta.
Hakuna kukata tamaa mpaka kieleweke.
 
Kwahiyo kuna nini kwani? Wapo mawaziri waliowahi hadi kuwa wamachinga nk; kwahiyo tufanyeje sasa, au wengine wanazaliwaga mawaziri?
 
Mfumo wangu wa Uzazi umeunganishwa na Neno la Mungu.

Watoto wangu sio mali yangu bali ni mali ya Mungu. Nikijidanganya kuwa ni mali yangu...watakua wa Ulimwengu huu ( watukutu a.k.a watoto wasiokua na maadili )
Hata watoto wa samweli walimshinda walikua na tabia mbaya, same kwa wajukuu wa Daudi
 
Tukianza kila mtu aielezee historia yake hapa sizan kama hii hostoria itakuwa hata ktk top 10. Itoshe tu kusema umempigia chapuo inatosha
 
Hata watoto wa samweli walimshinda walikua na tabia mbaya, same kwa wajukuu wa Daudi
Biblia/ Quran ni kama Marking Scheme ya maisha. Ndani yake kuna watu wema na wabaya.

It is all about mistakes & errors

Wapo waliokua wema...wakafanya mabaya na wakaya correct. Na kuna wengine walinyooka kwà kuwa na msimamo thabiti.

So it depends unataka / umechagua kufuata mfano wa kuishi kama nani ili wewe na kizazi chako muwe salama.

AND I tell you...ukichagua kuwa Jesusfied....lazima bloodline Yako itakua salama wakati wote.
 
Back
Top Bottom