Kutoka Kikao cha UKAWA

Naona kutujuza yaliyojiri kule vimeshindikana kazi kupeana umwamba au mkutano bado
 
najua huwezi kuelewa maana Akili kubwa ikiongozwa na Akili ndogo Utaelewa vipi?

Eheeeee nacheka nakufurahi kwa wakati mmoja kicheko cha machozi........Mkandara unachomwambia huyu na wana Ukawa kwa lugha nyepesi wasio jitambua labda wewe unamaanisha ama unawaambia matamko aka kauri mbiu au iweje vile wanavyosema au watakavyo sema maneno msukumo hayo au maneno hamasishi unaposema Uzanzibar /Utanganyika na Utanzania ni sawa na kusema Ukenya/Uburundi/Unyarwanda /Uganda na Ukamalizia Ueastafrica.

Yani ndio kusema hapo hapo unaamasisha kuwa unataka kuwa na UMOJA na UNDUNGU kama UKOO au FAMILIA lakini unatamka kutokutambua kwa kuhamasisha WATU WATAMBUANE kwa kuhamasisha ukaribu wao uwe ni kwa kusema huyu wa UJOMBANI, huyu wa UKWENI,Huyu wa UMAMANI, huyu wa UBABANI....kwanini usiseme huyu wa UKOO wangu ni binamu yangu, ni mkwe wangu, dada yangu, ni shangazi yangu, ni mjomba wangu nk.

Unapotaja UZANZIBAR/UTANGANYIKA NA UTANZANIA unahamasisha UTAIFA [Kitu ambacho ni Sumu] katika madaraja. Wakati MFUMO WA SERIKALI TATU haumaanishi kutambua WATU KWA UTAIFA WAO bali unatambua TAASISI TATU Ndani ya Ushirika mmoja.

Ndio maana akasema wakati wanapanga hiyo kauli mbiu [Slogan] walikuwa wanawaza nini?Hivi kweli ni kweli au ni Blabla za Mlopokaji.....na kama nik kweli basi msemaji mkuu wa CDM/UKAWA humu JF asije na neno hilo la UZANZIBAR/UTANGANYIKA NA UTANZANIA kulitambulisha kama Kuali mbiu....ndio kusema wanahamasisha sumu ya MATENGAMANO na sio Serikali tatu.

Mimi ni muumini wa Serikali tatu baada ya kujilizisha, mwanzoni nilikuwa muumini wa Serikali moja...lakini kwa maelezo ya Warioba na Tume yake na hali halisia nilijilizisha na kusimama kwenye tatu.Lakini kwa Matamshi hayo ya Ukawa kwangu yana maana nyingine kabisa katika kuhamasisha umma kwenye ujenzi wa Taifa la Tanzania kwa mfumo wa Serkai tatu

Kifupi Mkandara anasema mnahamasisha UZANZIBAR -TAIFA /UTANGINYIKA -TAIFA. Lakini TANZANIA TAIFA aliwezi kuwepo bila ya hizo mbili tajwa.Mtu wa kawaida anataka vitendea kazi kama mifumo -yani Serikali Zanzibar na Serikali Tanganyika huku Serikalihizo zikiwa chini ya Serikali Tanzania bila kujitanabaisha mie Mzanzibar, au Mie Mtanganyika.

Mwalimu anasema huyu Mzanzi-Bar huyu Mzanzi-Bara..................Kesho mtasema Upemba na Unguja.........hatujui kesho kama sio Ukristu ama Uislamu....aahaha CDM msikurupuke Analysis ni kitu muhimu sana kwenye mambo nyeti [Sensitive] kama haya msichafue hali ya hewa ya status yenu.
 
Sijawahi kuwa Chadema eeeh! sawa mkuu. Na ebu nambie ni lini mimi hapa nimepingana na Mbowe zaidi ya kusema kwamba anajazwa Ujinga na kundi la wachumia tumbo. Nimeandika mengi humu kuhusu Mbowe kiasi cha kusema wazi kwamba Mbowe ni kiongozi mzuri na hata kufikia kuwafananisha yeye na Zitto.

Niliwahi sema humu Mbowe ni mwanasiasa lakini Zitto bado hajakomaa kisiasa ila anaweza kuwa kiongozi mzuri wa serikali hata Urais. na nikasema Mbowe hawezi kuwa rais kutokana na yeye mwenyewe kutokubalika kama Zitto ambavyo asingeweza kuwa mwenyekiti wa Chadema kwa sababu hakubaliki. Muulize Sikonge nani alokuwa na hoja ya kwanza kabisa humu JF kuwa Slaa agombee Urais? hadi akaiweka mada nzima juu ya kumpigia kura za ndiyo. Muuulize hata huyo Mbowe mwenyewe akwambie msimamo wangu anajua sifuati mtu wala sibabaiki...

Nachokichukia ni Chadema kutoka katika misingi iloanzishwa na kukuzwa katika malezi ya Mbowe mwenyewe akisaidiwa na Slaa na Zitto lakini toka hawa wanafiki wakubwa kuingia mule wamejiona wao ndio wajuaji kupitiliza na bila shaka wametumwa. Sii wanasiasa sii lolote ni wachumia tumbo wanaotafuta umaarufu tu na wengine sasa michavu inawatoka ndio wanajiona wao ni wao. Pambaf kabisa watu hawa ni majangili ambao sitowasamehe hata kwa nini...Na mtakuja ipata sii leo wala kesho lakini nalolisema mtakuja liona wenyewe mbeleni.
 
hoja mfu siku zote humwangusha mtu, na hoja makini humwinua juu!
-mkandara kama una vihoja mfu kama hivi unadhani waweza mshawishi nani akubaliane na wewe?
-Ikiwa chamani A.C.T ZITTO ndiye alfa na omega huoni huo ni mwanzo mbaya wa kesho muitakayo? .
muungano ni ulazima wa wana bara na wana zanzibar kwa kuukubali ama kuukataa.
-swali dogo
>>ikiwa katiba pendekezwa hii ni maoni yetu kwanini serikali itushawishi kwa kampeni zitakazogharimu fedha nyingi?.
>>ikiwa muungano unapendwa na kukubalika na wa TANGANYIKA NA WA ZANZIBARI kwanini mwanasheria mkuu alipinga baadhi ya vipengele vya muungano kwa katiba yao hii pendekezwa,na pia ni kipi ambacho unataka kutushawishi wa bara na visiwani ikiwa MUUNGANO HUU MFU UMEKUWA NA KERO LUKUKI NA ZISIZO TATULIKA MIONGO NA MIONGO?


*mkandara acha usanii kama wasanii kijana!
 
Umenena ukweli mtupu mwanakwetu! chukua "like 5".
 
Huyu mleta mada anajiabisha kwa kutumia jina la Nyerere--Nyerere mwenyewe mwenye jina lake hakuwa kama huyu hamnazo!
 
Acheni uongo utawezaje kuwa na Undugu Na Mkenya kwa kutumia EAC. Huu ni umoja wa maridhiano katika maswala kadhaa na zinaweza kupigwa hata kesho tukafukuzana kama wanyama. Muungano ni kuunganisha WATU kuwa kitu kimoja sio vitu. Community ni jamii inaweza kuwa hata dunia nzima lakini hakuna Undugu hapo ni UTU wetu iwe mzungu, Mchina na kadhalika ni kutambua Ubinadamu ktk makundi yake hakuna udugu hapo.

Acheni kujaribu watu na kiswahili kibovu kama cha UKAWA ati UZANZIBAR na UTANGANYIKA ambao wao wanataka tuamini ati kuna Udugu baina yao kwa kuunda UKAWA wakati tunajua kabisa hakuna udugu hapo ni urafiki wa kinafiki kutafuta maslahi tu. Kama kweli wanataka kuungana wangetuononyesha kuungana ni kupi leo hii wasingekwua wanagombania Majimbo na Urais. Lini serikali ikawa ya UTanganyika au UZanzibar katika Muungano yaani wewe kesho huwezi kuhamia New York State kwa sababu unatoka Maryland ndio umoja huo?

Hawa nimewasoma hivi. Chadema inajua haikubaliki Zanzibar wanapigania Utanganyika. na CUF wanajua hawakubaliki bara wanapigania UZANZIBAR, huyo NCCR anaganja njaa tu humo kusikilizia upepo halafu wachepukie CCM. Sasa wanatafuta muafaka ili wachukue madaraka kisha wagawane Chako Chako, Changu Changu!..badala ya kuunganisha nguvu zao kwa UMOJA wao waiongoze Tanzania nzima. Kwao kutugawa ni sababu ni Waumini wa SEPARATION badala ya INTEGRATION hilo halifichiki na sio Chadema niloijua mimi..Siko nao na sintokuwa nao na nadhani ndio maana wanaifanya siri kumbe sisi wengine huwasoma baina ya maneno ya mtu..
 
UKAWA ni kikundi kilichoundwa kimagumashi!

Hakina protokali, kila mmoja ni msemaji wake!
 
Wewe nambie Muungano wowote usokuwa na Kero hapa duniani, nipe hata mmoja tu. Hizo ndoa zetu wenyewe zina kero, familia zina kero ndio uvunje udugu kwa sababu ya kero au unaitafutia suluhu. Akili ndogo jamani sheeedah! hakuna muungano wa aina yoyote hapa duniani usokuwa na changamoto zake - HAKUNA.. na huwezi vunja muungano kwa sababu ya kero..
 
mtanzania litangazwe rasmi kuwa adui namba moja wa chadema na ukawa, wanatunga mno!
mtanzania haliwezi acha vituko na kuonyesha sinema hii mana mharii kanunuliwa kwa bei chee kaacha kuwa mzalendo kwa taifa lake
 
UKAWA ni kikundi kilichoundwa kimagumashi!

Hakina protokali, kila mmoja ni msemaji wake!

wewe huwa nakuambia siku zote akili yako ni sawa na mabata yale yanachezea matope,au wale wanaume wanao jiuza! haiwezekani mwanaume mzima uposti kitoto hivyo,ukawa upo imara wala hautetereki.
 

Niliko bold wewe naye hapo umechemka nenda Tarime kamwambia maneno yako hayo Mkurya na Mluo uone atakachokufanya kama sio Panga ya Shingo kusambaratisha ubongo wako kisha utume dola ya Tanzana imtafute kama itampata nitajua wewe ni Mwanaume wa Shoka [Wao wanasema wewe ni Mumura]

Nenda Moshi mpakani mwa Tanzania na Kenya -Taita Taveta Ukaseme maneno yako hayo uone kile wachaga watakufanya hakuna rangi utaacha ona chariii.

Nenda Manyovu -Gasulu kisha waambie Waha na Warundi habari yako hiyo wakati Mwenyekiti wa Chama fododo Burundi mama yake Muha wa Kigoma sema maneno yako hayo kwa Waha na Wamanyema uone watakavyo kukokomora-Kama ujui kukomora nenda Mpakani Mwa Unganda na Mtukura kakutane na Warembo wa Kihaya wenye miguu chupa ya bia, tangaza ndoa kisha sikia atachokwambia kuwa mjiandae kuvuka mpaka mwende kwa Mjomba wake yuko Kampara ni Askari Jeshi mwende akawape Baraka zake kuwa unamuwowa binti yake.

Kwa hilo Keep Quite ujui unaloongea ....nawe kajifunze MASHIRIKIANO YANAANZAJE..hata Zanzibar biashara za Utumwa na biashara za Pembe kutoka Congo, Kigoma na Tabora miaka ile zilipelekea Waha , Wanyamwezi kuamia Zanzibar na makabila mengine kama Wanyasa, Wamakonde na Wangoni kuamia pia Zanzibar na leo kwa unasaba huo wa mashirikiano hata kabla ya ujio wa Wajerumani na Waingereza umekuwepo ambao ni sawa na Wakurya wa Tanzania na Watende wa Kenya, Wamanyema wa Kigoma na Wamanyema Burundi, Waangaza wa Tanzania na Wanayonkore wa Uganda, leo POVU mdomoni lakutoka kutetea MUUUNGANO WA WATU ujui ulianzaje Mkandara nawe kajifunze usipopome hapa.

Tena Mkandara ni waha nastaajabu wewe ni muha wa wapi ata mama Njerekela wa manyovu mpakani umujui....Jewe wewe wawapi yeheeee.
 
Huyu mleta mada anajiabisha kwa kutumia jina la Nyerere--Nyerere mwenyewe mwenye jina lake hakuwa kama huyu hamnazo!

wee ---- tulia sindano ikuingie mana mmezoea mada za kuisambaratisha ukawa na huku mnajua ni uwongo mtupu.sasa miezi inasonga mnahangaika na ukawa wakati nyie hamjapata hata mgombea.
 
wewe huwa nakuambia siku zote akili yako ni sawa na mabata yale yanachezea matope,au wale wanaume wanao jiuza! haiwezekani mwanaume mzima uposti kitoto hivyo,ukawa upo imara wala hautetereki.
Kwahiyo Yeriko ndio msemaji wa UKAWA? Kamanda jifunze siasa! acha dharau!
 
Ukisha yataja makabila tayari umesha watenganisha hakuna udugu pale ni ujirani mwema hata Marekani na Canada wao ujirani mwema hawana udugu. Ukiweza kutenganisha haya itakusaidia katika maamuzi yako ama kujenga hoja..
 

Kwahiyo CCM wanataka kujiunga UKAWa?!, ACT=CCM.
 
Kazi kwelikweli, kwahio unadhani tunaweza tegemea mgombea urais atoke nje ya CDM? Haya bwana ila wazalendo hawafi moyo na kusambaza uzalendo

Wazalendo huwa hawajitangaji bali matendo yao ndiyo huwafanya watu wawaite wazalendo. Mfano akina Nyerere, Sokoine, Karume n.k hawa hawakuwahi kupanda majukwaani na kujitangaza kuwa wao wazalendo,ila vitendo vyao ndivyo viliwafanya Watanzania wawaite wazalendo. Sasa nyie ACT uzalendo wenu wa kujitangaza huo kwanza jina la chama chenu tu lipo kwa lugha ambayo si kizalendo "Alliance for Change and Transparency", sasa hapo uzalendo upo wapi? bora hata CCM jina la kizalendo. Uzalendo huanza na lugha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…