Jamhuri ya Zanzibar
Senior Member
- Jul 17, 2012
- 127
- 195
Wazanzibari wanadai mamlaka kamili ya nchi yaoMazruiMediaLive on USTREAM: We are broadcasting live from MazruiMedia Studio!. Local News
Mkutano mkubwa uliovuta hisia za wananchi wengi wa Visiwa vya Unguja na Pemba umefanyika leo hapa Unguja eneo la Kibanda Maiti. Mkutano huo uliokuwa ukitangazwa na vituo kadhaa vya radio hapa Visiwani imehudhuriwa na viongozi na watu maarufu hapa Zanzibar, huku Maalim Seif akiwa mzungumzaji mkubwa katika mkutano huo. Agenda ikiwa ni Muungano na Mamlaka kamili ya nchi ya Zanzibar.
Miongoni mwa mambo yalizungumzwa ni
1. Zanzibar kuwa na Serikali huru na yenye mamlaka kamili
2. Kuwa na Baraza lake la Mitihani - kwa madai kuwa NECTA inawafelisha Wazanzibar
3. Mamlaka ya huru ya Mapato na TRA kutokuwa na mamlaka ndani ya Zanzibar
4.Zanzibar kuwa na fedha yake - na sio kutumia shilingi ya Tanzania
5.Tume ya Uchaguzi yaani NEC na msajili wa Vyama kwa Zanzibar pekee
6. Zanzibar kuachiwa rasilimali zake
7. Wizara ya Mambo ya Ndani yake na wala sio ya MUungano
6.Wizara ya Fedha
7. Kushughulikia mambo yake ya kimataifa yenyewe
8. Kuwa na sera ya dini kwa sababu Zanzibar ni nchi ya Kiislam.
9.Kuwa na Bunge lake lenye mamlaka kamili
10. Kuwa na katiba yake ambayo haingiliani na katiba ya JMT
Madai mengi yametoa mwanga kwamba Wazanzibari wanaonewa na kunyanyaswa kwa sababu ya ujanja wa Mwl.Julius Kambarage Nyerere.
Kwa hapa Zanzibar, mazungumzo katika vijiwe vyote maarufu kama Jaws Corner, Malindi na Mkunazini ni habari ya Zanzibar Huru.............