beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,877
- 6,326
Akizungumza kutoka Ikulu amesema, "Nilimwambia Rais Magufuli kama inawezekana ningependa kushikilia koti lake tu ili anapokimbia aweze kunivuta nami niende haraka kwa kasi yake"
Rais Lazarus Chakwera amesema yeye na Rais Magufuli wamekuwa na mazungumzo ya muda mrefu na wamekuwa na mambo mbalimbali ambayo yanaweza kuendeleza Tanzania na Malawi
Aidha, Rais John Magufuli amesema mataifa hayo yamekuwa marafiki tangu ukoloni, na hata aliyepandisha bendera kwenye Mlima Kilimanjaro baada ya Uhuru alikuwa na asili ya Malawi
Amesema kuna Makampuni 8 kutoka Malawi ambayo yamewekeza nchini na kuajiri Watanzania 390 hadi sasa. Amewapongeza wananchi wa Malawi kwa Rais Chakwera na kuwahikishia Watanzania wapo pamoja nao