Kutoka Ikulu, Dar: Rais Chakwera amfagilia Rais Magufuli, atamani kushikilia koti lake ili aende kwa kasi yake

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
1602070903225.png


Akizungumza kutoka Ikulu amesema, "Nilimwambia Rais Magufuli kama inawezekana ningependa kushikilia koti lake tu ili anapokimbia aweze kunivuta nami niende haraka kwa kasi yake"

Rais Lazarus Chakwera amesema yeye na Rais Magufuli wamekuwa na mazungumzo ya muda mrefu na wamekuwa na mambo mbalimbali ambayo yanaweza kuendeleza Tanzania na Malawi

Aidha, Rais John Magufuli amesema mataifa hayo yamekuwa marafiki tangu ukoloni, na hata aliyepandisha bendera kwenye Mlima Kilimanjaro baada ya Uhuru alikuwa na asili ya Malawi

Amesema kuna Makampuni 8 kutoka Malawi ambayo yamewekeza nchini na kuajiri Watanzania 390 hadi sasa. Amewapongeza wananchi wa Malawi kwa Rais Chakwera na kuwahikishia Watanzania wapo pamoja nao



1602070934680.png


1602070971863.png
 
Lisu akiiona hiyo picha anatamani kujirusha kwenye magorofa ya kwao ubelgiji kwa kuchanganyikiwa

Haya Chakwera huyo Chadema mliyekuwa kutwa mnasifia anamsifia Magufuli
Tundu yuko karakoo kaenda kununua matumizi yake muhimu nimemuona kwa wasiotaka hata kumsikia wakimsongasonga
 
Lisu akiiona hiyo picha anatamani kujirusha kwenye magorofa ya kwao ubelgiji kwa kuchanganyikiwa

Haya Chakwera huyo Chadema mliyekuwa kutwa mnasifia anamsifia Magufuli
Helewa kuwa chakwera alikuwa mpinzani miezi 3 iliyopita, wala hawana chakuongea labda kama angekutana na Lissu pamgenoga, Zanu pf ndio size ya ccm
 
Helewa kuwa chakwera alikuwa mpinzani miezi 3 iliyopita, wala hawana chakuongea labda kama angekutana na Lissu pamgenoga, Zanu pf ndio size ya ccm
Chakwera alikua Chama tawala wakazembea upinzani ukaingia na kuwavuruga ila sasa wamerudisha dola mkononi.
Ni vizuri kujifunza ila sio vizuri kufanya majaribio ya kuongoza..... sisi watanzania hatutadanganyika kama wamalawi
 
Nina wasiwasi na ujio wa huyu Malawi presidaa, uenda kuna secret agenda ambayo amekuja kumpa kilanja wetu kutokana na muelekeo wa uchaguzi hapa Tanzania.

ikumbukwe huyu Chakwera ni kutoka chama cha upinzani so kwa mtizamo wa haraka haraka i see something behind the president curtain.
 
Miafrika ndivyo tulivyo shenzi, lenyewe limeingia madarakani kwa nguvu ya umma na mahakama huru Leo linashangilia MTU anayeua Uhuru was mahakama, demokrasia
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom