Kutoka Ikulu, Dar: Rais Chakwera amfagilia Rais Magufuli, atamani kushikilia koti lake ili aende kwa kasi yake

Lissu akiiona hiyo picha anatamani kujirusha kwenye magorofa ya kwao ubelgiji kwa kuchanganyikiwa

Haya Chakwera huyo Chadema mliyekuwa kutwa mnasifia anamsifia Magufuli

Kuna kusifia na kupaka mafuta kwa mgongo wa chupa.
 
Aangalie kushikilia koti la mtekaji , mauaji , mpotezaji watu , mkiukaji haki za binadamu, mvunjaji katiba na sheria , Angalie mwenzie njia kuelekea ICC nyeupe anasubiri siku tu akaangwe .
 
Chakwera alikua Chama tawala wakazembea upinzani ukaingia na kuwavuruga ila sasa wamerudisha dola mkononi.
Ni vizuri kujifunza ila sio vizuri kufanya majaribio ya kuongoza..... sisi watanzania hatutadanganyika kama wamalawi
Aliyekwambia chama kikaa sana madarakani kinaleta maendeleo ni nani huyo?
 
Rais wa Malawi amekuja kuongea na Mh Magufuli ili kupush uwekezaji wao mkubwa unaosuasua wanaotarajia kuufanya katika sekta ya kibenki nchini.

National Bank Of Malawi ( NBM) ipo katika mchakato wa kununua hisa zaidi ya 75% katika moja ya benki hapa Tz na mchakato umekuwa wa kusuasua takribani mwezi wa tano sasa, na BOT ndio imekuwa ikisubiriwa kwa muda wote kuapprove mchakato huo ambapo mpaka sasa inasemekana mamlaka kutoka ngazi za juu ndio imeshikilia 'approval' hio

Hvyo imemlazimu Rais wa Malawi afunge safari kuja kuongea na mkubwa mwenzake kulainisha mambo
 
"Nilimwambia Rais Magufuli kama inawezekana ningependa kushikilia koti lake tu ili anapokimbia aweze kunivuta nami niende haraka kwa kasi yake" - Lazarus Chakwera
 
NATAMANI KULISHIKA KOTI LA RAIS JOHN MAGUFULI ILI ANAPOKIMBIA,NIKIMBIE NAE PAMOJA-RAIS LAZARUS CHAKWERA.

Leo 19:20hrs 07/10/2020

Rais Lazarus Chakwera akimpongeza Rais John Magufuli kwa kuipeleka Tanzania katika Uchumi wa kati,amesema Rais Magufuli ni mfano wake katika Utendaji kazi na angependa amshike koti ili anapokimbia Rais Magufuli nae Rais Chakwera akimbie,

Rais Chakwera amepongeza pato la taifa linalotokana na biashara,miundo mbinu ambayo Rais Magufuli ameijenga,na thamani ya Taifa la Tanzania kwa sasa ukiligawa na idadi ya watu unapata thamani ya hela ambayo inalipeleka Taifa la Tanzania kwenye Uchumi wa kati,

Rais Chakwera amesema Taifa la Malawi na Taifa la Tanzania yanaendesha miradi ya pamoja ya miundombinu, miongoni mwake vituo vya pamoja vya biashara na ukaguzi wa mpakani vilivyoko Songwe na Kasumulo, ukanda wa Mtwara, na pia katika bonde la Mto Songwe,

Rais Chakwera amesema mataifa haya jirani ya Tanzania na Malawi ambayo raia wake wanapatikana kwa wingi sehemu zote mbili,yanashabihiana na yana undugu na yanakubaliana kwa mengi,Sisi ni ndugu kila siku utapishana na Mmalawi pale Kariakoo,vile utakuta Watanzania kule Blantyre,

Rais Chakwera amesema Njombe kwake ni nyumbani,Sisi Malawi na Tanzania ni marafiki wa chanda na pete na urafiki wetu umeasisiwa tangu wakati wa utawala wa kikoloni na uhusiano huu umeendelea kuimarika hadi wakati huu ambako mataifa yote yamepindukia kipindi cha miaka 50 ya uhuru.

Rais Chakware amesema kuna umuhimu mkubwa wa nchi za Afrika kuanza kujitambulisha upya kuhusu demokrasia wanayotaka,hakuna haja tena kuendelea kukumbatia demokrasia inayotoka nje ya mipaka ya bara hili kwa kualika waangalizi wa kimataifa ambao mara zote ripoti zao haziakisi moja kwa moja matakwa ya kiafrika bali matakwa ya mabepari mabeberu,

Nimalizie kwa kukukaribisha Rais Lazarus Chakwera katika nchi ya amani,nchi ya kihistoria katika Ukombozi wa nchi za kusini mwa Afrika SADC,karibu kwa Taifa la Shujaa wa Afrika,Mwalimu Julius Nyerere,Karibu sana Tanzania,kama lilivyo jina lako,wewe ni Lazaro alama ya ufufuo lakini upo na John alama ya ubatizo,ninyi ni watu wa Mungu.

Nikiishia hapa,Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of Business Administration in International Business
-Master's in Leadership and Management

-Research; Assessment on the Effects of Micro-Financing on Poverty Reduction.
 
Umeisha tu Machoni mwetu ila Mioyoni mwao Wamalawi bado upo pale pale.

Unatakiwa umalizwe uishe..
Mgogoro toka wakati wa Nyerere na Kamuzu Banda ..ukaibuka wakati wa JK na Joyce Banda..
Wakijifanya haupo Leo utakuja ibuka miaka 20 mbele tutakuja pata Rais dhaifu awape eneo lote wamalawi...Bora ujadiliwe tujue moja..
 
Naona Brig. Alex Nyirenda aliyepandisha bendera mlima K'njaro akumbukwa.
 
Back
Top Bottom