Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,262
Mbunge wa Songwe (CCM), Philipo Mulugo amekerwa na majibu ya Serikali na kusema yamekuwa ni yale yale kila mwaka.
Mulugo alisimama na kuliambia Bunge kuwa hana mpango tena hata wa kuuliza swali la nyongeza kutokana na ukweli kuwa majibu ya Serikali kuhusu uvunaji wa mamba katika ziwa Rukwa yamekuwa hayaridhishi.
"Majibu ya Serikali ni yale yale tu kila mwaka na hata mwaka jana nilijibiwa hivyo hivyo kwa hivyo bora kunyamaza tu.
Mwanzoni mwa mwaka jana Mbunge huyo aliuliza swali kama hilo na katika swali la nyongeza aliangua kilio kwa kumbukizi kuwa mama yake mzazi aliuliwa na mamba.
Akijibu swali la msingi Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga amesema uwindaji wa mamba hufanyika kwa kuzingatia takwimu kuhusu idadi ya mamba.
Hasunga amesema wizara imekuwa ikifanya utafiti wa wanyamapori na sensa hiyo inalenga kubaini idadi ambayo inawezesha upangaji wa kuvuna wanyama hao.