Kutoka Bungeni: Mbunge asema majibu ya Serikali ni yale yale kila mwaka bora kunyamaza tu

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Mbunge wa Songwe (CCM), Philipo Mulugo amekerwa na majibu ya Serikali na kusema yamekuwa ni yale yale kila mwaka.

Mulugo alisimama na kuliambia Bunge kuwa hana mpango tena hata wa kuuliza swali la nyongeza kutokana na ukweli kuwa majibu ya Serikali kuhusu uvunaji wa mamba katika ziwa Rukwa yamekuwa hayaridhishi.

"Majibu ya Serikali ni yale yale tu kila mwaka na hata mwaka jana nilijibiwa hivyo hivyo kwa hivyo bora kunyamaza tu.

Mwanzoni mwa mwaka jana Mbunge huyo aliuliza swali kama hilo na katika swali la nyongeza aliangua kilio kwa kumbukizi kuwa mama yake mzazi aliuliwa na mamba.

Akijibu swali la msingi Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga amesema uwindaji wa mamba hufanyika kwa kuzingatia takwimu kuhusu idadi ya mamba.

Hasunga amesema wizara imekuwa ikifanya utafiti wa wanyamapori na sensa hiyo inalenga kubaini idadi ambayo inawezesha upangaji wa kuvuna wanyama hao.
 
CCM ni ile ile haitakaa ibadilike
inabadili tu wapiga Sound
mabadiliko Bongo yatakuja pale ambapo wabongo watabadilika
wazim wamekuwa mazwazwa longi tym kama wabongo na hadi wakawasaidiwa na mtaalamu mropokaji wa republican
 
Wewe kila siku unaambiwa ccm ni ile ile bado unashangaa eti majibu ni yale yale kwa hiyo ulitaka mti ule ule wa mchongoma leo utoe maembe.Utakula jeuri yako.
 
Binadamu jamani! Sijui unafiki unatupeleka wapi yaani, huyu kasahau kabisa alikuwa anatoa majibu yale yale nae akiwa naibu waziri wa Elimu, kasahau alikuwa akiinuka na makabrasha yake kujibu swali anajikita kwenye upembuzi yakinifu, wizara ikijiridhisha, wizara inakusanya takwimu, kipaumbele cha sera, kupitia taarifa za kamati, bajeti ikiruhusu na kadharika?
 
Viongozi wengine wapo kwa ajili ya kukamilisha tu muundo hawashirikishwi kwa chochote, ndio maana aliekuwa naibu waziri wa sekta nyeti nae analalama as if hakuona uhalisia kipindi kile akiwa kwenye kiti
 
Back
Top Bottom