Kutoka Bungeni - Jumamosi 21, Aprili 2012 (Videos)

USA(marekani) wasingekuwa na states government (serikali za majimbo) wasingefika hapo walipo.

Mafanikio ya china mpaka amekuwa super power. Ni kutokana na serikali za majimbo.

India, canada.. Hawa wote wana states goverment.

Faida za serikali ya majimbo

1) Itapunguza madaraka ya Raisi automatical

2) Geita almasi inapopatikana, haiwezekani, raia wake ni maskini. (Ndo maana Marekani, California ni tajiri kuliko Washngton. Ingawaje Washtongton ndiko ikulu ya Raisi ilipo)

3) Wananchi wa Tandahimba hawatasubiria waziri wa kilimo mwenye ofisi Dar es Salaam, kutatua matatizo yao. Na inawezekana huyo waziri mwenyewe Tandahimba hapafahamu. Sasa sijui Tandahimba atawasaidia kivipi. Huu ndo mwanzo wa ufisadi.

3) Utawapunguzia mzigo wa majukumu mawaziri. Mfano, Matatizo ya elimu shule ya sekondari Buguza. Yatasimamiwa na state gvt. Na sio kusubiri bajeti ipitishwa na wizara Dar, ndio Buguza wapate mgao wao.

4) Itapunguza ukubwa wa baraza la mawaziri. Kwasababu vitu vingi vitakuwa viko under state gvt.

5) Na mengine mengi....

Unachokiongelea nakifahamu sana, ila ufinyu na ubinafsi wa viongozi wetu ndio unaotatiza hilo. Nyerere alishaanza hilo kwa kusisitiza madaraka mikoani, ila ajenda hiyo imefifishwa na wajanja na kufanya serikali kuu ndiye msimamizi wa nchi nzima na kuleta mlolongo wa kuwaona viongozi wengi kitaifa jambo ambalo lingeishia mkoani tu.

Nchi kama Marekani utakuta secretaries hawana kazi nzito kwani kila state ina bunge na bajeti yake. Ajira za polisi haziligusi taifa La marekani, ila kila State ina utaratibu wake na bajeti kadiri ya hitaji lao, kwa maana hiyo polisi Marekani huajiriwa na manispaa, mji au jini na hivyo halmashauri za manispaa, mji au jiji ndizo zenye kauli kuhusu utendaji wao. Kama ni majukumu ya state, basi state ina polisi wake ambalo huushughulika na mambo ya state tu. Polisi wa kawaida huitwa local police officers.

Hoja ya uanzishwaji wa serikali na madaraka mikoani ni jambo litakalopunguza madaraka ya rais kwani kama kutahitajika mkuu wa mkoa atapatikana kwa kura za wananchi badala ya kuteuliwa kwa kujuana na Rais.
 
naomba niwaambie rais kikwete ni kikwazo kikubwa sana katika kuachia ngazi mawaziri...
 
noaona mzee wa chuchu moro anaongea...simuelewi mimi..hana mguu wa kuku kweli pale??
 
Nimemsikia na kumuona
'live' Sp (of cause kwenye Tv) akitamka kutoka mdomoni mwake kwa Mbowe kuwa, "JAMBAZI Lako" aki-refer Mh J Mnyika! pamoja na kuwa 'aliipotezea' lkn kwa hakika kimtokacho mtu ndicho alichonacho moyoni/nafsini/rohoni/utu wa ndani etc(you name it; soma Gal5:19) najua hawataiingiza kwenye 'hansaard' lkn masikioni mwetu na machoni imeingia! Ushauri Tundu Lisu/Mnyika/Nasari makamanda wetu omba muongozo ili hata kama ataipotezea lkn utu wake wa ndani utatolewa nje hadharani(kumb29:29) Mungu katufunulia kuliko kumezea kwani ndiyo njia pekee kwa sasa itayowapa watu uhalisia wa hawa watu

Nadhani ulimi uliteleza kidogo, alitaka kusema JEMBE LAKO.
 
Kwa wale wanaoangalia Bunge Mda huu, Mawaziri waliojiuzulu wameanza kujionyesha dhahiri kwa kukataa kuhitimisha hoja za za wabunge na taarifa za kamati kwa wizara zao. Wa kwanza ni Waziri wa nishati na Madini, Bwana Ngereja! Tutaendelea kuangalia kinachoendelea
 
MHONGA LUHANYWA:
Afunguka Data nyingi .....
Kahoji kuhusu Msamaha wa Kodi
Masilahi ya Polisi
KUBWA ZAIDI

Matumizi mabaya ya Fedha za Umma, Feni la Taifa limefika TRILIONI 14 huku Serikali inamiiliki magari yenye thamani ya TRILIONI 5 anazungumzia ya Viongozi tu na kwamba trend inaonyesha hakuna matabaka ya gari kwa kada ya kiongozi wote mwendo matanuzi, mbunge lexus, waziri lexus, dc lexus, RC lexus na haya yanauzwa milioni 100

Nchi tajiri kama Marekani magari yanayotumiwa na serikali ni kutoka makampuni ambayo magari yao ni bei ya chini kama Ford na Chev. Magari hayo ni ya kiwango cha chini ukilinganisha na magari yanayotumiwa na watu wa kawaida ambao wana uwezo wa kununua magari mazuri. Na bahati niko likizo huku nitapiga picha na kuiweka hapa kesho kutoka magari yanayotumiwa na serikali za Marekani. Nitamwomba mwenyeji wangu anipeleke kwenye parking lot yao.
 
UPDATES:

Mjadala wa CHAMWINO kwa sasa ni Tata na Sijui nini kitaamuliwa huko, Usiri ni wa hali ya Juu na GR cant cross over. Ha ha ha ha watanzania watashangaa sana leo kwa jinsi hii nchi inavyoendeshwa kwa REMOTE na kulindana.

PM yupo DODOMA si Dar uzi mmoja hapo juu usipotoshe

TETESI: Sizipendi sana ila kuna dalili za mchezo mchafu katika maamuzi ya Mawaziri
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom