Kutoka Bungeni - Jumamosi 21, Aprili 2012 (Videos)

GHOST RYDER

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
1,025
475
Saalaaaaam

Kumekucha baada ya hekaheka za jana huku macho na masikio yakiendelea kutosadiki yanayotarajiwa kujiri hasa baada ya kigugumizi kuwatawala wanaokusudiwa kufunguwa midomo yao kupaza sauti itakayokata mzizi wa fitna na kufungua ukurasa mpya wa historia ya uwajibikaji katika Serikali ya Awamu ya Nne.

Kwa ujumla wabunge wanaoonekana kuranda hapa katika viwanja vya bunge ni wachache saana, sijui wengine wako wapi na ORDER PAPER haionyeshi kama PM kapangiwa kusema jambo licha ya kuwa yeye a kama mtendaji mkuu wa serikali hawajibiki kufanya hivyo kwani wakati wowote anaohitaji kutoa taarifa kwa maelekezo na mwasiliano na Spika anaweza kufanya hivyo.

Tafakuri ni zito, na muda punde Bunge litaanza

Upande anaopitia PM ulinzi upo kuashiria anakuja na muda wowote atafika hapa mjengoni

Yapi yatajiri, Endelea kubaki JF


UPDATES: HOFU YANGU YA KUTOWAONA WABUNGE ILIKUWA SAHIHI

PM ana mjadala Mkali tena, Sitashangaa Maamuzi haya yakachakachuliwa Vibaya na zikazuka Hadithi mpya kabisa ambazo zitasononesha Vibaya mioyo ya Watanzania waliokwishajawa na dukuduku la kujua hatima ya Mawaziri wanaotuhumiwa kwa kutafuna mali ya UMMA na kukosa uwajibikaji.

Tunasaka DETAILS ZAIDI


UPDATES:

Muongozo Ulioombwa ni kutaka Ufafanuzi wa Serikali kwa nini haijatoa Tamko lolote wakati Nchi ipo katika sintofahamu zito na wananchi hawajui hatima ya Mawaziri wanaodaiwa kukaa Kujiuzuru. Naomba Muongozo wako Mh. Spika
KAUMINYA PENGINE ANATAKA USHAURI NINI ASEME ILA ATASEMA TU MAANA NDO KINACHOFUATA YEYE KUULIZWA BAADA YA MAJUMUISHO YA HOJA ZA KAMATI


RECENTLY: PM AMEINGIA MJENGONI NA LOTS OFKABRASHA....Ngoja Tuone




UPDATE: MEDIA zimetega anapotokea PM kwa shauku ya aina yake, ataingia mitini kamajana au atatoa neno?????


VIDEO:

[video=youtube_share;WiATzAGC7b I]http://youtu.be/WiATzAGC7bI[/video]




NOTE: MHE. SPIKA KAMWOMBA RADHI MH. MNYIKA KWA NENO 'JAMBAZI', LISOMEKE "JAMAA"
 
Last edited by a moderator:
Hon Mbowe: Anasisitiza kutojikita katika kujadili matatizo ya Taarifa za kamati na kuwa mchango wake leo utalenga katika kutoa mawazo yake ili kuondoka katika dilema hiyo
 
Spika Makinda to Mbowe "una bahati Jambazi lako limekuwahi kuomba mwongozo sivyo ungekosa nafasi" Mnyika aliomba mwongozo kabla ya Mbowe kuongea
 
Mfumo mbovu wa kurundika madaraka makubwa kwa mawaziri ndio chanzo hata kama tutabadilisha mawaziri leo bila kuwapunguzia madaraka waliyonayo tatizo litarejea tena.

Lawama kati ya watendaji hazitakwisha kama mfumo uliopo wa kurundika mayai yote katika kapu moja hautabadilika

Tuunde mfumo wa kugawa haya madaraka

Waziri hawezi kusimamia madini na rasilimali zote nchi nzima au kilimo

Katiba mpya iangalie jinsi gani tunadecentralize madaraka

kila mmoja anangojea serikali kuu itende, uzembe wa waziri mmoja unaweza kulisababishia serikali mgogoro mkubwa
 
Baraza lote la mawaziri livunjwe tu JK ajipange upya atafute damu changa,atuondolee vizee vilafi na mafisadi
 
Spika Makinda to Mbowe "una bahati Jambazi lako limekuwahi kuomba mwongozo sivyo ungekosa nafasi" Mnyika aliomba mwongozo kabla ya Mbowe kuongea

Aliteleza, inaelekea akiwa nje ya "Kiti" ana lugha za kawaida za mtaani.
 
Wakati tunasubiri Updates, Jiunge na Group Ukombozi Tanzania iliyo Facebook nawe ikiadd marafiki zako wote Watanzania. Kwa pamoja tutafika
 
Naendelea kuamini kuwa wabunge sasa wanafanya kazi waloagizwa na wananchi wao. Mungu na awape nguvu zaidi na kuyaondoa makandokando yote yanayowazunguka
 
Spika SEMAMBA amemwita Mnyika JAMBAZI. Kamwambia mbowe "ulikuwa umepitwa ila shukuru muongozo wa huyu JAMBAZI wako (Mnyika) umekuokoa"
 
Mbowe anawahamsisha watanzania wote viongozi wa Dini, vyama vya siasa na wadau wote katika mchakato wa katiba kuifikiria kwa kina Hoja ya Serikali za Majimbo na DECENTRALIZATION ndio utakuwa ufumbuzi wa matatizo haya ya watanzania, hata kama mabadiliko ya mawaziri yatafanyika bila kubadili mfumo huu ambao CDM imeshatoa mwelekeo katika sera yake ya MAJIMBO hakuna mabadiliko yatakayotokea

MBOWE KAHITIMISHA

KANGE LOGOLA NDEGE anazungumza
 
Tujulishe kaka yanayojiri hapo!Wengine tupo mashambani huku tunategemeat Jf tu kwasasa!
 
Waache waendelee kusuasua/kuhaha! Kiazi walicholishwa kinaunguza kote kote! Wakijiuzulu poa, wakigoma poa! Mungu wetu ni mwaminifu sana!
 

Similar Discussions

26 Reactions
Reply
Back
Top Bottom