Kutoka Bungeni Dodoma: Julai 18, 2011

hiyo ya ccm na wanachama wapya kawe ni uongo mtupu,jana nilikuwepo eneo lile,walikuja na watu wao kumi ,sijui hata walitoka wapi na kuwapa kadi. Na kama kawaida yao walikuja na mabasi lukuki yaliyojaa watu na magwanda yao ya kijani. Kwa ufupu wamechemsha kweli kweli, na hizo pikipiki vijana waliowapa sijuiwamewatoa wapi. Sio wa hapa kabisa. Hawa jamaa ni wasanii sijapata ona. Waliishia kuzomewa tu walivyomaliza ujinga wao.
 
Sasa Beatrice Shellukindo: Anadai eti aliombwa asichangie hoja lakini anamwomba Mungu amsaidie ili achangie!Wananchi wanadai umeme sio maneno!Amemlima Ngeleja kwamba amesoma Bajeti ya Mwaka huu bila confidence yoyote!Anasoma barua toka Wizarani kwa Katibu Mkuu kwamba Sh Milioni 50 ili ziende GST, jumla 1bn! Amemtaka Waziri afuatilie!Atatoa Hoja kwamba hoja ya waziri isipitishwe, irudishwe ikapitiwe upya!
 
betrice shelukindo kawasha moto kabisaaa... Ameweka hadharani barua ya kuwaonga wabunge wa kamati ya nishati na madini.!! Spika amemzimia mic mwshoni baada ya kupitiliza muda
 
Mb Nanyumbu: Dar majenereta kama vile mji umevamiwa na nyuki, nyingine ndogo, saizi ya kati, nk!
 
Asante Mkuu Buchanan kwa bungeni leo updates kwa sie ambao hatuoni wala kusikia live
 
dah pande hizi za shekilango washakata umeme dah mungu niepusha na hizi hasira!!!!!
 
umeme hakuna ...ila zinafanywa jitihada za kuwahonga wabunge wapitishe bajeti, duu! bongo noma. Kwa nn hizo fedha wasinunue madawati badala ya kuhonga wabunge?shame on them.
 
Nadhani mmesikia Mchango wangu leo wakuu. Nia ni kuwasulubu wote wasiolitakia mema taifa hili. Issue sio jina la Kigwangala ninalotumia bali ni Mchango wangu kwa jamii.
Hongera mkuu na mbadilike kama hivi mnapokua mnazungumza mambo ya kitaifa
 
maneno ya ngleja ziku zote ni haya

jitihada
mipango
juhudi
hatuza za mwisho
mkakati
upembuzi



kila sentensi mbili moja ya maneno hayo hapo juu azime ayaseme
 
Jamani niko live, Sasa yupo ole sendeka anasema atamuunga mkono hoja ya mama shelukindo, amemaliza na haungi mkono hoja, anayeongea sasa ni hamadi
 
Ole Sendeka: yaani anamwaga mijisifa tu kwa magamba! Kuwe na Kanuni Maalum za Kuchimba Madini ya Tanzanite! Umeme, Uvumilivu una ukomo, kwa nini serikali yetu isitoe fungu la kutosha kununua mitambo yake badala ya ile ya kukodi kinyume na mapendekezo ya Tume ya Mwakyembe! Suala la TSh 50m/- toka kila Idara (=1bn/-) zifuatiliwe, Waziri Mkuu amwagize Waziri husika afuatilie! HAUNGI MKONO HOJA!
 
maneno ya ngleja ziku zote ni hayajitihadamipangojuhudihatuza za mwishomkakatiupembuzikila sentensi mbili moja ya maneno hayo hapo juu azime ayaseme
uso wake umesawajika vibaya, wabunge wangekuwa na umoja leo asingechomoka.
 
Hamadi rashidi utadhani ana phd ya usimamizi wa madini, watanzania hawanufaishwi na rasimali za nchi yao, anawaomba wabunge walikomalie hili jambo, anasema iptl imeshafilisika sehemu peke yake iliyobaki kuchumia hela ni tz.
 
Rashid Hamad: Rais Kabila amepata wapi ubavu wa kuvunja mikataba Kongo na akabaki salama ili hali sisi tunaogopa kuvunja mikataba?
Madini: Ghana wameanzisha mpango wa Cash Distribution ili kuwafaidisha wananchi wanaozunguka maeneo ya madini! Tuige mpango huo! Pia upotevu mkubwa wa umeme uangaliwe! Kamati ya watu 9 iundwe!
Hali ya IPTL ni mbaya nchini kwao, isipokuwa tu hapa Tanzania! Anakusudia kutoa hoja ya kuunda kamati ya watu 9!
 
Back
Top Bottom