Kutoka Bungeni Dodoma: Julai 18, 2011

ikipita hii bajeti inabidi wananchi waikatae na waingie barabarani
 
Sasa Beatrice Shellukindo: Anadai eti aliombwa asichangie hoja lakini anamwomba Mungu amsaidie ili achangie!Wananchi wanadai umeme sio maneno!Amemlima Ngeleja kwamba amesoma Bajeti ya Mwaka huu bila confidence yoyote!Anasoma barua toka Wizarani kwa Katibu Mkuu kwamba Sh Milioni 50 ili ziende GST, jumla 1bn! Amemtaka Waziri afuatilie!Atatoa Hoja kwamba hoja ya waziri isipitishwe, irudishwe ikapitiwe upya!

Safiii. Lazima tufike mahali tuwajibishane. Aksante mkuu kwa updates!
 
Mpaka muda huu alieunga mkono hii bajeti ni mbunge wa Kibaha mjini kama nipo wrong Buchanan na wengine mnisahihishe wajameni
 
Kwa mujibu wa katiba na kanuni za bunge, bajeti ya wizara isipopita waziri anapewa muda wa kwenda kuipitia na kuianda upya au rais anayo madaraka ya kumfukuza kazi waziri kwa kuogopa kupigiwa kura ya kutokuwa na imani naye.
 
Wakuu hivi kuna online radio yoyote au tv inayorusha bunge? kwa watu tulio nje ya bongo tupate kuona au kusikia! msaada plse
 
Kwa mujibu wa katiba na kanuni za bunge, bajeti ya wizara isipopita waziri anapewa muda wa kwenda kuipitia na kuianda upya au rais anayo madaraka ya kumfukuza kazi waziri kwa kuogopa kupigiwa kura ya kutokuwa na imani naye.

hapo kwenye red kaka haiwezekani ....maana jk anahusika na mikataba mibovu .......
 
Kama bajeti kuu iliyosomwa na Waziri wa Fedha ilishapitishwa hii migawanyo ya wizara ikikwamishwa itasaidia nini? CCM walitakiwa wakwamishe bajeti kuu kama walivyofanya wapinzani na hoja ya wapinzani ilikuwa umeme haukupewa kipaumbele kinanchostahili.
 
Mpaka muda huu alieunga mkono hii bajeti ni mbunge wa Kibaha mjini kama nipo wrong Buchanan na wengine mnisahihishe wajameni
Yupo mbunge mwingine sijui mhindi yule, nadhani anatoka Magu au maeneo kama hayo. Yeye aliunga hoja kwa asilimia mia.
 
Esther Bulaya: Kwanza haungi mkono haja kama alivyotumwa na vijana wa kijiji cha Nyamongo! Serikali za Mitaa zimiliki hisa!
 
Mnyaa: mwongozo kuna mapungufu mengi, Waziri apewe muda kurekebisha asije kuaibika kukataliwa kwa Bajeti!Spika: kuanzia sasa mpaka jioni muda unatosha!
 
Hata huyo aliyeunga mkono alitoa masharti, mnyaa anaomba mwongozo kwa spika bajeti irudishwe chumbani spika amempuuza, bunge linaelekea mwishoni, ngeleja kavimba uso huwezi amini, saa11, tukutane hapa hapa.
 
Bunge limeahirishwa hadi jioni! Wabunge wa CCM watakutana muda wa saa 7 mchana, hapa mambo yanaenda kuwekwa sawa ili Bajeti ipite!
 
Back
Top Bottom