Kutoka Bungeni Dodoma: Julai 18, 2011

Kutoka Bungeni Dodoma: Julai 18, 2011

Sasa Mbunge wa CDM, Mngodo: Amemshukuru Mh Mbowe kwa kukiongoza Chama licha ya kuwekwa ndani ameweza kukiongoza Chama! Kuhusu Madini kuna ubaguzi katika machimbo ya kijiji cha Maganzo, Shinyanga ambapo wachimbaji wenye asili ya kiasia wanapendewa vs weusi!
Umeme: Tanzania imekuwa gizani kwa miaka 19! Nani alipitisha mikataba zaidi ya Bunge kwa mujibu wa Ibara ya 63 (3) ya Katiba ya JMT! Umefika wakati wa kushirikisha Sekta binafsi!
Taarifa: Serikali imeridhia Sekta Binafsi!
NETGROUP ilikuwa inatunyonya, DG wake alikuwa analipwa mshahara wa TSh 23!
Haungi mkono hoja!
 
Dr Hamis kingwangala anaongea bungeni....du moto mkali kwa serikali ya chama chake Khaaa
 
asante kwa taarifa mkuu huku umeme ushatika tangu jana so utujuze.
 
Tujuzeni basi anachosema wengine hatuko kwenye runinga kwa sasa
 
Mbunge Kigwangala: Kwanza haungi mkono hoja kwa sababu waliosaini mikataba mibovu wanajulikana na hawachukuliwi hatua yoyote! Lazima tuwe na intelijensia ya kutosha kujua maslahi ya kiuchumi ya makampuni yanayowekeza humu nchini na sio kutafuta intelijensia za watu wanaotaka kuandamana kule Nzega, Mwanza, Arusha na kwingineko! Pan African Energy wamekwepa kodi ya TSh 100bn/- kwa njia ya "tax haven!" Leseni zote zifutwe, mikataba yote ivunjwe!
 
jamaa amegoma kuunga mkono hoja. Amesema kwa hisia sana kwamba, ardhi yote yenye madini imeuzwa!
 
Leo naona kaamua kumwaga ugali, . Kaongelea madini na kagoma kuunga mkono hoja.
 
Dr Hamis kingwangala anaongea bungeni....du moto mkali kwa serikali ya chama chake Khaaa

Nafuatilia kwenye TV; jamaa kakata issue vizuri saana!!!! SPIKA ananza kuleta u-Headmisstress kwa kuwa mbabe🙂
 
waziri amekubali kwamba tumeibiwa na makampuni ya madini
 
amesema mawaziri wamejjengewa nyumba mbezi beach.
 
huyu mbunge alivyoanza nilidhani wa chadema kumbe ccm, kweli watu wameshachoka kubuluzwa... eti wanafikilia kwa kutumia matumbo.!! leo hapatoshi
 
Nagu: Dr Kigwangala atoe ushahidi kwamba kuna watu wamejengewa nyumba Mbezi Beach ili wasaini mikataba mibovu ya madini! Spika ameipotezea kiaina!
 
Back
Top Bottom