source mwananchi.
Malisa anayeishi Kata ya Ngarenaro jijini
humo alifika uwanjani hapo kumwokoa
baba yake Godwin Malisa ambaye ni
mlemavu, alijikuta akipata kipigo cha
mbwa mwizi.
Nilikuwa namfuata baba yangu ambaye ni
kada wa Chadema. Kutokana na ulemavu
wake nilihofu angepata matatizo kama
vurugu zingezuka, anasema Wema na
kuongeza:
Nilikuta uwanja ukiwa umefurika
wananchi wakiwasikiliza viongozi wa
Chadema. Viongozi hao ni Mbunge wa
Arusha Mjini, Godbless Lema ambaye
alihutubia na kumwachia Tundu Lissu
(Mbunge wa Singida Mashariki) naye
akamwachia Said Arfi (Mbunge Mpanda
Kati). Alipomaliza kuwataka wanachama
hao waelekee Hospitali ya Mount Meru,
ndipo mabomu yakaanza kulipuliwa.
Anaendelea kusema: Nilimwambia baba
tuondoke lakini tulikuwa tumeshachelewa,
kwani polisi walikuwa wametuzingira.
bomu la pili liliangukia mbele yetu. Askari
mmoja akasema laleni chini, tukalala
tukidhani tutakuwa salama. Lakini
walikuja askari na kutupiga marungu
mwili mzima mimi na baba,
Ghafla akatokea askari mwingine
akawakataza wasitupige, tukadhani
tumeokoka. Mara wakatokea askari
wengine, hapo ndipo kilikuwa kipigo
kitakatifu. Nilijaribu kuwazuia wasimpige
baba kwa kuwa ni mlemavu, wakanikebehi
kuwa huyo ni hawara yangu. Walinipiga
mpaka mkono na mguu ya kushoto
ikavunjika.
Tulikuwa kwenye kibaraza cha nyumba
wakati askari wanatupiga. Askari mmoja
alirarua gauni langu chini na juu, hadi
nikabaki uchi mbele ya baba. Mwingine
akakoki bunduki na kuielekeza katikati ya
mapaja yangu ili alipue sehemu za siri,
wenzake wakamkataza. Mwingine alisema
kuwa atanibaka. Baba alinikumbatia
akasema watuue wote, mimi niliomba
wasituue maana nimeacha mtoto mchanga
nyumbani.
Anasema askari walikuwa wakimbeza kwa
kumuuliza kwa nini yeye ni mwanachama
wa Chadema.
Walisema unajifanya wewe Chadema, sasa
ndiyo utajua kuwa CCM inatawala. Chezea
CCM wewe. Mimi niliwaambia sina chama
chochote nimekuja kumwokoa baba yangu.
Wakati huo wote walishanivua hereni, simu
wakachukua na fedha zilizokuwa ndani ya
pochi na kuitupa chini ikiwa tupu.
Malisa anayeishi Kata ya Ngarenaro jijini
humo alifika uwanjani hapo kumwokoa
baba yake Godwin Malisa ambaye ni
mlemavu, alijikuta akipata kipigo cha
mbwa mwizi.
Nilikuwa namfuata baba yangu ambaye ni
kada wa Chadema. Kutokana na ulemavu
wake nilihofu angepata matatizo kama
vurugu zingezuka, anasema Wema na
kuongeza:
Nilikuta uwanja ukiwa umefurika
wananchi wakiwasikiliza viongozi wa
Chadema. Viongozi hao ni Mbunge wa
Arusha Mjini, Godbless Lema ambaye
alihutubia na kumwachia Tundu Lissu
(Mbunge wa Singida Mashariki) naye
akamwachia Said Arfi (Mbunge Mpanda
Kati). Alipomaliza kuwataka wanachama
hao waelekee Hospitali ya Mount Meru,
ndipo mabomu yakaanza kulipuliwa.
Anaendelea kusema: Nilimwambia baba
tuondoke lakini tulikuwa tumeshachelewa,
kwani polisi walikuwa wametuzingira.
bomu la pili liliangukia mbele yetu. Askari
mmoja akasema laleni chini, tukalala
tukidhani tutakuwa salama. Lakini
walikuja askari na kutupiga marungu
mwili mzima mimi na baba,
Ghafla akatokea askari mwingine
akawakataza wasitupige, tukadhani
tumeokoka. Mara wakatokea askari
wengine, hapo ndipo kilikuwa kipigo
kitakatifu. Nilijaribu kuwazuia wasimpige
baba kwa kuwa ni mlemavu, wakanikebehi
kuwa huyo ni hawara yangu. Walinipiga
mpaka mkono na mguu ya kushoto
ikavunjika.
Tulikuwa kwenye kibaraza cha nyumba
wakati askari wanatupiga. Askari mmoja
alirarua gauni langu chini na juu, hadi
nikabaki uchi mbele ya baba. Mwingine
akakoki bunduki na kuielekeza katikati ya
mapaja yangu ili alipue sehemu za siri,
wenzake wakamkataza. Mwingine alisema
kuwa atanibaka. Baba alinikumbatia
akasema watuue wote, mimi niliomba
wasituue maana nimeacha mtoto mchanga
nyumbani.
Anasema askari walikuwa wakimbeza kwa
kumuuliza kwa nini yeye ni mwanachama
wa Chadema.
Walisema unajifanya wewe Chadema, sasa
ndiyo utajua kuwa CCM inatawala. Chezea
CCM wewe. Mimi niliwaambia sina chama
chochote nimekuja kumwokoa baba yangu.
Wakati huo wote walishanivua hereni, simu
wakachukua na fedha zilizokuwa ndani ya
pochi na kuitupa chini ikiwa tupu.