Kutoka Arusha: Mtutu katikati ya mapaja ni unyama

Kutoka Arusha: Mtutu katikati ya mapaja ni unyama

Sasa hivi kilicho baki ukipata jamaa wa huko mpaka ni chonga nae upate ya kujihami, maana huko tunakoelekea kama huna ya kuji hami maisha yako yako hatarini sana...Na shukru mimi Masanilo kani ahidi tubadilishane ni mpe viwanja viwili...


Nalilia taifa langu ulevi wa madaraka unatupeleka kubaya. Kuna watu wanafikiria wao wanahaki Miliki ya kututawala. Ukiwa mpinzani lazima uwe ngangali utafunguliwa Kesi za kugushi, Utatishiwa kufukuzwa kazi serikalini. Kuna vijana wengi wako rumande na dhamana zimefungwa nchi imekuwa Kama tunapigania uhuru. Pinda naye ameongeza kupigwa na kuuwawa

Yana Mwisho haya hakuna mahali duniani nguvu ya umma iliwahi shindwa
 
Kwa ushuhuda huu na nyingine nyingi zinazofanana na huu za polisi kupiga, kupora mali, kubaka na hata kuua, kauli ya waziri mkuu inastahili kulaaniwa na kupingwa kila mpenda amani ya nchi yetu. Je, kwa kauli ya waziri mkuu, ni nani mtovu wa nidhamu hapa, ni polisi au huyu dada asiye na hatia? Je, dada huyu na baba yake wamepigwa na kunyanyaswa kwa sababu wamekataa kutiii 'amri ya polisi' kama ambavyo waziri mkuu anataka umma wa watanzania uamini au kwa sababu ni wanachama wa cdm? Nini haki za walemavu na wanawake mbele ya polisi? Je, haki hizo zinapotea ghafla mtu anapokuwa mwanachama wa chadema au chama kingine cha upinzani? Watu wanaichukia vyombo vya dola na hasa polisi si kwa sababu ya mtu mmoja aliwahi kusema 'nchi haitawalika' bali ni kwa sababu ya matendo yao yanavuruga amani ya nchi kwa jina la 'kulinda amani ya nchi'. Na hii ndio hatari ya kuongozwa na watu 'waliochoka' kuongoza na badala yake wanatumia polisi kunyamazisha watu. Poor Tanzania!!!!!

Pinda, Wassira, Mwigulu na wengineo wenye mawazo kama haya watapita kama sio leo ni kesho au hata kesho kutwa, bali Tanzania na watanzania wataendelea kuwepo. Kwa kuwa 'serikali imechoka' na imekiri hivyo tena kupitia chombo cha kisheria cha kutunga sheria, ni vyema sasa wakaamua kupumzika na kuruhusu mchakato wa katiba kuunda serikali nyingine yenye ridhaa ya wananchi. Kwa nini uendelee kung'aninia kuongoza watu ambao wewe mwenyewe unasema umechoka? Tafakari!!!!!

source mwananchi.

Malisa anayeishi Kata ya Ngarenaro jijini
humo alifika uwanjani hapo kumwokoa
baba yake Godwin Malisa ambaye ni
mlemavu, alijikuta akipata kipigo cha
mbwa mwizi.
"Nilikuwa namfuata baba yangu ambaye ni
kada wa Chadema. Kutokana na ulemavu
wake nilihofu angepata matatizo kama
vurugu zingezuka," anasema Wema na
kuongeza:
"Nilikuta uwanja ukiwa umefurika
wananchi wakiwasikiliza viongozi wa
Chadema. Viongozi hao ni Mbunge wa
Arusha Mjini, Godbless Lema ambaye
alihutubia na kumwachia Tundu Lissu
(Mbunge wa Singida Mashariki) naye
akamwachia Said Arfi (Mbunge Mpanda
Kati). Alipomaliza kuwataka wanachama
hao waelekee Hospitali ya Mount Meru,
ndipo mabomu yakaanza kulipuliwa."
Anaendelea kusema: "Nilimwambia baba
tuondoke lakini tulikuwa tumeshachelewa,
kwani polisi walikuwa wametuzingira.
bomu la pili liliangukia mbele yetu. Askari
mmoja akasema ‘laleni chini', tukalala
tukidhani tutakuwa salama. Lakini
walikuja askari na kutupiga marungu
mwili mzima mimi na baba,"
"Ghafla akatokea askari mwingine
akawakataza wasitupige, tukadhani
tumeokoka. Mara wakatokea askari
wengine, hapo ndipo kilikuwa kipigo
kitakatifu. Nilijaribu kuwazuia wasimpige
baba kwa kuwa ni mlemavu, wakanikebehi
kuwa huyo ni hawara yangu. Walinipiga
mpaka mkono na mguu ya kushoto
ikavunjika.
"Tulikuwa kwenye kibaraza cha nyumba
wakati askari wanatupiga. Askari mmoja
alirarua gauni langu chini na juu, hadi
nikabaki uchi mbele ya baba. Mwingine
akakoki bunduki na kuielekeza katikati ya
mapaja yangu ili alipue sehemu za siri,
wenzake wakamkataza. Mwingine alisema
kuwa atanibaka. Baba alinikumbatia
akasema watuue wote, mimi niliomba
wasituue maana nimeacha mtoto mchanga
nyumbani."
Anasema askari walikuwa wakimbeza kwa
kumuuliza kwa nini yeye ni mwanachama
wa Chadema.
"Walisema ‘unajifanya wewe Chadema, sasa
ndiyo utajua kuwa CCM inatawala. Chezea
CCM wewe.' Mimi niliwaambia sina chama
chochote nimekuja kumwokoa baba yangu.
Wakati huo wote walishanivua hereni, simu
wakachukua na fedha zilizokuwa ndani ya
pochi na kuitupa chini ikiwa tupu."
 
Ni vigumu kuamini kwamba mambo ya kipuuzi kama haya yanatokea Tanzania....
Hapa ndipo tunapokosea! haya si mambo ya KIPUUZI,haya ni mambo serious kabisa! huu ni udhalimu ,unyama ukatili wa kiwango cha juu kabisa !
 
Polisi wengi wanaofanya kazi Arusha pamoja na Traffic wamesikitika sana na wanatengwa na jamii.

Wengi wa Polisi wemepanga mitaani, wanaenda bar za mitaani, wamejenga pia..


Sasa kitendo cha kutumika na Nyinyiem kulipua mkutano wa chadema na kesho yake kupiga mabomu kumewatenga na jamii, wanaonekana kama magaidi.

Polisi wanajieleza sana na kuomba msamaha na kusema wao hawahusika, Polisi walioletwa kutoka Morogoro na Kibaha ndo walitumika.

Huu mtindo wa serikali kuhamisha polisi kwenda kuua mikoa mingine ni cha kukemewa na watanzania wote wapenda amani. Mashirika ya Haki za binadamu na vyama vya wafanyakazi mbona wako kimyaaa??

Kwa mfano chama cha waaalimu, chama cha madaktari, TUCTA, chama cha wanasheria tanganyika, viongozi wa dini, kwa pamoja wakemee vitendo vya polisi kutumika na mafisadi na pia kauli ya PM.

Natoa wito kwa Polisi na JWTZ, wawe wazalendo kama baadhi ya usalama wa taifa, ambao wanasaidia kuvujisha siri za vikao vya kuihujumu CDM.

Mie nashangaa, Polisi akistaafu hapewi hata ukuu wa wilaya, ukuu wa Mkoa ama ujumbe wa board!!!!!.....
 
source mwananchi.

Malisa anayeishi Kata ya Ngarenaro jijini
humo alifika uwanjani hapo kumwokoa
baba yake Godwin Malisa ambaye ni
mlemavu, alijikuta akipata kipigo cha
mbwa mwizi.
“Nilikuwa namfuata baba yangu ambaye ni
kada wa Chadema. Kutokana na ulemavu
wake nilihofu angepata matatizo kama
vurugu zingezuka,” anasema Wema na
kuongeza:
“Nilikuta uwanja ukiwa umefurika
wananchi wakiwasikiliza viongozi wa
Chadema. Viongozi hao ni Mbunge wa
Arusha Mjini, Godbless Lema ambaye
alihutubia na kumwachia Tundu Lissu
(Mbunge wa Singida Mashariki) naye
akamwachia Said Arfi (Mbunge Mpanda
Kati). Alipomaliza kuwataka wanachama
hao waelekee Hospitali ya Mount Meru,
ndipo mabomu yakaanza kulipuliwa.”
Anaendelea kusema: “Nilimwambia baba
tuondoke lakini tulikuwa tumeshachelewa,
kwani polisi walikuwa wametuzingira.
bomu la pili liliangukia mbele yetu. Askari
mmoja akasema ‘laleni chini’, tukalala
tukidhani tutakuwa salama. Lakini
walikuja askari na kutupiga marungu
mwili mzima mimi na baba,”
“Ghafla akatokea askari mwingine
akawakataza wasitupige, tukadhani
tumeokoka. Mara wakatokea askari
wengine, hapo ndipo kilikuwa kipigo
kitakatifu. Nilijaribu kuwazuia wasimpige
baba kwa kuwa ni mlemavu, wakanikebehi
kuwa huyo ni hawara yangu. Walinipiga
mpaka mkono na mguu ya kushoto
ikavunjika.
“Tulikuwa kwenye kibaraza cha nyumba
wakati askari wanatupiga. Askari mmoja
alirarua gauni langu chini na juu, hadi
nikabaki uchi mbele ya baba. Mwingine
akakoki bunduki na kuielekeza katikati ya
mapaja yangu ili alipue sehemu za siri,
wenzake wakamkataza. Mwingine alisema
kuwa atanibaka. Baba alinikumbatia
akasema watuue wote, mimi niliomba
wasituue maana nimeacha mtoto mchanga
nyumbani.”
Anasema askari walikuwa wakimbeza kwa
kumuuliza kwa nini yeye ni mwanachama
wa Chadema.
“Walisema ‘unajifanya wewe Chadema, sasa
ndiyo utajua kuwa CCM inatawala. Chezea
CCM wewe.’ Mimi niliwaambia sina chama
chochote nimekuja kumwokoa baba yangu.
Wakati huo wote walishanivua hereni, simu
wakachukua na fedha zilizokuwa ndani ya
pochi na ku
 
source mwananchi.

Malisa anayeishi Kata ya Ngarenaro jijini
humo alifika uwanjani hapo kumwokoa
baba yake Godwin Malisa ambaye ni
mlemavu, alijikuta akipata kipigo cha
mbwa mwizi.
¡°Nilikuwa namfuata baba yangu ambaye ni
kada wa Chadema. Kutokana na ulemavu
wake nilihofu angepata matatizo kama
vurugu zingezuka,¡± anasema Wema na
kuongeza:
¡°Nilikuta uwanja ukiwa umefurika
wananchi wakiwasikiliza viongozi wa
Chadema. Viongozi hao ni Mbunge wa
Arusha Mjini, Godbless Lema ambaye
alihutubia na kumwachia Tundu Lissu
(Mbunge wa Singida Mashariki) naye
akamwachia Said Arfi (Mbunge Mpanda
Kati). Alipomaliza kuwataka wanachama
hao waelekee Hospitali ya Mount Meru,
ndipo mabomu yakaanza kulipuliwa.¡±
Anaendelea kusema: ¡°Nilimwambia baba
tuondoke lakini tulikuwa tumeshachelewa,
kwani polisi walikuwa wametuzingira.
bomu la pili liliangukia mbele yetu. Askari
mmoja akasema ¡®laleni chini¡¯, tukalala
tukidhani tutakuwa salama. Lakini
walikuja askari na kutupiga marungu
mwili mzima mimi na baba,¡±
¡°Ghafla akatokea askari mwingine
akawakataza wasitupige, tukadhani
tumeokoka. Mara wakatokea askari
wengine, hapo ndipo kilikuwa kipigo
kitakatifu. Nilijaribu kuwazuia wasimpige
baba kwa kuwa ni mlemavu, wakanikebehi
kuwa huyo ni hawara yangu. Walinipiga
mpaka mkono na mguu ya kushoto
ikavunjika.
¡°Tulikuwa kwenye kibaraza cha nyumba
wakati askari wanatupiga. Askari mmoja
alirarua gauni langu chini na juu, hadi
nikabaki uchi mbele ya baba. Mwingine
akakoki bunduki na kuielekeza katikati ya
mapaja yangu ili alipue sehemu za siri,
wenzake wakamkataza. Mwingine alisema
kuwa atanibaka. Baba alinikumbatia
akasema watuue wote, mimi niliomba
wasituue maana nimeacha mtoto mchanga
nyumbani.¡±
Anasema askari walikuwa wakimbeza kwa
kumuuliza kwa nini yeye ni mwanachama
wa Chadema.
¡°Walisema ¡®unajifanya wewe Chadema, sasa
ndiyo utajua kuwa CCM inatawala. Chezea
CCM wewe.¡¯ Mimi niliwaambia sina chama
chochote nimekuja kumwokoa baba yangu.
Wakati huo wote walishanivua hereni, simu
wakachukua na fedha zilizokuwa ndani ya
pochi na kuitupa chini ikiwa tupu.¡±

Niliwahi kuleta mada humu ndani kuwa Mtwara polisi wanafanya vitendo hivyo vya kusachi watu mifukoni, kunyang'anya simu, kubaka nk. Nikaleta uzi kuwa sasa Mtr wameleta vifaru vinaranda mitaani. Nyie ndyo mlikuwa wa kwanza kupinga na wengine walidiriki kuniita mzushi wakitaka niweke picha, nikaweka picha lakini bado sikueleweka, na mkawabeza sana watu wa huko. Leo yametokea Arusha, na kesho kwingineko kumbuka kuwa ''what goes arround comes arround'' shime tuungane, yale ya Mtr na ya Arusha yote lengo ni moja tu kukataa kuendelea kuonewa.
 
Hata Askari anapotekeleza amri ya mkuu wake bado anatakiwa atumie akili na utashi wake na kujali utu wa mwanadamu!Waweke tu akilini mwao kwamba kunakulipa tena haraka sana na wakati huo hakutakuwa na huyo mkuu/wakuu waliokuagiza kufanya hayo!Hapo hakutakuwa na CCM,CHADEMA wala nani.Jamani tuweni na HOFU YA MUNGU YUPO!
 
Dah...!!! mambo mengine yanafanyika ili kuharakisa ukombozi.

ukishindwa kwa Hoja lazima urushe mangumi.......sasa anayepigwa akiamua kurudisha mangumi sijui nini kitatokea.
 
Mi naomba jeshi la polisi libadili sare na na zile bendera vituoni ziwe na rangi ya ccm!!
Ccm oyee
 
Hii habari imetungwa na vijana wa BAVICHA, nampongeza sana mtunz wa riwaya hii kwa kujitahid walau ifanane na ukweli lakini naona amechemka, si vibaya akijipanga upya huenda itakuwa tamu zaidi!
 
niliwahi kuleta mada humu ndani kuwa mtwara polisi wanafanya vitendo hivyo vya kusachi watu mifukoni, kunyang'anya simu, kubaka nk. Nikaleta uzi kuwa sasa mtr wameleta vifaru vinaranda mitaani. Nyie ndyo mlikuwa wa kwanza kupinga na wengine walidiriki kuniita mzushi wakitaka niweke picha, nikaweka picha lakini bado sikueleweka, na mkawabeza sana watu wa huko. Leo yametokea arusha, na kesho kwingineko kumbuka kuwa ''what goes arround comes arround'' shime tuungane, yale ya mtr na ya arusha yote lengo ni moja tu kukataa kuendelea kuonewa.
watanzania wenzangu wapenda haki,jambo la mhimu hapa ni kuwapiga chini ccm,tukiwapiga chini huenda hawa askari wachache wanaotii amri za kijinga watakoma,tujaribu vyama vingine tuone watafanya nini,kuna baadhi ya askari hawapendi kabisa mambo haya yanayofanywa na ccm tena wanatamani sana ccm ipigwe chini
 
Back
Top Bottom