Baada ya kusikia habari za mtanzania aliyeuawa vitani nchini Ukraine akipambana upande wa Urusi dhidi ya Ukraine nilishangazwa sana na kujiuliza, ilikuwaje?
Maneno mengi nikaanza kusikia kabla ya siku ya leo serikali kutoa taarifa ya kilichotokea. Kuna wengine walidai ni mwanafunzi alilazimishwa kubeba silaha. Mtazamo huu hasi umejengwa kuficha ukweli halisi.
Siku ya leo tumeona wizara ya mambo ya nje ikitoa maelezo ya kilichojiri na kusema kwamba mtanzania huyo anaitwa Nemes Tarimo alikuwa ni mfungwa na alihukumiwa miaka 7 gerezani. Alipewa uamuzi wa kuchagua kwenda vitani na kulipwa na Vita ikiisha awe huru au kuendelea kutumikia kifungo na yeye akajua kwenda vitani.
Uchaguzi aliofanya ndio umenifanya niwiwe kuandika ninachokiandika.
Tanzania ni mwanacha wa umoja wa nchi zisizofungamana na Upande wowote(NAM) na hii ni sera ya Tanzania kimataifa.
Bila kutambua ,baadhi ya wanaoenda nje ya nchi pengine kwa ajili ya masomo ,kazi n.k wanasahau au hawajui sera hii ya Tanzania kimataifa.
Kwa kufanya hivi ,kwa sababu utaifa ni moja ya kitambulisho Cha Taifa wanajikuta wakiingiza nchi kwenye migogoro ya kimataifa.
Bw. Nemes Tarimo kwa kutokuwa na uelewa au kutamani kuwa huru akasahau kwamba huko alipo anaiwakilisha Tanzania. Kujiingiza kwake vitani ni kusema kwamba Tanzania Ina upande na ipo upande wa Urusi jambo ambalo kwa sera yetu ya kimataifa ya kutofungamana na upande wowote ni kutengeneza mgogoro.
Nemes Tarimo amefanya makosa makubwa na hili linafanya taswira ya nchi kimataifa kupata muonekano mbaya, tuanze kwa Nemes kurekebisha.
Katika kurekebisha ni vema ikaweka mkazo wa kutosha kwa wote wanaoenda nje ya nchi juu ya sera hii. Hili litasaidia kuondoa uwezekano wa kutokea kwa migogoro kwa watu kutoelewa sera hii.
Nimalize kwa kusema kwamba" mavumbini tulitoka na mavumbini tutarudi, Mwenyezi Mungu aipumzishe Roho ya Marehemu mahali pema Peponi.Amen"