Serikali ya Tanzania yasema Nemes Tarimo alihukumiwa miaka 7 jela, akafariki akiwa vitani

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,460
Waziri wa Mambo ya Nje, Stergomena Tax amesema Mtanzania aliyefariki Dunia Nchini Urusi, Nemes Tarimo alikuwepo nchini humo kwa ajili ya masomo na alijiunga na Chuo cha Moscow Technology Pro mwaka 2020 kwa masomo ya Shahada ya Uzamili katika fani ya 'Business Informatics'.

Waziri amesema taarifa ambazo Serikali imezipokea ni kuwa mwezi Machi 2022, Mtanzania huyo alikuhumiwa kifungo cha miaka saba gerezani kwa mujibu wa Sheria za Urusi kutokana vitendo vya uhalifu.

Ameongeza kuwa akiwa gerezani alipewa nafasi ya kujiunga na kikundi cha kijeshi kilichopo nchini humo kinachofahamika kama Wagner akihadiwa kulipwa fedha lakini pia kwa ahadi ya kuachiwa huru mara baada ya vita ambapo inadai kuwa alikubali kujiunga na kikundi hicho.

Ikumbukwe kauli ya Waziri siku chache baada ya kuibuka taarifa zilizodai uwepo wa Mtanzania aliyefia Nchini Urusi akihusishwa katika mapigano ya vita vya baina ya Urusi na Ukraine ambavyo vimedumu kwa muda.

Familia ya Nemes Tarimo ilithibitisha kutokea kwa kifo hicho na kuwa wanasubiri mwili wa mpendwa wao kwa ajili ya maziko.

Aidha, kwa mujibu wa familia hiyo alifariki mwishoni mwa mwezi Oktoba 2022 na kwamba taarifa ya kwanza walipatiwa na marafiki wa karibu mwishoni mwa mwezi Desemba 2022 kuwa kijana wao amefariki lakini baadae walidai kupata taarifa rasmi kutoka Ubalozi wa Tanzania Moscow, Urusi.

Pia soma:
Safari ya kuusafirisha mwili wa Mtanzania Nemes Tarimo kutoka Urusi hadi Tanzania inaanza 24 Januari, 2023

Tarimo Nemes, anayedaiwa alifariki akiwa vitani Ukraine, aligombea Ubunge Jimbo la Kibamba kupitia CHADEMA
 
Pia, Nemes Tarimo alikuwa mwana CHADEMA na aligombea ubunge 2020 kupitia kwenye Jimbo la Ubungo.

Mungu amweke mahali pema peponi lakini Jambo hili CHADEMA walitakiwa watoe maelezo ya kutosha kilichopelekea mwanachama wao akafungwa miaka 7
 
Aliyegombea Ubungo ni Boni Yai!
Alishindwa ktk kura ya maoni ndani ya chama na kushika nafasi ya pili

Kwa kifupi kura hazikutosha kumvusha, hivyo akarejea zake urusi kutafuta maisha

Huko ndipo balaaa likamfika

280858A2-4204-457F-A103-90115424AA61.jpeg


85A5D996-E051-4067-87D9-44E328829C28.jpeg


3ADEAC56-13CA-4AAD-8AA6-151E3557F260.jpeg


1FBB82B3-3F86-4D64-829B-0E8D971E3147.jpeg


CE4C154F-DC9E-44D5-B0FC-718ADEFBBC3A.jpeg


181FC144-D3D2-4BAD-ACE6-DC302989C3BB.jpeg
 
Kulingana na ushahidi wa nyaraka za mahakama ya Urusi ambazo jarida la “The Chanzo” imeweka wazi mtandaoni, marehemu hakuwahi kuhukumiwa bali kesi yake ilikuwa ikisogezwa na yeye kubaki jela hadi alipojiunga na kundu la Wagner. Hicho kifungo cha miaka 7 alichohukumiwa mwezi March 2022 si kweli kulingana na documents za mahakama zilizopo mtandaoni.
 
Kulingana na ushahidi wa nyaraka za mahakama ya Urusi ambazo jarida la “The Chanzo” imeweka wazi mtandaoni, marehemu hakuwahi kuhukumiwa bali kesi yake ilikuwa ikisogezwa na yeye kubaki jela hadi alipojiunga na kundu la Wagner. Hicho kifungo cha miaka 7 alichohukumiwa mwezi March 2022 si kweli kulingana na documents za mahakama zilizopo mtandaoni.
Unataka sema tumedanganywa na MFA au wao ndo wamedanganywa na RF?
 
Back
Top Bottom