Kutoboa kimaisha

Kutoboa kimaisha

MIHAYO1710

Member
Joined
Apr 7, 2018
Posts
20
Reaction score
47
Wakuu habari zenu?

Ni vigezo gani vitumike vunatumika kuhitimisha kwamba fulani katoboa? Uzi huu unalenga kuwatia moyo wale ambao pengine wanaelekea kukata tamaa ilhali kwa vigezo vya walimwengu ni wametoboa tayari
 
Kutoboa kimaisha maana yake kuwa na uwezo wa kupata mahitaji muhimu ya mwanadamu.mfano ukiumwa sasa hivi figo au moyo uweze kumudu gharama za kujiuguza hata kama kwenda nje ya nchi ukatibiwe na kupona huko ndiyo kutoboa.Ikitokea umepata changamoto kidogo tu huwezi kuitatua ujue kabisa bado hujatoboa.
 
Ni vigezo gani vitumike vunatumika kuhitimisha kwamba fulani katoboa? Uzi huu unalenga kuwatia moyo wale ambao pengine wanaelekea kukata tamaa ilhali kwa vigezo vya walimwengu ni wametoboa tayari
Msosi wa kushiba huwa unaonekana hata ukiwa kwenye sahani, sio lazima Ule.

Ukitoboa kimaisha utajiona mwenyewe, uliyekuwa jana utakuwa tofauti na Leo. Mahitaji muhimu ya binadamu kwako yatakuwa rahisi kumudu (Umetoboa kiuchumi) na Afya ikiwa njema (Umetoboa kiafya).

Be a Man, muhimu ni yajue ya kuzingatia ili uache comparison na maisha ya wengine.
 
Ni vigezo gani vitumike vunatumika kuhitimisha kwamba fulani katoboa?
Ukiweza kuacha kazi(hands off) na ukaendelea kuishi life style yako decently!. Jua ushatoboa,lkn Kama una life ya utoke ndio ule,Basi unamwendo mrefu sana ....

Buffet alisema ''ukishindwa kuingiza hela ukiwa umelala,utakuwa mtumwa maisha yako yote''
 
Pambana kila siku usilale njaa.... mengine yatajulikana mbele ya Safari !

NB... Unaweza kuutafuta huo utajiri/kutoba, na ukafa kapuku
 
Ukiona unaagiza bia kisha baadaye unaanza kupiga hesabu ile hela imetumikaje ujue bado hujatoboa.

Au ukianza kujutia pesa uliyohonga baada ya kupewa tunda ujue hujatoboa.

Mwanamke kama huwezi kujihudumia mwenyewe kwa kazi halali na unategemea kuwapiga mizinga wanaume wawili na zaidi ujue hujatoboa.
 
Back
Top Bottom