Kutoa pesa ili kuonana na mtumishi wa Mungu

Mtoa mada ulitakiwa kutaja jina la mchungaji au kanisa lilipo.kuweka uhalali wa madai yako.pia kama ni kweli basi tatizo ni waumini na si mtumishi
 
Mkuu Login17, kama nimekuelewa vizuri ulikuwa unataka kujikeep busy na fellowship...sasa kwa mtumishi nabii ulienda kufanyaje?

Mi naona sometimes wanaweka hela(kama ni kweli lakini) ili kupunguza jam kwa kweli
Lengo ni kujua utaratibu wao wa ibada n.k. Sasa kabla sijapewa utaratibu nikaambiwa nionane na Nabii. Ndio nikakutana na mambo ya appointment na kulipia
 
Jifunze kujiombea na kumweleza Mungu unachohitaji maana bibilia inasema mtumainiaye mwanadamu am........so ni bora ukasimama mwenyewe na Mungu anajibu.Imewahi nikuta kitu ka hicho nilitupa pesa sana mwisho nikajiambia mwenyewe lazima Mungu atambue hitaji langu kwa kweli nilifanikiwa.
 
Makanisa mengi wanayofundisha neno la Mungu na Kuhimiza kulijua neno la Mungu na Kuomba yanawashirika wachache sanaa ila makanisa ya Mitume na Manabii yana watu nyomii mbayaa.kanisa haliwezi kukusa support ya shetani huku inaviambatanishi vingiiii vya shetaniii.Mungu wa kweli hana viambatanishi zaidi ya roho yako tu inayoongozwa na Roho mtakatifu.makanisa yote yakinabii na mitume yanahubiri habari za baraka za mwilini magari,nyumba,mke ,mume na watoto.WATU HAWATAKI KUSOMA NENO LA MUNGU WALA KUSALI WANAHITAJI MIUJIZA YA GHAFLA.BILA KUJENGA UHUSIANO NA MUNGU BINAFSI KWENYE MAOMBI NA NENO LAKE UTAZUNGUKA MAKANISA YOTE DUNIANI.
 
Ahsante!

Next time uweke alama ya ulizo (?.) katika swali ili maswali yapungue.Back to your question, si kweli kwamba Uliyemtaja hatozi fedha.

Anatoza fedha (Sadaka) tena hataki mchezo.Pia fikiria nje ya box ya namna ya kutoza fedha (Usiishie kwenye sadaka tu) kwakuwa zipo means nyingi mno za kutozana fedha katika nyumba za Ibada.
Hahahahaaaa jamani
 
Wewe ebu ruhusu ubongo wako ufanye kazi....ni nani aliyekudanganya kuna manabii siku hizi??????
 
nyie ndio ma'ngombe ambayo mkisikia mtalipwa makinikia thamani ya noah moja moja mnashangilia na marinda mnachanua kabisa nyambaaaf.
 
Usipomtaja huyo nabii bila shaka ni uongo.
Hii ndio mara yako ya kwanza kusikia habari hizi za kumuona Mtumishi wa Mungu,nabii au mchungaji anaweka kiasi cha kumuona "ofisini"...?


Mfatilie nabii mmoja anaitwa Frank kilawa nadhani Jibu utalipata.
 
Inaonekana akili zako huzitumii vizuri. Yaani unaambiwa utoe pesa uonane na huyo unayedai mtumishi halafu unashindwa kuelewa kwamba unadanganywa?

Imeandikwa mmepewa bure, toeni bure. Ukiona mtu anadai pesa ili akupe msaada wa kiroho, elewa kuwa mtu huyo hana chochote alichopewa na Mungu. Inawezekana anachotaka kukupatia naye kapewa kwa gharama flani kutoka kwa shetani.
 
Pole sana kwa Masaibu yaliyokupata Mkuu.

Jifunze kuwa Mfuasi wa Kristo na si Mfuasi wa haya Makanisa wala Watumishi wake wa Kimwili.Ukiwa Mfuasi wa Kristo hutohitajika kumuona kwa Fedha wala Sadaka (Gharama ya kuonana na Kristo ni Maombi na kusoma Neno la Mungu).Pia unaonana naye muda wowote.

Ukiisoma Biblia vizuri (Si kusoma vifungu), basi utagundua kuwa tunachezewa abrakadabra nyingi sana na hawa watu wanaojiita Manabii, Wachungaji nk.

Yesu aliagiza "Kuenenda ulimwenguni kuwafanya Mataifa yote kuwa wanafunzi, tukiwabatiza kwa jina la Baba, Mwana na Roho Mtakatifu" (Mathayo 28:19).Si kujenga Nyumba na kuchuna Fedha sehemu miaka nenda rudi.

Hizi sinema za Makanisa lukuki kila uchwao ni Uchafu tu uliojificha kwa mwamvuli cha kueneza neno la Mungu.

Makanisa hayawafundishi watu neno la kweli.Kazi yao ni Kuhubiri kupiga hela tu na si vinginvyo.Hii inakera sana na inarudisha nyuma imani za wachache waaminio.

Mahubiri yametawaliwa na Kupigana vijembe, unazi, ushaitwani nk.Je Injili ya Kristu itafundishwa muda gani?.

Nimeishaachana na haya Makanisa ya dili, Dini yangu iliyo safi isiyo na taka mbele za Mungu ni hii, kwenda kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao, na kujilinda na dunia pasipo Mawaa (Waraka wa Yakobo 1:27).
Kama ni kweli kuwa umeamua kuwatazama wajane na yatima hebu tuambie mpaka sasa umehudumia wajane na yatima wangapi na imekugharimu sh. ngapi katika huduma hiyo?
 
Wanatumia matatizo ya watu kujipatia fedha.Waumini nao kwa kusongwa na shida nyingi wamewageuza watumishi hawa kama waganga wa kienyeji.Waumini hawafundishwi neno la Mungu wanaishia kutishwa na kukamuliwa mpaka senti ya mwisho.Wahuni wengi siku hizi wamejiingiza kupiga dili kwa njia hii ya kutumia matatizo ya watu

Hasa wakina Mama
 
Back
Top Bottom