HS CODE
JF-Expert Member
- Jul 5, 2019
- 1,779
- 4,330
Iwe ni serikalini au taasisi binafsi wapo wafanyakazi wanaotekeleza majukumu yao kwa ufanisi wa hali ya juu sana. Ukikutana nao, watakuhudumia vizuri mpaka utamani wengine wote wangekuwa kama wao. Hawa watu wanahitaji kufahamishwa kwamba ubora wa wanachokifanya tunautambua, ili wapate nguvu ya kututumikia kwa wema zaidi. Soma hii mifano miwili:
Wakwanza
Siku moja nilikuta mzozo mkubwa maeneo ya kivukoni kutoka upande wa Kigamboni, kwenda Magogoni. Kusikiliza kwa makini, nikabaini kuna jamaa aliahidiana na mwenzake kuvuka pamoja, hivyo alipofika eneo la kukata tiketi akakata mbili, yakwake na ya mwenzie. Bahati mbaya huyo mwingine akapata dharura iliyopelekea kutokuvuka.
Ikabidi aliyekata tiketi atafute mtu atakayeinunua moja ili na yeye abaki na nyingine. Shida ni abiria hawakuonyesha kumuamini na wakawa wanakata zakwao mpya dirishani. Jamaa akaona isiwe kesi, akaenda sehemu ya kuskani, akapitisha moja kisha ile isiyoskaniwa akaitia mfukoni huku anakimbia kuingia kwenye pantoni lisimuache. Ghafla wasimamizi wakamuita kwa makelele sana, kufika mahojiano yao yalikuwa hivi:
Msimamizi: Sasa kwanini unatia tiketi mfukoni badala ya kupitisha zote kwenye mashine? (Aliuliza kwa ukali sana).
Abiria: Ni kweli nimeskani moja kwa kuwa navuka mimi mtu mmoja, nyingine bado haijatumika, japo sina mpango wa kurudi kuitumia sijaona ulazima wa kuiskani (Alijibu kwa upole).
Msimamizi: Kuskani tiketi sio maamuzi binafsi, ni sehemu ya utaratibu. Tiketi zote zinazotolewa ni lazima ziskaniwe na sio vinginevyo (Jamaa ndio kwanza akazidi kupandisha sauti).
Abiria: Inawezekana ni kweli uko sahihi, lakini humu kwenye hii tiketi kuna hela yangu ambayo ni haki yangu itakayoisha endapo tu nikiitumia. Hata hivyo pamoja na kuwepo mashine, mbona kuna baadhi yenu mnapokea tiketi mkononi na kuzichana badala ya kulazimisha ziskaniwe? Utofauti uko wapi kati ya hii ninayopita nayo na hizo mnazozichana bila ya kupitishwa kwenye mashine. Au kama itafaa naomba mnirudishie pesa yangu niwaachie tiketi yenu (Abiria akaona unyonge utamkosti, nayeye akawaka, japo hakufikia kwa wasimamizi waliokuwa wanamchangia).
Msimamizi: Maafandeeeeee huyu abiria analeta vurugu njooni mumchukue, akafundishwe adabu.
Basi jamaa wa Suma JKT wakamiminika kwa kasi ya ajabu, hawakutaka kuuliza kitu, hawa jamaa huwa wanajiona ni makomandoo wenye mafunzo ya hali ya juu sana, kumbe hamna kitu. Wakampiga mikwara mingi abiria huku wameshaanza kumkanda makofi ya hapa na pale kadiri walivyoona ina swihi.
Ndipo ghafla akatokea kamanda mmoja wa FFU huwa anamikwara mingi ya kimuonekano, anavaaga kama yuko vitani huku amepiga miwani nyeusi, umri wake umesogea kidogo. Nadhani wengi wanaotumia ile njia wanamfahamu. Ndugu zangu, ule usemi wa sura sio roho ni wa kweli, yule afande alipoelezewa ile shida, akawaambia wale JKT, nyie ni wapumbavu sana. Mnamchelewesha raia kwenye majukumu yake kwa sababu ya hovyo kabisa. Kisha akaingiza mkono mfukoni na kutoa Tzs 200/= akamuamsha jamaa chini alipokuwa amekalishwa kwa mabavu, na kumuomba amuuzie hiyo tiketi.
Kama hiyo haitoshi pantoni lilikuwa limeshaanza kuondoka akamuombea kwa nahodha kupitia zile redio zao asubiriwe, na kweli jamaa akaliwahi na kuvuka upande wa pili. Nadhani unaweza kuona namna kuna watu wana ubinadamu wa hali ya juu.
Wapili
Miaka ya nyuma nilikuwa nafanya kazi ya mkataba wa muda mfupi na NGO fulani ya kimataifa. Ilitokea jukumu linalohitaji kufanya tafiti fulani fulani. Nikapewa maelekezo ya kwenda Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) nikakutane na Dkt. Godwin Kaganda ambaye kwa sasa nilisikia yuko Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMU).
Basi kufika ofisini kwake nikapokelewa na sekretari wake, ni mdada fulani anavaa kiheshima, lugha na muonekano vyote vizuri. Alinikaribisha kwa ukarimu na uchangamfu wa hali ya juu. Nilipomuelezea shida yangu, akanijibu kwa upole kwamba kwa sasa Dokta ametoka kidogo, kama muda unaniruhusu nimsubiri. Yule dada akaniuliza kama natumia kahawa, nikamjibu ndio, akaniwekea huku tunabadilishana mawazo kusogeza muda. Kwa kuwa hana uhakika atarudi muda gani, na nimeshakaa muda mrefu akashauri nimuachie mawasiliano yangu na baadhi ya nyaraka chache kisha nivute subira, atanipigia kunijulisha ni kipi kitawezekana.
Kweli, mchana akanipigia niende, nikakutana na Dokta tukamalizana, nilipokuwa natoka, akaniambia ameona kwenye fomu zangu kuna wengine natakiwa kuonana nao, kwa hao kuwapata watanizungusha sana. Aisee, huwezi amini, alitoa simu na kumpigia mmoja baada ya mwingine, kuwauliza kama wako ofisini kisha akanitambulisha kwamba mimi ni ndugu yake nina suala langu anawaomba wanisaidie lifanikiwe mapema. Dah, wakuu hii kitu ilinigusa sana, mpaka nikajiapiza na mimi popote nitakapokuwa na nafasi ya kuhudumia watu, nitakuwa mwema hata kwa nisiowajua. Na ni kweli, hiyo imekuwa ni moja ya sera zangu za maisha.
Hao ni wachache miongoni mwa wengi waliopewa dhamana ya kutoa huduma na wanafanya kazi zao vizuri sana. Tuwapeni moyo hawa watu. Wewe ni nani ulikutana naye akakuvutia namna ya utekelezaji wake wa majukumu?
Kwa upande wa mazuri kama unamfahamu kwa jina mtaje na ofisi yake, hata kama jina hulikumbuki vizuri au hutaki kulitaja, muelezee kwa namna watu wamtambue, iwe ni tukio lilitokea kipindi kilichopita au hata siku za karibuni, usiache kutupa kisa angalau kwa ufupi tupate cha kujifunza.
Endapo pia kuna mahala hukuhudumiwa vizuri sio vibaya ukaizungumzia kwa maelezo yenye stara bila kulenga kumchafua mtu wala kumdhalilisha, itakayotosha kumfanya muhusika kujijua na kujirekebisha, upande huu naomba tusitaje majina moja kwa moja.
Asante.