Kutoa pesa ili kuonana na mtumishi wa Mungu

Login17

Member
Jun 21, 2017
83
69
Habari zenu wakuu...

Niliomba appointment na mtumishi flan ambaye ni maarufu tu hapa Dar (Nabii) akaniambia yeye anakutana na waumini wake kila siku lakini ili nionane naye ni lazima nitoe kwanza laki 2.2 na ndio utaratibu wake. Nikaamua kwenda ofisini kwake nikakuta utaratibu ni uleule. Sasa nikafikiria maana kwa usawa huu laki 2.2 ni pesa nyingi kwa kama condition ya kumwona mtumishi ili aweze kukuombea.

Hili swala limekaaje wadau? maana limenipa ukakasi sana!
 
Pole sana kwa Masaibu yaliyokupata Mkuu.

Jifunze kuwa Mfuasi wa Kristo na si Mfuasi wa haya Makanisa wala Watumishi wake wa Kimwili.Ukiwa Mfuasi wa Kristo hutohitajika kumuona kwa Fedha wala Sadaka (Gharama ya kuonana na Kristo ni Maombi na kusoma Neno la Mungu).Pia unaonana naye muda wowote.

Ukiisoma Biblia vizuri (Si kusoma vifungu), basi utagundua kuwa tunachezewa abrakadabra nyingi sana na hawa watu wanaojiita Manabii, Wachungaji nk.

Yesu aliagiza "Kuenenda ulimwenguni kuwafanya Mataifa yote kuwa wanafunzi, tukiwabatiza kwa jina la Baba, Mwana na Roho Mtakatifu" (Mathayo 28:19).Si kujenga Nyumba na kuchuna Fedha sehemu miaka nenda rudi.

Hizi sinema za Makanisa lukuki kila uchwao ni Uchafu tu uliojificha kwa mwamvuli cha kueneza neno la Mungu.

Makanisa hayawafundishi watu neno la kweli.Kazi yao ni Kuhubiri kupiga hela tu na si vinginvyo.Hii inakera sana na inarudisha nyuma imani za wachache waaminio.

Mahubiri yametawaliwa na Kupigana vijembe, unazi, ushaitwani nk.Je Injili ya Kristu itafundishwa muda gani?.

Nimeishaachana na haya Makanisa ya dili, Dini yangu iliyo safi isiyo na taka mbele za Mungu ni hii, kwenda kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao, na kujilinda na dunia pasipo Mawaa (Waraka wa Yakobo 1:27).
 
ndo hali halisi...mni jambo la mda mrefu sana...
tuliostuka tumekaa pembeni tunacheki wajinga wanavyoliwa
yasome maandiko yakuongoze kijana..iliandikwa watatokea manabii wa uongo.mbwa mwitu wataojivika msvazi ya kondoo na tutawatambua kwa matendo yao..
kamwe mzabibu hauwezi kutoa tini.
 
Kazi kweli kweli.
Nilikuwa naongea na mkazi mmoja wa jiji la mwanza juu ya mambo haya, aliniambia kitu cha kushangaza kama hiki.
Kuwa yule bwana mwenye tambo nyingi na sijui mhubiri, nabii anyejitambulisha Kwa jina gumu dr geodavies ( sina hakika kama nimeliandika vizuri) alikuwa akitoza shilingi laki moja Kwa kila aliyekwenda kushiriki semina yake iliyofanyika gold crest hotel.
Utapeli katika nyumba za ibada hasa hizi zinazoibuka kila kukicha unazidi kuongezeka huku ule mstari katika biblia kuwa watu wangu wanaangamia Kwa kukosa maarifa ukidhihiri.
Mtu huyo aliniambia juu ya kanisa moja lililoko maeneo ya Nyegezi, Iseni, jijini mwanza ambako eti watu maarufu waliofariki wako ktk kanisa hilo
Anasema kuna viti zaidi ya kumi mbele ambavyo huruhusiwi kuvikalia kwakuwa hapo ndio hao watu maarufu waliofariki wanapoketi!
Ingawa hakuna mtu anayeonekana lkn waumini wanaaminishwa kuwa kanumba , Michael Jackson nk, wako ktk viti hivyo ila huwaonj kwa kuwa unatumia macho ya kidunia!
 
Habari zenu wakuu...

Mimi ni mkazi wa Tabora, nipo Dar kikazi kama week mbili hivi zimepita. Katika upweke na majaribu ya mji huu nikasema ngoja nitafute mahala ili niwe busy kidogo na semina na fellowship ili kushinda majaribu. Sasa kilichonishangaza niliomba appointment na mtumishi flan ambaye ni maarufu tu hapa Dar (Nabii) akaniambia yeye anakutana na waumini wake kila siku lakini ili nionane naye ni lazima nitoe kwanza laki 2.2 na ndio utaratibu wake. Nikaamua kwenda ofisini kwake nikakuta utaratibu ni uleule. Sasa nikafikiria maana kwa usawa huu laki 2.2 ni pesa nyingi kwa kama condition ya kumwona mtumishi ili aweze kukuombea.

Hili swala limekaaje wadau? maana limenipa ukakasi sana!
 
Attachments

  • Screenshot_20170623-191139.png
    Screenshot_20170623-191139.png
    266.5 KB · Views: 61
nakuuliza
Ahsante!

Next time uweke alama ya ulizo (?.) katika swali ili maswali yapungue.Back to your question, si kweli kwamba Uliyemtaja hatozi fedha.

Anatoza fedha (Sadaka) tena hataki mchezo.Pia fikiria nje ya box ya namna ya kutoza fedha (Usiishie kwenye sadaka tu) kwakuwa zipo means nyingi mno za kutozana fedha katika nyumba za Ibada.
 
mmmh sawa mkuu
 
Kazi kweli kweli.
Nilikuwa naongea na mkazi mmoja wa jiji la mwanza juu ya mambo haya, aliniambia kitu cha kushangaza kama hiki.
Kuwa yule bwana mwenye tambo nyingi na sijui mhubiri, nabii anyejitambulisha Kwa jina gumu dr geodavies ( sina hakika kama nimeliandika vizuri) alikuwa akitoza shilingi laki moja Kwa kila aliyekwenda kushiriki semina yake iliyofanyika gold crest hotel.
Utapeli katika nyumba za ibada hasa hizi zinazoibuka kila kukicha unazidi kuongezeka huku ule mstari katika biblia kuwa watu wangu wanaangamia Kwa kukosa maarifa ukidhihiri.
Mtu huyo aliniambia juu ya kanisa moja lililoko maeneo ya Nyegezi, Iseni, jijini mwanza ambako eti watu maarufu waliofariki wako ktk kanisa hilo
Anasema kuna viti zaidi ya kumi mbele ambavyo huruhusiwi kuvikalia kwakuwa hapo ndio hao watu maarufu waliofariki wanapoketi!
Ingawa hakuna mtu anayeonekana lkn waumini wanaaminishwa kuwa kanumba , Michael Jackson nk, wako ktk viti hivyo ila huwaonj kwa kuwa unatumia macho ya kidunia!
Biashara msingi wake ni shida za watu.
 
Habari zenu wakuu...

Mimi ni mkazi wa Tabora, nipo Dar kikazi kama week mbili hivi zimepita. Katika upweke na majaribu ya mji huu nikasema ngoja nitafute mahala ili niwe busy kidogo na semina na fellowship ili kushinda majaribu. Sasa kilichonishangaza niliomba appointment na mtumishi flan ambaye ni maarufu tu hapa Dar (Nabii) akaniambia yeye anakutana na waumini wake kila siku lakini ili nionane naye ni lazima nitoe kwanza laki 2.2 na ndio utaratibu wake. Nikaamua kwenda ofisini kwake nikakuta utaratibu ni uleule. Sasa nikafikiria maana kwa usawa huu laki 2.2 ni pesa nyingi kwa kama condition ya kumwona mtumishi ili aweze kukuombea.

Hili swala limekaaje wadau? maana limenipa ukakasi sana!
Wezi tu hao! Injili gani ya kununuliwa? S-----nzi type!!!
 
Msipokubali kuyasoma maandiko yanavosema, mtasombwa na kila upepo unaopita, na mtatafunwa sana. Maandiko humweka mtu ktk mazingira ya kujua ukweli na atakuwa huru kwel kweli dhidi ya kila aina ya madanganyifu ya wachungaji, manabii, wainjilisti waliokuja na jina la Yesu lakini mioyoni mwao wako mbali nae
 
Back
Top Bottom