Kutoa pesa ili kuonana na mtumishi wa Mungu

Pole sana kwa Masaibu yaliyokupata Mkuu.

Jifunze kuwa Mfuasi wa Kristo na si Mfuasi wa haya Makanisa wala Watumishi wake wa Kimwili.Ukiwa Mfuasi wa Kristo hutohitajika kumuona kwa Fedha wala Sadaka (Gharama ya kuonana na Kristo ni Maombi na kusoma Neno la Mungu).Pia unaonana naye muda wowote.

Ukiisoma Biblia vizuri (Si kusoma vifungu), basi utagundua kuwa tunachezewa abrakadabra nyingi sana na hawa watu wanaojiita Manabii, Wachungaji nk.

Yesu aliagiza "Kuenenda ulimwenguni kuwafanya Mataifa yote kuwa wanafunzi, tukiwabatiza kwa jina la Baba, Mwana na Roho Mtakatifu" (Mathayo 28:19).Si kujenga Nyumba na kuchuna Fedha sehemu miaka nenda rudi.

Hizi sinema za Makanisa lukuki kila uchwao ni Uchafu tu uliojificha kwa mwamvuli cha kueneza neno la Mungu.

Makanisa hayawafundishi watu neno la kweli.Kazi yao ni Kuhubiri kupiga hela tu na si vinginvyo.Hii inakera sana na inarudisha nyuma imani za wachache waaminio.

Mahubiri yametawaliwa na Kupigana vijembe, unazi, ushaitwani nk.Je Injili ya Kristu itafundishwa muda gani?.

Nimeishaachana na haya Makanisa ya dili, Dini yangu iliyo safi isiyo na taka mbele za Mungu ni hii, kwenda kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao, na kujilinda na dunia pasipo Mawaa (Waraka wa Yakobo 1:27).
mie muislam ila nimekupa like maana unajitambua na unaitumia akili yako vizuri kuliko kufata kibubusa
 
Inaonekana akili zako huzitumii vizuri. Yaani unaambiwa utoe pesa uonane na huyo unayedai mtumishi halafu unashindwa kuelewa kwamba unadanganywa?

Imeandikwa mmepewa bure, toeni bure. Ukiona mtu anadai pesa ili akupe msaada wa kiroho, elewa kuwa mtu huyo hana chochote alichopewa na Mungu. Inawezekana anachotaka kukupatia naye kapewa kwa gharama flani kutoka kwa shetani.
Ni kweli
 
Kuna mijitu mijinga kweli kweli na unakuta imejazana.
Sijui hata uncle Magu ameliona kama hili ni eneo la kukusanya kodi.
Mimi naichukulia hiyo ni sawa na kwenda kwa sangoma. Na ukiona anaejiita mtumishi anafanya hivyo hujue hamna kitu hapo ni nguvu za giza ndio zimetamalaki.

Wote wanaijiita manabii na mitume ni wezi tu.
 
Wanatumia matatizo ya watu kujipatia fedha.Waumini nao kwa kusongwa na shida nyingi wamewageuza watumishi hawa kama waganga wa kienyeji.Waumini hawafundishwi neno la Mungu wanaishia kutishwa na kukamuliwa mpaka senti ya mwisho.Wahuni wengi siku hizi wamejiingiza kupiga dili kwa njia hii ya kutumia matatizo ya watu

Ndugu watumishi wa design hii wengi wao ni wachawi wakubwa.
 
Kuna mijitu mijinga kweli kweli na unakuta imejazana.
Sijui hata uncle Magu ameliona kama hili ni eneo la kukusanya kodi.
Mimi naichukulia hiyo ni sawa na kwenda kwa sangoma. Na ukiona anaejiita mtumishi anafanya hivyo hujue hamna kitu hapo ni nguvu za giza ndio zimetamalaki.

Wote wanaijiita manabii na mitume ni wezi tu.
Sio wote. Ukisema wote unakosea na unatenda dhambi ya kuhukumu, ambayo sio kazi yako.
Imeandikwa katika kitabu cha Amosi kama sijakosea kwamba Mungu hatafanya neno lolote duniani kabla ya kuwafunulia manabii. Hizo karama za nabii, mitume, wachungaji,wainjilisti, na walimu, zipo na wapo watu ambao Mungu amewainua na kuwakirimia sawasawa na neni lake.

Kasome biblia yako vizuri na umwombe Roho wa Mungu akufundishe upate ufahamu wa maarifa ili na wewe usiwe mzururaji wa kwenye makanisa ambayo Mungu wa kweli hayupo.

Ubarikiwe
 
Huku waganga feki kule mtumishi wa mungu anataka utoe kiingilio cha laki moja uweze kumuona
na nasikia pia kuna maombi ya elfu 10, maombi.ya milioni moja, n.k kwaio kila maomb yanaenda na uwezo wa mtu..
hayo maombi ya elfu kumi yatakuwa yanadumu dakika moja tu
 
Mmmh ngoja nipite kimya maana huyo jamaa mwenye shati la rangi nyekundu mmmmmh .
 
Nimeona nyumba ya mzee wa upako,kweli wajinga ndio waliwao.
Jamaa anapiga pesa sana
 
Sio wote. Ukisema wote unakosea na unatenda dhambi ya kuhukumu, ambayo sio kazi yako.
Imeandikwa katika kitabu cha Amosi kama sijakosea kwamba Mungu hatafanya neno lolote duniani kabla ya kuwafunulia manabii. Hizo karama za nabii, mitume, wachungaji,wainjilisti, na walimu, zipo na wapo watu ambao Mungu amewainua na kuwakirimia sawasawa na neni lake.

Kasome biblia yako vizuri na umwombe Roho wa Mungu akufundishe upate ufahamu wa maarifa ili na wewe usiwe mzururaji wa kwenye makanisa ambayo Mungu wa kweli hayupo.

Ubarikiwe

Mkuu samahani kama ntakuwa nimekukwaza. Na ni kili mini si msomaji mzuri wa bibilia. Ila hapa namaanisha wale wote wanaodai pesa tena pesa zaidi ya mshahara wa kima cha chini. labda uniambie wasio na pesa hawastahili huduma. Wewe kama ni mtumishi wa Mungu wa kweli kwa nini uchaji pesa kwa wenye shida na neno la Mungu.

Wapiga ramli ndio wanadai watu pesa.

Kwangu mimi kwa yoyote anaedai pesa namuona ni nabii wauongo. wengine wanafikia hatua ya kuuza maji ya ubavu wa yesu, mara machugwa ya upako mara sabuni na hata vitambaa. wafanya biashara tu.

Naamini pia wapo watoa huduma ya haki wengi.
 
Unamfahamu Mtumishi asiyetoza fedha Mkuu?.

Kama ndiyo, please nielekeze anapopatikana.
Nenda ubungo barabara ya kwenda kibangu utakuta barabara ya vumbi nadhani inaitwa jeshini kuna prophet anaitwa Clear Malisa. Hatozi hata mia ila uwezo aliopewa sio wa nchi hii.
 
Kama ni kweli kuwa umeamua kuwatazama wajane na yatima hebu tuambie mpaka sasa umehudumia wajane na yatima wangapi na imekugharimu sh. ngapi katika huduma hiyo?
Heshima Boss!

Umelazimisha kunielewa makusudi ndiyo maana hujanielewa nilichokimaanisha.Naomba ukanisome tena kwa mara ya pili then utanielewa.

Pia unipe jibu la hili swali "Kwanini unadhani kuwatizama Yatima na Wajane ni mpaka utumie fedha"?.Msaada kwako unamaanisha nini?.

Je unajua kuwa matumizi ya fedha yameanza kutumika mika gani iliyopita?.Kama ndiyo, Je huku kuwatizama Yatima na Wajane katika dhiki yao ilikuwa na maana gani/ipi?.Tafakari..

Eid njema, Nb;Kama ni muumini wa Madhehebu ya Mashariki ya mbali.
 
Nenda ubungo barabara ya kwenda kibangu utakuta barabara ya vumbi nadhani inaitwa jeshini kuna prophet anaitwa Clear Malisa. Hatozi hata mia ila uwezo aliopewa sio wa nchi hii.
Ahsante kwa Majibu, ila n'na swali dogo!

Kwanini unadhani uwezo aliopewa siyo wa nchi nchii?.
 
Pole sana kwa Masaibu yaliyokupata Mkuu.

Jifunze kuwa Mfuasi wa Kristo na si Mfuasi wa haya Makanisa wala Watumishi wake wa Kimwili.Ukiwa Mfuasi wa Kristo hutohitajika kumuona kwa Fedha wala Sadaka (Gharama ya kuonana na Kristo ni Maombi na kusoma Neno la Mungu).Pia unaonana naye muda wowote.

Ukiisoma Biblia vizuri (Si kusoma vifungu), basi utagundua kuwa tunachezewa abrakadabra nyingi sana na hawa watu wanaojiita Manabii, Wachungaji nk.

Yesu aliagiza "Kuenenda ulimwenguni kuwafanya Mataifa yote kuwa wanafunzi, tukiwabatiza kwa jina la Baba, Mwana na Roho Mtakatifu" (Mathayo 28:19).Si kujenga Nyumba na kuchuna Fedha sehemu miaka nenda rudi.

Hizi sinema za Makanisa lukuki kila uchwao ni Uchafu tu uliojificha kwa mwamvuli cha kueneza neno la Mungu.

Makanisa hayawafundishi watu neno la kweli.Kazi yao ni Kuhubiri kupiga hela tu na si vinginvyo.Hii inakera sana na inarudisha nyuma imani za wachache waaminio.

Mahubiri yametawaliwa na Kupigana vijembe, unazi, ushaitwani nk.Je Injili ya Kristu itafundishwa muda gani?.

Nimeishaachana na haya Makanisa ya dili, Dini yangu iliyo safi isiyo na taka mbele za Mungu ni hii, kwenda kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao, na kujilinda na dunia pasipo Mawaa (Waraka wa Yakobo 1:27).
Wako hivyo wana viwango rasmi kabisa kwa kila huduma na malipo ni kabla si baada
 
Back
Top Bottom