Kutoa hela UTT changamoto CRDB

Kutoa hela UTT changamoto CRDB

Kwa hiyo hizo za BOT ni mpaka watangaze, huwezi kwenda kujinunulia siku ukiwa na pesa?
Ingia Instagram, tafuta namba ya Solomon Brokers. Wao ni mawakala wa stock market na UTT watakua na majibu ya maswali yako yote. Ukitaja tu jina la kampuni kuna watu huwa wanahisi labda ni tangazo la biashara, kama ni mtu wa kujituma basi hutakuwa na maswali tena. Tafuta any broker, piga simu na utapata msaada.
 
Mkuu Mi sina HAja ya kubishana na wewe kuhusu SIku ya kupata peaa yako baada ya kujaza fomu. Nilitoka pesa mwezi WA nne ilikuwa SIku ya Jnne nilipojaza fomu pesa nilipata ijumaa. Nikatoa pesa tena mwezi WA Saba pesa nilipata ñdani ya SIku mbili yaani siku mbili baada ya kujaza fomu. Kama humu kungekuwa safe Sana ningeweka namba ya Jamaa aliyeko makao makuu DSM apigiwe maana ndiye huwa nawasiliana Nate toka nmefungua akaunti kwao mi sizungumzii uzoefu wako hapa nazungumzia reality kabisa za juzi juzi Tu hapa pesa unapata baada ya SIku mbili baada ya kujaza fomu
Mkuu hebu dadavua zaidi, nasikia inategemea na kiasi cha fedha unachohitaji kutoa. Kama ni kikubwa wanakusumbua ukate tamaa
 
Pesa za utt hazitoki. Nini kinaendekea wakuuu..au tumepigwa
 
Dunia ya leo mkuu bado unajaza fomu? Kwanini usiwe na app?? Ni rahisi zaidi na hakuna kulipa 23k
 
Ukisema hazitoki unamaanisha nini??
Kwanza app yao haifanyi kazi.. customer care hawapikei simu au wakipokea wanasema tusubiri.. Kifupi hawapo hewani saivi .. ni zaidi ya mwezi nilitakiwa kupewa pesa pia na jamaa wengine wawili wanasema ni mzunguko huu huu..
 
Kama uko mkoa ambao una ofisi, nenda. Lakini nimekua nikifanya transactions kwenye mfumo na inakubali fresh tu.
Mkuu last time kufanya ni lini.. kwa kua hata app haifanyi kazi.. walisema wana update kwa kuleta app mpya toka hapo nikiwauliza wanasema app haipo tayari mpaka iwe tayari ndo watatujuza na transaction hazifanyiki
 
Back
Top Bottom