Kutoa hela UTT changamoto CRDB

EL ELYON

JF-Expert Member
Jan 2, 2013
1,563
1,886
Wakuu mmebarikiwà Sana na Mungu WA Mbinguni.

Nilikwenda kujaza fomu za UTT Benki CRDB Kwa lengo kutoa pesa yaani re purchase units.

Baada ya kumaliza kujaza fomu nikaambiwa nilipie elfu 23 kwa madai kwamba ni gharama ya kumtuma fomu.
Nikaelekezwa niende kwenye dirisha la teller nilipe nilipofika pale nashangaa teller ananiambia huyo aliyekutuma amekupa akunti namba NENDA umwambie akupe akaunti namba.

Nikarudi Kwa aliyenielekeza niende Kwa teller nikamueleza akaanza kuzugazuga pale kisha akanipa akaunti namba nikalipa.

Sasa jUZi Tena NimEkwenda kujaza fomu ili nitoe pesa UTT nilipomaliza kujaza nikapeleka Kwa wahusika Benki crdb wakawa kama hawajari vile yaani wako busy na Mambo mengine. Nilichokifanya nikaitelekeza kwenye meza moja ya wahusika nikaondoka zangu sasa jioni nikapigiwa simu na Mtu WA Benki akaniulza je fomu yangu waitume au waiache.

Nikamjibu ñdiyo itumwe kwani si ndo maana nimeijaza akanambia Sawa anaituma.
Mkumbuke sikuwa nmelipia kama Ile ya mwanzo.

Sasa hoja yangu au swali langu je tunapokwenda kujaza fomu za UTT Kwa lengo la kutoa pesa ni kweli inatakiwa ulipie fomu gharama ya kumtuma ambayo ni elfu 23 au ni free maana kuna SIku nililipia ikaenda na jUZi sikulipia na imetumwa.

Asanteni.

Karibuni kwa majibu, kejeri, povu, matusi, dharau NK.
 
Kwa kawaida fomu ya kutoa pesa kwenye akaunti ya UTT hujazwa kwenye ofisi za UTT, pesa unayotaka kutoa huingizwa kwenye akaunti yako baada ya siku saba.

Sina hakika na hiyo 23000tsh uliyoombwa kama iko kihalali... Jaribu umuone Manager wa tawi kwa ufafanuzi.
 
Fomu za UTT kwenye mikoa ambayo hawana ofisi au kama UKo mbali na UTT basi wakala ni crdb fomu zipo hapo Benki iwe ni kuweka au kutoa na ndo maana hata wao UTT hushauri mtu awe na akaunti ya crdb.
Pesa inaingia ndani ya siku 3 si Saba labda we Una taarifa za zamani.

Kiukweli hiyo elfu 23 Nina wasiwasi wale wafanyakazi WA Benki wanaipiga wao Tu kijanja ndo maana hata siku ya Kwanza KWENDA kutoa walisema nikalipe Kwa teller wakaanza kurushiana mpira kuhusu akaunti ya kuweka pesa hiyo. Nadhan Kila mmoja hakutaka lawama kuhatarisha kazi yake. HII mara ya pili sjatoa hela na fomu wameituma.
 
Baadhi ya wafanyakazi wa benki hawafahamu itifaki zinazotumika kati yao na UTT, inawezekana hata managers wanakwama. Mimi ni mwanachama UTT tangu ilipoanza hadi leo !. Hakuna utaratibu wa kutozwa 23000 unapotoa pesa.

Hiyo siku tatu kuingizwa pesa yako kwenye akaunti pia sio kweli!. Inachukua siku saba hadi kumi! Hii nakupa uzoefu wangu ndani ya UTT zaidi ya miaka kumi.
 
Baadhi ya wafanyakazi benki wa hawafahamu itifaki zinazotumika kati yao na UTT, inawezekana hata managers wanakwama. Mimi ni mwanachama UTT tangu ilipoanza hadi leo !. Hakuna utaratibu wa kitozwa 23000 unapotoa pesa.

Inategemea na aina ya account, inaonyesha wewe sio mteja wa liquid fund. Bond fund ni moja ya account zinazokaa hizo siku unazosema
 
GwaB, vipi ile faida wanayotangaza kutoa kulingana na aina ya uwekezaji..vipi wanatoa kwa wakati?
 
Baadhi ya wafanyakazi benki wa hawafahamu itifaki zinazotumika kati yao na UTT, inawezekana hata managers wanakwama. Mimi ni mwanachama UTT tangu ilipoanza hadi leo !. Hakuna utaratibu wa kitozwa 23000 unapotoa pesa.

Hiyo siku tatu kuingizwa pesa yako kwenye akaunti pia sio kweli!. Inachukua siku saba hadi kumi! Hii nakupa uzoefu wangu ndani ya UTT zaidi ya miaka kumi.
Mkuu Mi sina HAja ya kubishana na wewe kuhusu SIku ya kupata peaa yako baada ya kujaza fomu. Nilitoka pesa mwezi WA nne ilikuwa SIku ya Jnne nilipojaza fomu pesa nilipata ijumaa. Nikatoa pesa tena mwezi WA Saba pesa nilipata ñdani ya SIku mbili yaani siku mbili baada ya kujaza fomu. Kama humu kungekuwa safe Sana ningeweka namba ya Jamaa aliyeko makao makuu DSM apigiwe maana ndiye huwa nawasiliana Nate toka nmefungua akaunti kwao mi sizungumzii uzoefu wako hapa nazungumzia reality kabisa za juzi juzi Tu hapa pesa unapata baada ya SIku mbili baada ya kujaza fomu
 
UTT ni kitu gani?
 
Sawa... Unaweza kunifafanulia hiyo 23,000 tsh uliyoambiwa ulipe kwanza ni ya nini?.
 
Baadhi ya wafanyakazi benki wa hawafahamu itifaki zinazotumika kati yao na UTT, inawezekana hata managers wanakwama. Mimi ni mwanachama UTT tangu ilipoanza hadi leo !. Hakuna utaratibu wa kitozwa 23000 unapotoa pesa.

Hiyo siku tatu kuingizwa pesa yako kwenye akaunti pia sio kweli!. Inachukua siku saba hadi kumi! Hii nakupa uzoefu wangu ndani ya UTT zaidi ya miaka kumi.
Ni sawasawa. Nami pia ni mwanachama. Unajaza fomu ofisini. Fedha yako inatumwA ndani ya siku kumi za kazi kwenye akaunti yako ya benki. Ikiwa haikutumwa kuna namba za simu ambazo utapiga ambazo hata kama huna salio zitaita utataja taarifa zako. Ikiwa jambo lako halitapata majibu ya moja kwa moja watakupigia simu baada ya muda mfupi ndani ya siku hiyo hiyo kukujuza kuwa jambo lako limefikia wapi
 
Nilikuwa na vipande 1000 wakati wanaanza nikavuna 900 ..vile 100 si vitakuwapo bado !!?? Siku mingi sana tangu 2007/8
 
GwaB, vipi ile faida wanayotangaza kutoa kulingana na aina ya uwekezaji..vipi wanatoa kwa wakati?
Faida inaingizwa kwenye akaunti yako, ili ujue kama inaingizwa kwa wakati ni lazima usubiri wakutumie statement. Nakumbuka kuna wakati niliwahi kugombana nao kwenye hilo. UTT wanakutunzia hesabu na thamani ya vipande vyako kwenye makaratasi wakati pesa iko benki.
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom