CRDB rekebisheni mifumo yenu ina kasoro ndogondogo.

CRDB rekebisheni mifumo yenu ina kasoro ndogondogo.

Mkumbwa Jr

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2016
Posts
2,702
Reaction score
3,839
Ukiingia kwenye App ya CRDB inakua haina usumbufu tatizo ni mrejesho wa ujumbe wao.
Unaambiwa umetuma hela kwa kutajiwa akaunti namba yako lakini hutajiwi namba na jina la uliyemtumia hela.
Kwanini msirudishe majibu kwa kutaja namba na majina ya aliyetumiwa hela? Hii inasaidia hata kufanya mapitio kibiashara. Watu wanalazimika kujaza fomu kwasababu taarifa zenu hazijakaa sawasawa. Hivyo kutumia mda mwingi kwajambo linaloepukika.

Kwenye hili jifunzeni kwa benki kongwe nchini NMB.

Ukitaka sasa kutoa hela kwa menyu yao hapo utakutana na maswali kibao yakujirudia. Mfano ukiwa katikati ya utaratibu unaulizwa accont inayotumika. Sasa account inayotumika mtu siashaingia tangu mwanzo na aliingiza namba ya siri? Punguzeni maswali. Rekebisheni mifumo yenu

Ninamalizia kwa kusisitiza kwamba rudisheni ujumbe unaoonesha jina na account namba ya aliyetumiwa fedha
 
Back
Top Bottom