Kutimiza ahadi kwa kiongozi ni taswira ya heshima yake: Ahadi ya mama ya goli moja sh 10M kwa Simba

zeuman

JF-Expert Member
Aug 2, 2023
261
480
Wote tulisikia na tulielewa!! Kuwa mama amewaahidi simba sh 10M kwa kila goli watakalofunga!! Hayo maelezo ya ziada hakuyasema na hatukuyasikia (kuwa simba mpaka ishinde, kama angekuwa amesema hivyo, Msigwa asingekuwa na sababu ya kutoa maelezo na Simba isingetarajia pesa hizo) na yamekuja kusemwa baada ya jasho kuvuja na simba kupata magoli 2 hapo kwa Mkapa, hivyo mama kujua simba inatarajia hizo pesa.

Huko Misri Simba ilipata goli moja!! Mama anadaiwa sh 30M na Simba!! Naomba mama alinde heshima yake kwa kutunza na kutimiza ahadi yake!! Asitafute mpenyo wa kukwepa!! Halafu huko nyuma aliwahi kutoa hizo pesa kwa timu iliyofungwa!! Mama ni wa wote!!

Chonde chonde mama itabidi tu utoe hizo 30M. Vinginevyo hiyo haikuwa ahadi ya dhati bali ilikuwa ni kejeli kwa kuamini kuwa simba haina uwezo wa kufunga goli dhidi ya Al Ahly).

Bila kutimiza ahadi ujue kabisa kuwa umejipatia doa kubwa katika vigezo vya kuaminika na uadilifu!! Huyu mh Msigwa asikuingize chaka!!​
 
Ni kweli kabisa kushindwa kutimiza ahadi kwa mtu ni nonsense!! Haileti mantiki nzuri!! It is opposed to sense (hence nonsense) in failing to abide to one's pledges!! Kinachosikitisha ni haop wasaidizi ambao walipaswa kumsaidia mama, ndo wanakuwa wa kwanza kumwandalia mazingira ya kuonekana si wa kuaminika!!
 
Msigwa alisema toka siku ya kwanza, kila goal la ushindi
Siyo kweli!! Kama ingekuwa ni hivyo Msigwa asingekuwa na sababu ya kujieleza sana baada ya ushindi na simba isingedai wala isingetarajiwa kudai!! Msigwa amemfedhehesha sana mama!! Inabidi ajiuzulu ili kulinda heshima ya mama!! Uto walipewa japo walifungwa, sembuse sare!! (Japo kigezo cha madai si kwa kuwa uto walipewa, ila ni kwa sababu mama aliahidi).
 
Tatizo watu wa dar huchanganya neno kushinda na kufunga goli,dar kufunga goli wanasema kibu kashinda moja,chama kashinda moja,huko ni kufunga goli siyo kushinda, kushinda ni matokeo ya jumla
Sahihi kabisa

Siyo kila goli ni goli la Ushindi

Ila Makolokolo FC Wapewe tu hiyo 30 😂😂😂 Goli ni Goli mura!
 
Tatizo watu wa dar huchanganya neno kushinda na kufunga goli,dar kufunga goli wanasema kibu kashinda moja,chama kashinda moja,huko ni kufunga goli siyo kushinda, kushinda ni matokeo ya jumla
Hakuna asiyejua kiswahili na wote tulisikia na hii haikuwa mara ya kwanza!!! Tunatetea uadilifu wa mama!! Msigwa ajiuzulu!! Hajaonesha heshima kwa mama!! anamfedhehesha mbele ya jamiii, hamna namna ni lazima ajiuzulu na mama atoe hizo 30M kulinda hashima na uadilifu wake!!
 
Timu ikiwa timu imeshinda ndilo tamko la mwisho la mama. Nililisikia.

Kwa kuwa umepata goli tu, bila ushindi wa mechi hiyo ulipwe? Ujinga huo.
 
Sasa kwani kiswahili kinahusianaje na kukaa Dar wapo watu wanakaa Tanga ,Zanzibar, pemba na Mombasa na hawajui kiswahili vilevile
Uhusiano wa kiswahili na Dar ni kwamba asili ya Kiswahili kwa Tanzania ni ukanda wa pwani.
Ukimuona mkazi wa Dar hajui kiswahili huyo sio mswahili atakuwa mhamiaji.
 
Uhusiano wa kiswahili na Dar ni kwamba asili ya Kiswahili kwa Tanzania ni ukanda wa pwani.
Ukimuona mkazi wa Dar hajui kiswahili huyo sio mswahili atakuwa mhamiaji.
Vipi kuhusu Zenji (unguja na pemba) ,Bagamoyo,Mombasa,Tanga na Pwani nyingine wapo ambao kiswahili kinawashinda na ndo kilianzia huko kabla ya Dar
 
Back
Top Bottom