Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 364,938
- 842,522
Bado naikumbuka siku ile mgombea wa CCM alipotangazwa mshindi na siku zilizofuatia mpaka kuapishwa kwake.... Sikuona shamrashamra zozote na nchi ilikuwa kama kwenye msiba mkubwa... Sikuona shangwe zozote.. Popote... Kuanzia kwenye mitandao ya kijamii mpaka kwenye vijiwe mitaani na sehemu za starehe... Watu walijitenga vikundi vikundi wakijadiliana kimya kimya... Walikuwa hawaamini kwamba ccm imerudi madarakani tena, licha ya madhila yote kwa zaidi ya miaka 40.! Nyuso zao ziliakisi masononeko rohoni....
Wengi walijua baada ya usiku mrefu sana hatimaye kumepambazuka.... Kumbe jimbi liliona mwanga wa mwezi likawika likijua kumekucha....
Kila kitu hutokea kwa sababu... Hakuna kitu kinachoitwa bahati mbaya! HAKUNA....Gari huanza kukosa mwelekeo, huyumba na mwishowe hupinduka... Na kusababisha vifo majeruhi ama ulemavu
Gari yetu kama taifa gari yetu ilikosa mwelekeo mara baada ya mwalimu Nyerere kung'atuka mwaka 1985... Ukisoma kile kitabu chake cha UONGOZI WETU NA HATIMA YA TANZANIA.. utaona wazi kabisa kwamba aliona kila dalili za gari kuyumba
Akaingia mzee Mwinyi akapiga kona kali sana bila hadhari kwa kufungua milango ya biashara huria... Huu ndio ukawa mwanzo wa kuua viwanda vyetu vya ndani, ujasiriamali na ubunifu wetu vikazikwa rasmi... Ikawa ni mwendo wa mitumba toka nje.... Gari ikaacha njia kuu na kuchanja mbuga kuelekea vichakani
Awamu ya mzee Mwinyi ikaisha, akachukua mzee Mpaka, akataka kurekebisha makosa ya mtangulizi wake bila hadhari pia, yani akataka kulirudisha njia kuu gari lile bila kupunguza mwendo... Akafanya ubinafsishaji mkubwa, alichokijenga Nyerere kwa miaka 37, Mkapa akakibomoa overnight... Mashamba makubwa, viwanda vyetu na maghala ya mabilioni tukayauza kwa bei ya kutupa kwa jina la ubinafsishaji! Migodi yetu mashirika yetu ya biashara nk, tukauza vyote...
Wale wageni walioua viwanda vyetu ndio hao hao wakaja kuvinunua kwa bei ya kutupa.... Mpaka akamaliza awamu yake kwa staili hii... Akiwa kaacha matabaka makubwa kati ya walio nacho na wasio nacho... Mgeni alikuwa anapewa daraja la kwanza, mzawa mlalahoi daraja la pili
Movie ya kuyumba gari inaendelea akaingia Jakaya.. Huyu hakutaka kuumiza kichwa hakujua aanzie wapi wala aishie wapi akaacha mambo yaende kama yalivyo.. Akafanya alichoweza lakini bila kujenga misingi yoyote.... Alipozidiwa kabisa akaacha gari liingie kwenye auto mode drive... Likiweza lirudi njia kuu likishindwa liendelee kuchanja mbuga... Hakutaka pressure
Jakaya kaondoka na akaleta mpokea kijiti ambaye anataka kurudisha misingi ile iliyojengwa na mwalimu Nyerere... Lakini kwa kutumia nguvu nyingi na akili binafsi.. Hataki shirika hata ushauri,... Lakini matumizi ya nyakati ni kitu muhimu sana... Tafakuri inahitajika sana kwenye hili....
Ni rahisi kuchonga kinyago kizuri toka kwenye gogo.. Lakini ni ngumu mno kurekebisha kinyago kilichokwisha haribiwa
Ndugu zetu wote hawa kwa nyakati zao wote wamesahau mambo muhimu ya kitaifa na kung'ang'ania chama kubaki madarakani..... Tabu yetu yote huu ndio mzizi wake lakini hata usiku uwe mrefu kiasi gani... KUTAPAMBAZUKA....

