Kutangulia sio Kufika; Goli la mapema

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,894
KUTANGULIA SIO KUFIKA; GOLI LA MAPEMA

Anaandika, Robert Heriel
Jasusi

Wengi wanapenda kutangulia, hata Mimi ni mmoja wao. Napenda magoli ya mapema, napenda ushindi wa mapema.
Ushindi wa mapema ni mtamu Sana. Ushindi wa mapema unafaida zake nyingi mno ingawaje zipo hasara.
Kama ungenikuta nikiwa na- dribble Mpira Enzi hizo, namba Saba, kwenye chandimu basi, nilikuwa napenda kuhakikisha timu yetu inafunga mabao ya mapema.

Falsafa ya ushindi wa mapema ni chachu Kwa Watu wote Makini na wenye Akili. Sisi wenye Imani ndogo kiukweli hatuamini muda hasa hatunaga Imani na dakika za lalasalama. Sisi tunaamini katika alfajiri na mapema,
Kama ni kwenye ngumi, ushindi wetu tutahakikisha tunaupata dakika za mwanzo, unaweza kuita timing Wakati MTU akiwa hajajiandaa vizuri. Unapiga moja tuu! Chalii Watu wanashangilia.

Tatizo lako Taikon unapenda kuandika madude marefu, embu fupisha!
Sawa nimewaelewa!

Katika sekta ya kijasusi, wale wanaoteuliwa kufanya Mauaji, HITMAN
Moja ya Kanuni muhimu ni kumchagua Hitman Mvivu ambaye kivyovyote atataka ushindi wa mapema, yaani ataifanya kazi yake mapema, Kwa wepesi bila kutumia nguvu kubwa. Ingawaje ili uwe hivi lazima uwe Smart.
Raha ya goli la mapema ndio hiyo. Utafanya Kwa wepesi, hautatumia nguvu kubwa, Kwa sababu adui bado hajajipanga vyema, pia anajua muda anao, hapo ukipiga right target mchezo umeisha. Unarudi zako kulala au Kula bata.

Kanuni hizi zimetumiwa na mabingwa wote Duniani, Kanuni hiyo hutumiwa na wafanyabiashara pia, ambao husema Biashara Asubuhi jioni mahesabu. Kifursa ni muhimu MTU kuifanya biashara au fursa Mpya mapema Kabla Watu hawajaishtukia. Elewa kuwa Watu wengi Hawana macho ya kuona mpaka waone MTU akifanya, pengine wengine ni waoga sio wathubutu hivyo huogopa kuanza vitu vipya, hivyo wanasubiri muanzilishi kisha wao wafuate Nyuma.

Katika uwindaji, Simba au chui anapowinda hufanya mashambulizi ya kushtukiza na yamapema zaidi Kabla hajashtukiwa na Prey "windo lake" lakini pia Kabla kina Fisi hawajafika. Bado tupo kwenye Goli la mapema, au ushindi wa mapema.

Kwa Wanafunzi, Wanafunzi wote wajanja hutumia pia Kanuni hiihii ya chukua chako mapema, shinda mapema. Nyakati tunasoma chuo kikuu moja ya mbinu za kimedani nilizokuwa nazitumia ni kuhakikisha coursework inasoma alama za juujuu ili kujihakikisha kuwa UE(mtihani wa mwisho) hautanisumbua. Hivyo zile individual assignments au group assignments na zile test nilikuwa nahakikisha napata marks nzuri ili kujihakikishia usalama katika mitihani ya mwisho. Mbinu hiyo inafanya kazi kwani itakuzuia Kupata Supplementary au kukeri kozi.
Pia itakufanya uishi chuo Kwa raha mustarehe ukifurahia Maisha ya chuo pamoja na warembo au mishe za Club, kama mnavyojua Ujana.

Kwenye mahusiano, ewe Binti, Umepata kakijana kako, ni kweli unakapenda na kanakunyotoa nyotoa moyoni, kapige Kata funua za mapema kujihakikishia ushindi, lakini kamwe usionyeshe umeshinda au umekashinda, lakini pia usionyeshe Kwa marafiki zako the way uko happy na huyo Boy Mpya. Jitahidi ku-fake ni mbinu muhimu katika mapambano.

Kutanguliwa ni kutanguliwa tuu. Hakuna kazi ngumu kama kurudisha Goli.

Katika ujasusi, unaweza kumtangulia mtu kumbe alishakutangulia muda mrefu. Yani unamshinda MTU aliyekushinda bila ya wewe kujua. Hii ni Ile unampeleleza MTU ambaye anakupeleleza na anajua unampeleleza.
Alafu kuna Ile unampeleleza MTU hajui unampeleleza. Yaani unamshinda MTU asiyejua umemshinda.

Kwenye upelelezi hakunaga kitu inaitwa Imani, kuridhika, kuamini kuwa upo salama. Muda wote ni kuwa macho. Kwa sababu kile usichokijua ndicho kitakachokushinda, na kile unachokijua ndicho utakachokiweza.

Kutangulia sio kufika, hiyo kauli muhimu na nyeti katika mapambano yoyote ya Majasusi.

Unaweza kutangulia Kuoa au kuolewa, ukadhani umefika kumbe haujafika, ndani ya miaka Mitano au kumi unapiga mzinga, umekwama.
Wale uliokuwa unawacheka wamekosa Waume wa kuwaoa wanakutazama tuu, wao muda huo NAO wapo kwenye Ndoa.
Wewe unahangaika na kugawana Mali, kutupiana matusi, yaani ni kwamba mechi inakushinda.

Ni lazima kila hatua ihesabiwe, itolewe macho na hesabu yake.

Umetangulia kujenga nyumba, lakini hiyo sio Guarantee ya kuwa ndio umefika. Hujawahi kuona MTU kajenga nyumba lakini ameikimbia? Hausikii kesi Mahakamani za kugawana Mali au nyumba kuuzwa? Unafikiri ule ulikuwa ni ushindi au ni Goli la mapema tuu?

Kijasusi, unaposhinda Goli la mapema haupaswi kushangilia, unapopata windo au unapolenga Target hautakiwi kupiga piga Kelele. Wakati hata mechi haijaisha.

Ooh! Taikon usitupangie Maisha!
Noop! Sikupangii Maisha, hapa si tunapiga tu Stori!

Anyway! Kama hautaki Stori zangu za Kitibeli Fresh!
Zingatia Wakati WA Kula Watu hawapigi Kelele,

Mimi ngoja Nilale, tutaendelea nikiamka!

Sabato NJEMA

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Mbona mechi nyingi timu huwa zinashinda na goli la mapema tu mkuu.Unakuta bao linapigwa mapeemaa dakika ya 2 na bao Hilo likasimama mpaka mechi inaisha.
 
Nazani kitu ambacho mtu anatakiwa kukifanya baada ya kupata goli la mapema Ni kutafuta mbinu muafaka ya kulilinda Hilo goli la mapema ili lisije likapotea.
Anza kwa kulilinda Hilo goli Kisha uanze kutafuta magoli mengine ya kuongezea.
😀😀
Sijakataa
 
Daah

Leo nmitoka NUNGE TAIKON Sijaambulia chochote mwalimu

Katika battle yoyote uhakikishe unashinda mapema ili kujiwekea usalama na wala usiwacheke wale ambao hawajashinda yaani uko ndani ya gari unamcheka mtembea kwa miguu, mbele kidogo unapata ajali na gari inakua rightoff na wewe unarudi kutembea kwa miguu, lakini kazungumzia kutokukata tamaa kwenye mapambano yaani muandishi amekumbusha umuhimu wa kujitambua kwenye maisha halisi
 
90 minutes meza za pinduliwa .... Kikubwa utanguliapoo usijisahauuu wengine wakaja na mbio za farasii
 
Katika battle yoyote uhakikishe unashinda mapema ili kujiwekea usalama na wala usiwacheke wale ambao hawajashinda yaani uko ndani ya gari unamcheka mtembea kwa miguu, mbele kidogo unapata ajali na gari inakua rightoff na wewe unarudi kutembea kwa miguu, lakini kazungumzia kutokukata tamaa kwenye mapambano yaani muandishi amekumbusha umuhimu wa kujitambua kwenye maisha halisi

Hii ndio Ile fupisha habari Kwa maneno hamsini.
Somo la ufupisho ulifanikiwa kulielewa
 
Nazani kitu ambacho mtu anatakiwa kukifanya baada ya kupata goli la mapema Ni kutafuta mbinu muafaka ya kulilinda Hilo goli la mapema ili lisije likapotea.
Anza kwa kulilinda Hilo goli Kisha uanze kutafuta magoli mengine ya kuongezea.

Exactly!
Màgoli ya mapema mara nyingi yanafanana na lile Goli la dakika za lalasalama
 
Back
Top Bottom