Kutangazwa Arusha kuwa jiji

Wanatujazia foleni tu hapa. Kesho itabidi nidamke niwahi kazini! Period.....
 
Katika hali isiyokuwa ya kawaida ni kwamba mamia ya watu wamezombwa kutoka sehemu mbali mbali za mkoa wa Arusha kuhudhuria uzinduzi wa jiji la Arusha hapo kesho.
Hotel za hapa jijini Arusha tayari zimeshajaa na wakazi wa Arusha wametoa tahadhari kwamba uzinduzi wa jiji kesho usihusishe siasa zozote especially za ccm maana wataipinga hali hiyo kwa nguvu zote.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Ni kweli kaka,nimeshuhudia kwa macho yangu maeneo ya makao mapya,majengo na katikati ya jiji
 
Kwa kumbukumbu zangu ni kuwa Arusha iliondolewa hadhi ya JIJI kipindi kile kutokana na kutokidhi matakwa ya JIJI,
Hivyo ikaonekana ni bora kusogeza mbele tarehe ya kupewa hadhi ya JIJI huku wakirekebisha hayo matakwa,
Cha kushangaza sana sababu hazijulikani ni zipi zilizuia Arusha isiwe JIJI kipindi kile, na kama hizo sababu/matatizo sasa yametatuliwa au LA?

Arusha ina barabara kadhaa za kuingia katikati ya JIJI
Njia ya Moshi/Arusha kwa wanaotokea Moshi na pande hizo
Njia ya Namanga kwa wanaotokea Nairobi, Namanga na kwingineko
Dodoma road, hii kwa wanaotokea Babati, Singida, Kondoa, Ngorongoro nk
Barabara ya Mdauda inayotokea Kwa Mromboo, hii ni kwa wale wanaotokea Oljoro, Simanjiro nk
Nelson Mandela Road, hii inaunganika na Moshi/Arusha maeneo ya USA river
Na barabara ya Njiro ielekeayo VETA na kwenda hadi Simanjiro
 
Kwa Arusha kutangazwa kuwa jiji na ona ni haraka tu! Mji wa Arusha una changamoto nyingi ambazo wange zishughulikia kabla ya kutangazwa kuwa jiji.
Changa moto kama!
1 barabara hili ni tatizo kubwa hata zilizopo ni nyembamba sana, kwakweli huu mji una hitaji barabara za kutosha ni haibu kusema Arusha ni jiji labda kwa mtu ambaye ajawai kuishi au kupita Arusha anaweza asishangae!
Japo miundo mbinu si kigezo pekee lakini kwa hili kuna udhaifu sana!
Kwakweli ni bora nguvu nyingi zingeelekezwa kwenye kuuboresha mji huo, sijajua hiyo haraka ni ya nini?

Ukweli lazima usemwe Arusha bado huku ni kujifariji, lakini pamoja na vitega uchumi vingi vilivyoko hasa utalii nashangaa mji wa Arusha kuwa na miundo mbinu hafifu!

Linganisha Arusha na Tanga, Mbeya na Mwanza useme zipi zilistahili kuwa majiji kabla ya mengine na utoe sababu. Kwa mimi Mbeya kuitwa jiji si sawa kwani pia nayo iko backward kwa mambo mengi. Huwezi linganisha hiyo miji niliyoitaja na Arusha labda iwe wewe hujawahi ishi Arusha labda huwa unapitaga tu.
 
Katika hali isiyokuwa ya kawaida ni kwamba mamia ya watu wamezombwa kutoka sehemu mbali mbali za mkoa wa Arusha kuhudhuria uzinduzi wa jiji la Arusha hapo kesho.
Hotel za hapa jijini Arusha tayari zimeshajaa na wakazi wa Arusha wametoa tahadhari kwamba uzinduzi wa jiji kesho usihusishe siasa zozote especially za ccm maana wataipinga hali hiyo kwa nguvu zote.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums

Wa kina mama wa kimasai kama kawaida yao wataletwa kutoka Monduli na wabarabeig wataletwa na Bajuta kutoka Hanang kuja kuruka uchi mbele ya rais halafu wanaambulia maji ndogo ya uhai chupa moja moja. JK amehisi watu wa hapa mjini AR wako busy sana hawawezi ku attend hadi akawatoe wazalishaj na wafugaji kwenye shughuli zao za mashambani
 
Arusha ina changamoto nyingi..lakini huwezi kuifananisha Arusha na Mbeya au Tanga..Arusha is Next level..kwanza it is the second town to contribute national income..Mwanza is better kuliko Arusha in few areas only
 
Azimio la arusha linakujaje hapo mbona tunatumia asilimia ndogo ya akili zetu? Rais anazindua jiji what is the connection with Arusha declaration ? tumia akili mtoa mada umtendee Munguarded wetu haki aliyekupa akili
 
Padri wenu juzi kaumbika igunga mkakodi coster mbili kutoka igunga ,choma na nkinga anayebisha ajitokeze chezea igunga wewe anahutubia watu bize na kazi hahahaahahaha hadi kasulumbai akasema igunga hali imekuaje mbona tunaporomoka eti wanapanga kuja ku M4D kwa mwezi watu sio wamechoka porojo
 
Kwa Arusha kutangazwa kuwa jiji na ona ni haraka tu! Mji wa Arusha una changamoto nyingi ambazo wange zishughulikia kabla ya kutangazwa kuwa jiji.
Changa moto kama!
1 barabara hili ni tatizo kubwa hata zilizopo ni nyembamba sana, kwakweli huu mji una hitaji barabara za kutosha ni haibu kusema Arusha ni jiji labda kwa mtu ambaye ajawai kuishi au kupita Arusha anaweza asishangae!
Japo miundo mbinu si kigezo pekee lakini kwa hili kuna udhaifu sana!
Kwakweli ni bora nguvu nyingi zingeelekezwa kwenye kuuboresha mji huo, sijajua hiyo haraka ni ya nini?

Ukweli lazima usemwe Arusha bado huku ni kujifariji, lakini pamoja na vitega uchumi vingi vilivyoko hasa utalii nashangaa mji wa Arusha kuwa na miundo mbinu hafifu!

Bila kusahau maji machafu yanayotiririka kutoka vyooni hasa mfereji wa kutoka Kaloleni kupitia Mnara wa Mwenge na Hospitali ya Kaloleni, mtaro unaoanzia jengo jipya la NSSF( kama sikosei) linalojengwa maeneo ya round about ya Florida na kushuka Golden Rose na Mbele ya Blue Rock, mashimo ya maji machafu katika barabara inayoanzia Arusha by Night/ upande wa juu wa uwanja wa mpira kuelekea Kanisa la Anglican, na chini ya ofisi ya Kata ya Kaloleni maeneo yote hayo kwa wastani kila siku yanavuja lakini hakuna kinachofanyika kurekebisha tatizo hili. Sina uhakika kama mtaro unaojengwa kule soko kuu kama nao hautakubwa na tatizo hili badala ya kuchukua maji ya mvua. Hayo ni maeneo machache ninayoyaona kila siku sina uhakika kule chini barabara ya uhuru kulikoni?
 
Wadau arusha inauzwa kwa jina. Najua idadi ya watu na miundombinu duni ilikuwa gigezo cha kunyimwa jiji. Sasa hivi wametenga bajeti ya miundombinu ndo wamefikiliwa
 
Anyway,kwanini kwa Arusha imekuwa so special? Mbeya,Tanga,Mwanza ilikuwa hivi? Politics?

Moja mkuu wa kaya anakwenda kuzindua chuo cha Nelson Mandela kule TENGERU KESHOKUTWA. Akaona ni muda hajasafiri. Akapanga safari, Same, Rombo,Hai, Moshi, Arusha, Nelson Mandela.

Pia anaonyeha jinsi CCM inavyofanya kazi hata kwenye vitu visivyo vya msingi.

Imemtosha.
 
nadhani ni mwendelezo uleule wa kutumia vibaya rasilimali za wa-tz, watafanya remix sn kuizndua Arusha kuwa jiji bt kamwe hawatofanikiwa, najua kesho watasomba watu km kawaida yao waje kuwatzama ze-komedy kwasbb hata kinachofanyika ni KOMEDY pia. Arusha ni mwiba mkali sn kwa serikali hili linaonekana dhahili. Poleni sn govt ya magamba kwa ufinyu wa kufikri hata kwa hili dogo.
 
mtoto aliliye maziwa ili mama amnyonyeshe ndiye anyonyeshwaye. Arusha wanatetemekewa kwanini usiniulize.... nadhani mikoa mingine na yenyewe ililie maziwa.
 
Back
Top Bottom