Hahaha umeishiwa hoja unaeta vioja!
Kaka jamani!!!
Mbona hivyoooooooo!!!
Kaleta mfano wa Babu aliyewahi kutokea.
Mi sioni kosa lake kwa kweli.
Judy endelea kunyamaza Kimya.
Binafsi nashukuru kwa hili pia.
Hahaha umeishiwa hoja unaeta vioja!
mi kwa kweli ndio maana siku hizi sijihangaishi kuchangia kitu JF. hapa siku hizi pana vimambo vya kitoto kitoto sana. sasa MJ kakosea kutufahamisha yaliyotokea huko pepmbe ya afrika?
Kaka jamani!!!
Mbona hivyoooooooo!!!
Kaleta mfano wa Babu aliyewahi kutokea.
Mi sioni kosa lake kwa kweli.
Judy endelea kunyamaza Kimya.
Binafsi nashukuru kwa hili pia.
Hivi ni waafrika peke yao ndio wanaletewa ufunuo wa kutibu kwa mizizi..?
Hivi ni waafrika peke yao ndio wanaletewa ufunuo wa kutibu kwa mizizi..?
Nashindwa kupata picha ya huyu kaka anayejiita MISS JUDITH anafananaje!Mtu Mmoja humjui huyu MJ hajaanza leo kuleta habari za babu yaani kila akiamka yeye na babu ndo maana watu washamchoka na hata mod kaihamishia hii thread huku kijiweni!!!
Wapendwa,
Kama nilivyowaahidi ndio namaliza mazungumzo na rafiki yangu kutoka Eritrea kuhusu "babu" wa huko kwao na shughuli zake. Kimsingi hatofautiani sana na babu wetu huyu wa TZ. Mambo ya "babu" wa Eritrea kwa mujibu wa huyu rafiki ni kuwa:
1.
Alijulikana kwa jina la Armalakha na alikuwa muinjilisti na mhubiri hodari katika nchi za Ethiopia na Eritrea hata kabla Eritrea haijajitenga kutoka Ethiopia.
2.
Aliwahi kuingia katika migogoro kadhaa na makanisa ya kikatoliki na orthodoxy (amabyo ndiyo makubwa na yanaheshimika sana nchini humo) ya Eritrea na Ethiopia kwa sababu makanisa hayo yalipinga utaratibu wa tiba yake kwa kuhusianisha uganga wake na mafundisho ya biblia.
3.
Mwaka 1996 alianza kudai kuwa mungu amemuotesha mchanganyiko wa madawa asilia ambayo huyachanganya na kuyachemsha na kasha maji yake kuwanywesha wagonjwa wake na makapi ya maji yake kuwafungia wagonjwa wake kwenye mkono wa kuume na kuuning'iniza mkono huo kama POP. Hiyo ni baada ya kusema mungu kamtokea katika ndoto na kumfunulia kuwa maradhi yote yanayowasumbua watu yako tumboni na hutokea mwilini kupitia mkono wa kuume.
4.
Watu wa kwanza kunywa dawa zake walikuwa wakiongea kwa lugha za ajabu na yeye akawa anadai ndizo lugha mpya zilizotabiriwa na nabii Yoeli!
5.
Alidai anatibu magonjwa makuu kama kansa, ukimwi, kisukari na kutoa mapepo ya aina zote kwa dawa zake hizo!
6.
Alidai mungu kamwagiza atibu kwa Nakfa 8/- tu (nakfa ni sarafu ya Eritrea na nakfa moja ni sawa na senti kama 30 za USD)
7.
Alipata umaarufu mkubwa sana na wa ghafla sambamba na kutajirika sana katika kipindi kifupi sana na kulikuwa na shuhuda nyingi sana kuwa watu wengi walipona maradhi yao kwa muda mfupi sana na kimiujiza japo hospitali za Ethiopia na Eritrea hazikuwahi kuthibitisha uponyaji wake hata mara moja!
8.
kutokana na uhasama ulioibika baada ya Eritrea kujitenga na Ethiopia (baada ya eritrea kujitangazia uhuru), alituhumiwa kuwa alikuwa wakala wa intelijensia ya Ethiopia (yaani alikuwa anaipatia serikali ya Ethiopia taarifa za siri za kijasusi) na kufuatia kuandamwa sana na vyombo vya dola aliuawa kwa kupigwa risasi June mwaka 2006.
Hayo ndiyo niliyopata kwa rafiki yangu huyu.
Wapendwa tusiache kuzijaribu kila roho ili tujiridhishe kuwa zimetokana na Mungu. Neno la mungu ni taa na mwangaza wa maisha yetu, liyumulikie kila tuendapo. Amina.
Nawatakia tafakari njema
Glory to God
Hatuhitaji masimulizi yako binafsi uliyoyabatiza jina la masimulizi ya rafiki yako wa eritrea.
Lakini lililo kubwa hapa ni kwamba habari kama hiyo lazima ingeripotiwa na vyombo vya habari, nadhani we mwenyewe unaelewa ni kwa kiasi gani babu wa loliondo amepata promo ya vyombo vya hyabari, si vya ndani tu bali hata vyombo vya habari vya kimataifa kama BBC, VOA, DEUSTCHWELLE, RFI na vingine.
Ingekuwa jambo la msigi sana kama ungetusaidia link ya kuonyesha hiyo habari ya miujiza ya babu wa eritrea na si masimulizi yako binafsi na rafiki yako. Haiwezekani babu wa eritrea afanye maajabu hayo yote halafu habari zake zisifike kwenye vyombo vya habari, au unataka kutuambia eritrea na ethiopia hakuna vyombo vya habari??
Tafakari Judith!!
Very Low indeed! huhmazungumzo ni kitu cha kawaida kabisa katika jamii yoyote. kila litokeapo jambo linalovuta hisia za watu kama hili la babu wa kijijini samunge, ni kawaida watu kulizungumzia na hata kushare na marafiki na jamaa zao ikiwa na lengo la kufahamishana, kutahadharishana au kuelimishana.
mi nimedokeza nilichozungumza na rafiki yangu jana, so usiniachie mwenyewe kazi ya kutafakari, tutafakari kwa pamoja mpendwa
stay blessed
Glory to God