'Kuta kwelikweli, ulinzi wa CDF, lakini Tanzanite inatoroshwa kama mwanzo', hii imekaaje jamani?

Mwanamayu

JF-Expert Member
May 7, 2010
10,450
2,000
Sasa Mhe. Rais Samia Hassan Suluhu anasema juhudi zimefanyika kudhibiti wizi wa Tanzanite pale Mererani. Juhudi hizo ni pamoja na ujenzi wa ukuta wa umbali kama km 25 hivi, na kuweka ulinzi wa JWTZ. Lakini bado Tanzanite inaondoka kama mwanzo. Neno hilo limemfanya mpaka CDF 'ametikisika kwenye kiti.' Yale tuliyoyaona na kupiga picha na Rais ni yaliyokamatwa!

Maswali: 1. hao waliotoa taarifa ya madini kutoroshwa, mbona awakutoa hiyo taarifa wakati wa hayati Dr. JPM? 2. Je, CDF ana kesi ya kujibu? 3. Hivi hapa Mhe. Rais anaongea kama vile ni kurusha jiwe gizani?

 

vvm

JF-Expert Member
Jul 18, 2014
3,959
2,000
CDF Alisema kuna jambo atamwambia mama kwa private. Maana naye katutonya hilo ndugu zangu tuikua tunapigwa. Kumaliza rushwa na ufisadi Africa ni mpaka Mungu mwenyewe atuondelee hii laana aliyotuachia.
 

Terrible Teen

JF-Expert Member
May 1, 2017
734
1,000
Ninachojua mimi na ripoti zilizopo India sio mzalishaji namba moja tena wa tanzanite duniani na uzalishaji wa tanzanite Kenya umeshuka kwa kiwango kikubwa sana.
Unachojua ni utopolo, watu waliwahi kuiba stuli ya kuwekea mwenge usiku. JPM alitumia maguvu kuliko akili takati wa kudhibiti utoroshwaji wa tanzanite. Sasa hivi ndo inaibiwa na kuuzwa kwenye soko jeusi kuliko kawaida.
 

sweettablet

JF-Expert Member
Nov 16, 2014
6,550
2,000
Unachojua ni utopolo, watu waliwahi kuiba stuli ya kuwekea mwenge usiku. JPM alitumia maguvu kuliko akili takati wa kudhibiti utoroshwaji wa tanzanite. Sasa hivi ndo inaibiwa na kuuzwa kwenye soko jeusi kuliko kawaida.
Mkuu huwa unajishughulika hata kidogo kusoma taarifa na ripoti mbalimbali? Ebu pitia basi na zinazohusu tanzanite uwe na knowledge kidogo ya kitu unachojadili.
 

Graph Theory

JF-Expert Member
Jul 2, 2011
4,837
2,000
Kwani hao wajeda watakuwepo kila mahali na kila wakati? Huo ukuta una - cover eneo gani la mraba? Kama ni dogo sana hilo eneo, hapo sawa. Ulinzi wa maliasili unaanzia katika kitu wazungu wanaita mindset, na siyo kwenye kujenga kuta.
Nilipata sema hivi wakati wanajenga huo ukuta.
 

Pslmp

JF-Expert Member
Mar 18, 2021
528
1,000
Taifa na rasilimali zake hulindwa na wananchi, Serikali haiwezi kulinda kila kitu na kila pahala

Shida sio serikali, shida ni wananchi, Kwa sababu kama Kweli tunataka tutoke tulipo, ni Sisi kubadirika na kuwachukia wezi wa Mali zetu, tukishirikiana na Serikali, hatutaibiwa tena
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom