Kusuluhisha ugomvi wa wanandoa..heri ukimbize upepo utaimarisha afya yako!

Himidini

JF-Expert Member
May 8, 2013
5,540
1,225
^^
Kama kuna taasisi ina waigizaji wazuri basi ndoa ni mojawapo! Kuna wakati wananuniana tu, wanatazamana kama watani wa jadi, na kuwashana vibao vya hapa na pale ilimradi tu maigizo ya maisha ya ndoa yalete maana!
..
Wakati fulani niliwahi kuugua ndani kwangu! Sikuwa na msaada, siku mbili sikuinuka ndani jambo lililo wafanya majirani wadadisi kulikoni. Mmoja wapo ni mwanamke mwenye mtoto mmoja na mume wake, ndiye alijua wa kwanza. Na kama tujuavyo linapokuja suala la kuhudumia wagonjwa, wanawake wanajua wafanye nini. Nilihudumiwa vizuri tu kama rafiki jirani. Na nikapona.
..
Siku zote hisani bora hulipwa kwa matendo bora na si maneno bora! Siku, miezi ikapita. Na usiku mmoja mnamo muda wa saa 7 nikagutuka usingizini niliposikia vipigo,vilio na kelele za kuomba msaada! Nikatoka nje na kuisikia sauti ya mwanamke jirani yangu, msamaria wangu, na mtu mwema kwangu aliyehitaji usaidizi toka mikononi mwa mumewe ambaye fani ya ubondia ilimwonea kutomchagua
...
Dhamira ilinisukuma na kunipa nguvu kuwa nahitaji kusaidia. Pamoja na kuwa majirani walikuwa nje bado walikuwa wakisita sita kusaidia! Naam nilijitosa na kusukuma mlango kwa nguvu na kumkuta Mwanaume ameshika panga anataka litue juu ya shingo la mkewe!! Nilimuwahi na kumtoa nje jirani yangu huyo mwanamke, nikimsukuma mumewe arudi ndani. Nilifunga mlango kwa nje nikimfungia mumewe ndani ili asilete madhara zaidi.
...
Mwanamke huyo, kwa kushirikiana na jirani zangu tulimweka kwa mama mwingne ambae hakuwa na mume, akachemshiwa maji, akakandwa na kulala hapo. Asubuhi niliamkia kazini. Jioni niliporudi bado makovu, mwili kuvimba na maumivu vilionekana wazi. Mumewe hakuwepo. Siku ya pili yake, sikwenda kazini nilikuwa mapumziko. Hapo ndipo nilishangaa
..
Kilichonishangaza ni kuwa baada ya wanandoa hawa kurudiana wao wenyewe! Tulimwagiwa mvua ya maneno na vijembe
'wapendanao kuwatenganisha ni vigumu'..
"ha haa mnaingilia yanawahusu! Mnajua tulikutanaje?"
Taarabu na mipasho iliunguruma "wape wapee vidonge vyaoo wakimeza wakitema ni shauri yao!"
Ni mengi
..
SIO SIRI NILIJIFUNZA
1. WANANDOA HUANGUKA MARA 7 MARA YA NANE WANASIMAMA KAMA HUJAJUA NI MARA YA NGAPI FANYA KAZI ZAKO
2
UGOMVI WA WANANDOA NDIO UPYA WA UPENDO
3
HAKUNA KIKAUKACHO MAPEMA KAMA CHOZI LA WAPENDANAO
4
KAMA WANAJUA KUFANANA KWAO BASI HATA TOFAUTI ZAO WANAJUA
...
Ukiona wanandoa wanapigana au umeitwa kusuluhisha kesi au kushauri juu ya ndoa! Basi usipoweza kupita kimya kama mwanafalsafa, we kimbiza upepo unaweza kuimarisha afya yako
^^
 
Mr Rocky

JF-Expert Member
Oct 10, 2007
15,188
2,000
Katika vitu ninavyoviogopa mkuu Himidini ni kuongeza au kuongea neno kwenye ugomvi wa wapendanao. Waache wenyewe waongee yao na wewe kaa kimya usiongeze au kupunguza neno wala usijifanye wewe ni msuluhishi mzuri ukajifanya kuweka sheria zako na kanuni zako na sijui utaalam wako kwenye mambo yao. Kaa mbali na hao watu siku wakipatana wewe utaonekana mbaya
Kuna kesi moja iliwahi kuendeshwa mahakamani mke na mume wanadaiana talaka. Walishatengana kila mtu kwake. Walikuwa wakikutana pale mahakamani kabla ya kesi kuanza wanatukanana na mpaka kufikia kutaka kupigana. Kesi ikaendeshwa vizuri tuu mpaka siku wakaambiwa sasa hukumu ni kesho so mje msikilize hukumu yenu mahakama itoe mustakabali wa kesi yenu kama inastahili talaka au la. Kesho yake walifika mahakamani wameshikana mikono wanacheka na kukumbatiana na wanaomba chonde chonde hukumu isisome washapatana na hawataki tena kupeana talaka wala hawataki kusikia hakimu anasema nini kuhusu ndoa yao.
Ugomvi wa wanandoa uache kama ulivyo na usiuingilie kabisa
 
Last edited by a moderator:

Himidini

JF-Expert Member
May 8, 2013
5,540
1,225
Mh ila mngewaacha napo msingefanya vyema.Kuna mambo yakuingilia na mambo yakutoingilia ila hilo mlikuwa sahihi kusaidia haijalishi mlilipwa nini?

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums

^^
Ni kweli, lakini kwa nini sehemu kubwa ya wanaosuluhishwa hugeuka tofauti?
Ablessed njoo usaidie hapa
^^
 
Last edited by a moderator:

Himidini

JF-Expert Member
May 8, 2013
5,540
1,225
Katika vitu ninavyoviogopa mkuu Himidini ni kuongeza au kuongea neno kwenye ugomvi wa wapendanao. Waache wenyewe waongee yao na wewe kaa kimya usiongeze au kupunguza neno wala usijifanye wewe ni msuluhishi mzuri ukajifanya kuweka sheria zako na kanuni zako na sijui utaalam wako kwenye mambo yao. Kaa mbali na hao watu siku wakipatana wewe utaonekana mbaya
Kuna kesi moja iliwahi kuendeshwa mahakamani mke na mume wanadaiana talaka. Walishatengana kila mtu kwake. Walikuwa wakikutana pale mahakamani kabla ya kesi kuanza wanatukanana na mpaka kufikia kutaka kupigana. Kesi ikaendeshwa vizuri tuu mpaka siku wakaambiwa sasa hukumu ni kesho so mje msikilize hukumu yenu mahakama itoe mustakabali wa kesi yenu kama inastahili talaka au la. Kesho yake walifika mahakamani wameshikana mikono wanacheka na kukumbatiana na wanaomba chonde chonde hukumu isisome washapatana na hawataki tena kupeana talaka wala hawataki kusikia hakimu anasema nini kuhusu ndoa yao.
Ugomvi wa wanandoa uache kama ulivyo na usiuingilie kabisa

^^
Da! Sasa hapo si kudhalilisha sheria? Aisee mi kama hakimu nashauriana na baraza la wazee mlipe disturbance allowance!!
Wapi Nivea ?
^^
 
Last edited by a moderator:

foshizzle

JF-Expert Member
Dec 4, 2013
374
0
Kwanini hukumtoa nje mwanaume ili asiendelee kumpiga mkewe badala yake ukamtoa nje mwanamke na ukamlaza unapojua?
 
CORAL

JF-Expert Member
Jun 26, 2011
2,699
2,000
Himidini, hujakosea kabisa kuingilia ugomvi huo wa wanandoa majirani zako. Usibabaishwe na hizo taarabu ma ngonjera. Fikiria kidogo: Kama mgewaacha bila kuingilia na mmoja akamuua mwenzake ungejisikiaje? Hizo taarabu na ngonjera zingeimbwa? Kimsingi hukua unaingilia ugomvi bali ulienda kuokoa uhai. Hivi kweli ni sahihi kujuta kwa sababu ya kuokoa uhai wa mtu?
Wewe na wenzako mlifanya jambo linalostahili pongezi! Kama mlichofanya hakikuwa sahihi kwa nini mke alikubali kulala kwa jirani mliyemchagulia? Kwa nini hakukataa kuondoka kwake kama hakukuwa na hatari yoyoye? Siku zote usipende kujilaumu kwa kufanya jambo jema. Hii haijalishi yule unayemfanyia atachukulia vipi huo msaada wako. Ndio maana waswahili wanasema: TENDA WEMA UENDE ZAKO USINGOJE SHUKRANI.
Kwa hiyo, wanandoa wanapogombana zingatia yafuatayo:
  • kama wanatukanana, kufokeana, kupigana makofi, ngumi, waache. Usiingilie ama kwa maneno au vitendo
  • kama wameshikiana silaha mfano,bastola,bunduki,jembe,panga,kisu, mti au chochote ambacho kinaweza kuleta madhara makubwa, nenda umsaidie yule aliye hatarini kwa kumdhibiti aliyeshika silaha na kuhakikisha yule mwenzake yuko mahali salama. Ukifanikiwa kunyang'anya silaha usiirudishe hadi wapatane.
  • usimhukumu yeyote hata yule aliyetaka kuua, wewe okoa tu basi hukumu watafanya wenyewe.
Kumbuka kuwa watu wanaogombana uwezo wao wa kufikiri unakuwa likizo. Lolote laweza kutokea. Wangapi wanajuta maisha yao yote kwa kuua wake/waume zao? Hasira ni kitu kibaya sana lakini ugomvi ukiisha na hasira zikapoa akili zikarudi ofisini, ndipo mwenye makosa atatambua makosa yake, labda wataombana msamaha na kupatana. Kwa kawaida wanandoa wakishapatana ndio wanaanza kumtafuta mbaya wao nani. Ndipo hapo zinapoimbwa taarabu, nginjera, mashahiri,nk.
Himidini hayo si mambo ya kufuatilia mradi unaamini ulifanya jambo sahihi.
 
Himidini

JF-Expert Member
May 8, 2013
5,540
1,225
Kwanini hukumtoa nje mwanaume ili asiendelee kumpiga mkewe badala yake ukamtoa nje mwanamke na ukamlaza unapojua?

^^
Inawezekana ni kosa la uchaguzi lakini ni nguvu ya kulipa fadhila, ambayo ushahidi wa macho na mazingira ungenisaidia. Nakiri kwa misingi ya ndoa nilipotoka.
^^
 
Ennie

JF-Expert Member
Jan 15, 2011
7,140
2,000
^^
Vipi Ennie ni sahihi kubeza waliokunusuru kipigo cha mumeo?
^^
Yaani mi nilivyo muoga wa kupigwa! Nikifanikiwa kuponyoka sijui kama kuna siku nitageuka nyuma.
Kutofautiana kupo na kukitokea tutasuluhisha wenyewe bila mtu wa tatu.
Binafsi sipendi kuhusisha ndugu,jamaa wala marafiki kwenye migogoro ya mapenzi na huwa naamini tukishindwa kusuluhisha wawili tuliopendana hakuna atakayetoka nje aweze.
 
Himidini

JF-Expert Member
May 8, 2013
5,540
1,225
Himidini, hujakosea kabisa kuingilia ugomvi huo wa wanandoa majirani zako. Usibabaishwe na hizo taarabu ma ngonjera. Fikiria kidogo: Kama mgewaacha bila kuingilia na mmoja akamuua mwenzake ungejisikiaje? Hizo taarabu na ngonjera zingeimbwa? Kimsingi hukua unaingilia ugomvi bali ukienda kuokoa uhai. Hivi kweli ni sahihi kujuta kwa sababu ya kuokoa uhai wa mtu?
Wewe na wenzako mlifanya jambo linalostahili pongezi! Kama mlichofanya hakikuwa sahihi kwa nini mke alikubali kulala kwa jirani mliyemchagulia? Kwa nini hakukataa kuondoka kwake kama hakukuwa na hatari yoyoye? Siku zote usipende kujilaumu kwa kufanya jambo jema. Hii haijalishi yule unayemfanyia atachukulia vipi huo msaada wako. Ndio maana waswahili wanasema: TENDA WEMA UENDE ZAKO USINGOJE SHUKRANI.
Kwa hiyo, wanandoa wanapogombana zingatia yafuatayo:
  • kama wanatukanana, kufokeana, kupigana makofi, ngumi, waache. Usiingilie ama kwa maneno au vitendo
  • kama wameshikiana silaha mfano,bastola,bunduki,jembe,panga,kisu, mti au chochote ambacho kinaweza kuleta madhara makubwa, nenda unsaidie yule aliya hatarini kwa kumdhibiti aliyeshika silaha na kuhakikisha yule mwenzake yuko mahali salama. Ukifanikiwa kunyang'anya silaha usiirudishe hadi wapatane.
  • usimhukumu yeyote hata yule aliyetaka kuua, wewe okoa tu basi hukumu watafanya wenyewe.
Kumbuka kuwa watu wanaogombana uwezo wao wa kufikiri unakuwa likizo. Lolote laweza kutokea. Wangapi wanajuta maisha yao yote kwa kuua wake/waume zao? Hasira bi kitu kibaya sana lakini ugomvi ukiisha na hasira zikapoa akili zikarudi ofisini, ndipo mwenye makosa atatambua makosa yake, labda wataombana msamaha na kupatana. Kwa kawaida wanandoa wakishapatana ndio wanaanza kumtafuta mbaya wao nani. Ndipo hapo zinapoimbwa taarabu, nginjera, mashahiri,nk.
Himidini hayo si mambo ya kufiatilia mradi unaamini ulifanya jambo sahihi.

^^
Umenena vema CORAL japo umenipa kazi mpya ya kufikiri, Is experience a bad teacher?
Wanandoa wa aina hii wanakatisha sana tamaa, wema unapogeuka ubaya inatesa akili.
^^
 
Last edited by a moderator:

Himidini

JF-Expert Member
May 8, 2013
5,540
1,225
Yaani mi nilivyo muoga wa kupigwa! Nikifanikiwa kuponyoka sijui kama kuna siku nitageuka nyuma.
Kutofautiana kupo na kukitokea tutasuluhisha wenyewe bila mtu wa tatu.
Binafsi sipendi kuhusisha ndugu,jamaa wala marafiki kwenye migogoro ya mapenzi na huwa naamini tukishindwa kusuluhisha wawili tuliopendana hakuna atakayetoka nje aweze.

^^
Kweli Ennie ni busara wanandoa wenyewe wakasuluhishana tofauti zao, vipi ktk hatari ya panga au bastola kama alivosema CORAL uachwe tu?
^^
 
Last edited by a moderator:

Ennie

JF-Expert Member
Jan 15, 2011
7,140
2,000
^^
Kweli Ennie ni busara wanandoa wenyewe wakasuluhishana tofauti zao, vipi ktk hatari ya panga au bastola kama alivosema CORAL uachwe tu?
^^
Hiyo ni next level na ni busara mlio jirani mkaingilia kuokoa maisha ila yatakayofata baada ya ugomvi huo yasiwashangaze.
 
DEMBA

JF-Expert Member
May 10, 2012
8,244
2,000
huyo mwanamke hana akili kabisa. hata kama wamepatana hakupaswa kuwakejeli waliomsaidia, siku nyingine mwacheni afie huko ndani.
^^
Vipi Ennie ni sahihi kubeza waliokunusuru kipigo cha mumeo?
^^
 
Last edited by a moderator:

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom