Himidini
JF-Expert Member
- May 8, 2013
- 5,534
- 4,185
^^
Kama kuna taasisi ina waigizaji wazuri basi ndoa ni mojawapo! Kuna wakati wananuniana tu, wanatazamana kama watani wa jadi, na kuwashana vibao vya hapa na pale ilimradi tu maigizo ya maisha ya ndoa yalete maana!
..
Wakati fulani niliwahi kuugua ndani kwangu! Sikuwa na msaada, siku mbili sikuinuka ndani jambo lililo wafanya majirani wadadisi kulikoni. Mmoja wapo ni mwanamke mwenye mtoto mmoja na mume wake, ndiye alijua wa kwanza. Na kama tujuavyo linapokuja suala la kuhudumia wagonjwa, wanawake wanajua wafanye nini. Nilihudumiwa vizuri tu kama rafiki jirani. Na nikapona.
..
Siku zote hisani bora hulipwa kwa matendo bora na si maneno bora! Siku, miezi ikapita. Na usiku mmoja mnamo muda wa saa 7 nikagutuka usingizini niliposikia vipigo,vilio na kelele za kuomba msaada! Nikatoka nje na kuisikia sauti ya mwanamke jirani yangu, msamaria wangu, na mtu mwema kwangu aliyehitaji usaidizi toka mikononi mwa mumewe ambaye fani ya ubondia ilimwonea kutomchagua
...
Dhamira ilinisukuma na kunipa nguvu kuwa nahitaji kusaidia. Pamoja na kuwa majirani walikuwa nje bado walikuwa wakisita sita kusaidia! Naam nilijitosa na kusukuma mlango kwa nguvu na kumkuta Mwanaume ameshika panga anataka litue juu ya shingo la mkewe!! Nilimuwahi na kumtoa nje jirani yangu huyo mwanamke, nikimsukuma mumewe arudi ndani. Nilifunga mlango kwa nje nikimfungia mumewe ndani ili asilete madhara zaidi.
...
Mwanamke huyo, kwa kushirikiana na jirani zangu tulimweka kwa mama mwingne ambae hakuwa na mume, akachemshiwa maji, akakandwa na kulala hapo. Asubuhi niliamkia kazini. Jioni niliporudi bado makovu, mwili kuvimba na maumivu vilionekana wazi. Mumewe hakuwepo. Siku ya pili yake, sikwenda kazini nilikuwa mapumziko. Hapo ndipo nilishangaa
..
Kilichonishangaza ni kuwa baada ya wanandoa hawa kurudiana wao wenyewe! Tulimwagiwa mvua ya maneno na vijembe
'wapendanao kuwatenganisha ni vigumu'..
"ha haa mnaingilia yanawahusu! Mnajua tulikutanaje?"
Taarabu na mipasho iliunguruma "wape wapee vidonge vyaoo wakimeza wakitema ni shauri yao!"
Ni mengi
..
SIO SIRI NILIJIFUNZA
1. WANANDOA HUANGUKA MARA 7 MARA YA NANE WANASIMAMA KAMA HUJAJUA NI MARA YA NGAPI FANYA KAZI ZAKO
2
UGOMVI WA WANANDOA NDIO UPYA WA UPENDO
3
HAKUNA KIKAUKACHO MAPEMA KAMA CHOZI LA WAPENDANAO
4
KAMA WANAJUA KUFANANA KWAO BASI HATA TOFAUTI ZAO WANAJUA
...
Ukiona wanandoa wanapigana au umeitwa kusuluhisha kesi au kushauri juu ya ndoa! Basi usipoweza kupita kimya kama mwanafalsafa, we kimbiza upepo unaweza kuimarisha afya yako