Kusomea udaktari wa mifugo inalipa sana?

dottoz

JF-Expert Member
Jan 29, 2012
1,510
868
Jamani nisaidieni kwa hili ambalo linanitatiza kidogo. Eti wanaosomea udokta mifugo wanapata ajira za haraka na mishahara yao ni mikubwa?
 
Tusubiri wadau watakusaidia.

Ushauri: Kama mapenzi yako kwenye fani fulani yame-base katika ujira na ajira, mbele ya safari ni giza! Usisomee fani yoyote ati kwasababu tu inalipa! Mapenzi yako ya ndani kwenye kazi fulani ndiyo tu yakupe msukumo wa kusomea kazi hiyo na si vinginevyo. Kuna watu pamoja na mishahara yao mizuri huamua kuacha kazi hizo kwasababu MIOYO yao haipendi kazi hizo.

Ukipenda kazi nayo itakupenda.
 
VM inalipa,namjua mkaka m1 hvi jiran yetu anachukua zaid ya mil 2.5 kwa mwez.
 
Kaka/dada ,kama unapenda BVM kasome tu kwa moyo mmoja mambo ya kushauriwa ati "namjua jamaa mmoja jirani" utadhani wao ndio wanamchukulia mshahara utakuja juta. Mimi naamini kila kitu kinalipa ukijipanga tu. Ngoja nikupe ushuhuda wangu maana BVM ilikuwa one of my options,kwa kifupi mwalimu wangu wa chemistry a-level alikuwa daktari wa mifugo,anaitwa dr sanga,mara ya mwisho alikuwa headmaster moshi sec sijui kama alihamishwa,jamaa ilibidi apige chaki kupunguza ukali wa maisha,na ni very smart....waulizd waliosoma tosamaganga enzi hizo,hashauri kabisa mtu asome hiyo kitu,pia nishakutana face to face na madaktari wa mifugo wasio na kazi,ni nzuri ukijiajiri ila yataka mtaji...pia shule yake ngumu si masihara,kwa hiyo changa karata zako vizuri....
 
Mfano halisi, producer HERMY B ni daktari wa mifugo,graduate wa SUA, jamaa kaamua kupiga zake vinanda,....
 
dogo achana na mawazo mgando ya kuajiriwa, mwaka huu govt imeajiri mamia ya graduates hawa na wengine wengi wamekosa ajira. Elewa kuna kitu inaitwa "future", hata kama ajira zipo je baada ya miaka mitano ambapo utagraduate unafikiri bado kutakuwa na nafasi za ajira hii??
Asikudanganye mtu sasa hivi mtu makini anaangalia kujiajiri hategemei kusoma ili aje kuajiriwa, usipokuwa na future utarudi mtaani na degree yako kuja kuuasugua @ by the time wenye fani kama yako mtakuwa maelfu mnagombania nafasi 15
 
Du!ukisoma fani hy unaingia chaka bovu ndugu yangu!nani anasema TZ unasema fani uiependandayo?achana na maneno ya nadharia hayo.Cha msingi ni kujikwamua kimaisha. Je, umeshawahi ona kazi ya bwana mifugo ikitangazwa mara ngapi gazetini?fungua macho na ona mbali ndugu yng.ushauri:kama ni SUA soma uchumi kilimo.Later utaweza chomoka ktk kilimo uwe mchumi na uvae tai!lol
 
Ajira ya udaktar mifugo huwa ni serikalini 2 na sivngnevyo.
 
Jamani nisaidieni kwa hli ambalo linanitatza kdogo,eti wanaosomea udokta mifugo wanapata ajira za haraka na mishahara yao ni mikubwa?

Mkuu,

Inategemea na mambo mawili;

Kwanza, ni kama unapata ajira serikalini ambapo kuna miradi kadhaa inayohusiana na mifugo na mishahara na marupurupu na mafunzo zaidi inakuwa ni kitu cha kawaida.

Pili ni kama baada ya kupata shahada yako kutoka pale SUA utaweza kujiunga na private veterinary clinic au hospital (kama zipo) na kuwa associate na ukaanza ku-practice fani yako ukizingatia maeneo kadhaa kama vile:

Utunzaji wa taarifa za wanyama

Upasuaji na utoaji huduma ya dawa kwa wanyama

Na mambo mengine mengi tu na ukiwa unaipenda kazi yako na ukaonekana basi unaweza ukapelekwa ughaibuni kujifunza zaidi na kufahamu kutumia vifaa vya kisasa zaidi.

Unafahamu kwa vile bado tupo nyuma sana na zahanati za kujitegemea bado ni chache mno ndio maana inabidi ubanane na zile shughuli za serikalini.
 
Hata mm nmechaguliwa BVM Lakini wazazi wangu wanadai haina soko la ajira na pia ni ngumu sana hapo SUA nifanye nini jamani
 
Back
Top Bottom