Kusiwe na Sare za Vyama vya Siasa

Goodrich

JF-Expert Member
Jan 29, 2012
2,091
1,177
Moja kati ya mapendekezo niliyoyasikia na kuyakubali sana katika hili suala la katiba mpya ni kufutwa kwa sare na bendera za vyama.
Itumike alama au bendera ya taifa tu !
Mambo ya sare ndio yamekuwa kichocheo cha vurugu na migawanyiko katika jamii yetu!
Nchi nyingi hazina sare wala bendera za vyama
, wanatumia alama za kitaifa.

Tuwe hivi:

1500_bk-obama-20121023.jpg

2012-08-01t170304z_624217185_gm1e88202mg01_rtrmadp_3_usa-campaign-obama.grid-6x2.jpg

Tusiwe hivi

images.jpeg
 
Attachments

  • 8E9U1900.jpg
    8E9U1900.jpg
    78.2 KB · Views: 214
Moja kati ya mapendekezo niliyoyasikia na kuyakubali sana katika hili suala la katiba mpya ni kufutwa kwa sare na bendera za vyama.
Itumike alama au bendera ya taifa tu !
Mambo ya sare ndio yamekuwa kichocheo cha vurugu na migawanyiko katika jamii yetu!
Nchi nyingi hazina sare wala bendera za vyama, wanatumia alama za kitaifa.

mkuu hebu tupe mfano,
 
Itabidi hata timu maarufu za mpira nazo zisiwe na bendera/sare zenye rangi wanazozipenda!
 
Umeongea point kubwa sana, sikuwahi kuifikiria na hii ndio kama unavosemw itafuta kuangaliana na kuchunguzana
 
Angalau hii itapunguza kukereka kila nikiona Magamba yao ya Njano sijui kijani!!!!
 
Utaratibu wa sare za vyama kimsingi unagawa watu katika taifa kutojiona kitaifa bali makundi ndani ya taifa. Binafsi nimefurahishwa sana na maoni hayo na pia nilikuwa mbioni kuanzisha mada inayohusu jambo hilo.

Nilipokuwa nchini Marekani nilifanikiwa kuona kampeni vipindi viwili vya uchaguzi, katika vipindi vyote sijawahi kuona:
  • watu kwenye kampeni wakivaa sare za vyama vya siasa.
  • Bendera za vyama vya siasa
  • Utitiri wa ofisi za vyama vya siasa
  • Mikutano ya vyama vya kisiasa
  • Kuhamasisha watu kujiunga vyama vya kisiasa.

Nilichojifunza ni kwamba kuna itikadi mbili kubwa nchini Marekani ambazo zinabebwa na vyama husika ambavyo ni:
  • Republican - Hutetea mfumo wa kikapitalist/matajiri
  • Democratic - Wa kipato cha kati na cha chini ambao wengi wao ni wafanyakazi serikalini na wa matajiri.

Binafsi kwa mtazamo wangu, mambo ya sare, bendera za vyama vya siasa:
  1. Hutugawa wananchi katika makundi
  2. Huhamasisha uhasama baina ya vyama vya siasa
  3. Hautuunganishi kitaifa
  4. Unahamasisha watu kuchagua rangi badala ya mtu anayefaa.
  5. Huchochea rushwa katika kampeni
  6. Huhamasisha viongozi serikalini na wafuasi wao kuvaa sare wakati shughuli ni za kitaifa.

Bora mambo ya sare za vyama bora kuyaondoa zaidi hapo tutajenga taifa moja lenye umoja kwa wananchi wake, kitakachoshindaniwa na vyama si sare bali Itikadi. Bendera wenzetu wanazo lakini ni pale kwenye ofisi ya chama na ofisi zao zipo kikanda zaidi badala ya kuzagaa kila kona na vijiweni kama Tanzania. Nilibahatika kupitia State zaidi ya 15 Marekani lakini sijakutana na bendera ye yote ya chama cha siasa. Mara chache nilipobahatika kuona ofisi za wilaya na state za kichama ndipo nilipoona bendera ya chama.

Mikutano ya kampeni wananchi wote hubeba bendera ya taifa, na wagombea huwa na taswira za kitaifa si kichama, hata siku moja hutakuta mgombea kuvaa nguo za chama. Hata kwenye mikutano mikuu ya kichama ya kumpitisha mgombea hakuna alama ya kichama ila bendera ya taifa na sare yao ni itikadi zao zinazotofautiana na sare ya wapinzania ambao ndio itikadi zao pia.

Katika uchaguzi tunachagua mtu anayefaa mwenye sera nzuri, hatutakiwi kuchagua chama, hawa wanasiasa wanatupotosha sana. Mbaya zaidi bendera zenyewe za vyama vya siasa haziakisi na rangi ya bendera ya Taifa, jambo ambalo nalishangaa. Angalia alama za Vyama vya siasa Marekani.
images
images

images
images

Unaona Sign zao zinaakisi utaifa, tofauti na mambo ya vyama vyetu Tanzania utafikiri ni vita baina ya nchi na nchi hadi kuchukuliana majambia.

images
9k=
images
images

Barack Obama Campaign rally/United States of America

images
images
images

Mitt Romney Campaign rally/United States of America

Nakala kwa:
Mabreka, TANMO, Indian, , Goodrich, Mabreka
 
Itabidi hata timu maarufu za mpira nazo zisiwe na bendera/sare zenye rangi wanazozipenda!

Utawala wa nchi huwezi kulinganisha na ushabiki wa michezo ya burudani, kuongoza nchi si burudani bali ni uwajibikaji kwa taifa.
 
Hii ni bonge la wazo. Tujenge Tanzania sio vyama. kwa wenzetu Taifa kwanza vyama baadae. Tanzania ni chama kwanza Taifa baadae. wasi wasi wangu sijui kama CCM watakubali kwani kwao huu ndio mtaji.
 
Nahisi itabidi Mode aanzishe jukwaa la "TANZANIA TUITAKAYO". Haya ndio mambo muhimu ya kujadili hapa jamvini sio kutumika tu kisiasa. Si kwamba watanzania wote ni wanasiasa
 
Naitafakari Tanzania yenye Utaifa, naona inawezekana kabisa. Candid Scope ametoa ufafanuzi mzuri sana katika hili refering to USA.
 
WANA JANVI MI NI MEMBER MGENI SANA KWENYE JANVI HILI KW HIYO NAOMBA MSAADA WENU WA MAMBO YAFUATAYO: 1. NAOMBA NIIONE BENDERA YA CHAMA CHA DEMOCRATIC CHA PRESIDAA OBAMA WA KOGELO
2. UNIFORM ZA CHAMA CHA DEMOCRATIC
3. PICHA AMBAYO INAMUONYESHA OBAMA AKIWA KWENYE KAMPENI AKIWA AMEVAA UNIFORM YA CHAMA CHAKE 4.PICHA YA MWL NYERERE AKIWA AMEVAA GAMBA LA KIJANI THANX, am stand to be corrected
 
Wakuu mnaongea vitu msivyovijua kabisa, kwa mfano
1/Huko marekani nk kutokuwa na bendera ni sheria au utamaduni?

2/Huku Tanzania sheria za matumizi ya alama za taifa kama bendera inasemaje?

3/Bendera tu ndio zinaweza kuwagawa watanzania?
What about uwepo wa vyama vingi, chaguzi za kisiasa, mahubiri ya dini, Mila za Makabila, kampeni za kisiasa, slogan, sera, itikadi, Ushabiki wa michezo(Simba na Yanga nk), Uhuru wa vyombo vya habari(Radio Iman, TBC, nk) na mitandao ya kijamii(JF nk), Taasisi za kijumuiya(Jumuiya ya waarabu, wahaya, wachaga, Uamsho, Bakwata, CCT nk)
 
Haya CCM kijani, hamas kijani, Ghadaffi kijani, etc.i Madikteta na Magaidi trademark rangi yao ni kijani?
attachment.php

CCM

hamas1.jpg

Hamas

mass_demo_for_qadaffi_july_72.jpg

Wafuasi wa Ghadaffi
 
WANA JANVI MI NI MEMBER MGENI SANA KWENYE JANVI HILI KW HIYO NAOMBA MSAADA WENU WA MAMBO YAFUATAYO: 1. NAOMBA NIIONE BENDERA YA CHAMA CHA DEMOCRATIC CHA PRESIDAA OBAMA WA KOGELO
2. UNIFORM ZA CHAMA CHA DEMOCRATIC
3. PICHA AMBAYO INAMUONYESHA OBAMA AKIWA KWENYE KAMPENI AKIWA AMEVAA UNIFORM YA CHAMA CHAKE 4.PICHA YA MWL NYERERE AKIWA AMEVAA GAMBA LA KIJANI THANX, am stand to be corrected

Hili ndilo jibu lake unalotaka?
Angalia alama za Vyama vya siasa Marekani.
images
images

images
images

Unaona Sign zao zinaakisi utaifa, tofauti na mambo ya vyama vyetu Tanzania utafikiri ni vita baina ya nchi na nchi hadi kuchukuliana majambia.

images
9k=
images
images

Barack Obama Campaign rally/United States of America

images
images
images

Mitt Romney Campaign rally/United States of America

Wenzetu hufanya hivi.
 
Wakuu mnaongea vitu msivyovijua kabisa, kwa mfano
1/Huko marekani nk kutokuwa na bendera ni sheria au utamaduni?

2/Huku Tanzania sheria za matumizi ya alama za taifa kama bendera inasemaje?

3/Bendera tu ndio zinaweza kuwagawa watanzania?
What about uwepo wa vyama vingi, chaguzi za kisiasa, mahubiri ya dini, Mila za Makabila, kampeni za kisiasa, slogan, sera, itikadi, Ushabiki wa michezo(Simba na Yanga nk), Uhuru wa vyombo vya habari(Radio Iman, TBC, nk) na mitandao ya kijamii(JF nk), Taasisi za kijumuiya(Jumuiya ya waarabu, wahaya, wachaga, Uamsho, Bakwata, CCT nk)

Huwa unajisikiaje unapokuwa umevaa Gamba la kijani halafu unakutana na watu wamevaa Magwanda ya Khaki ?
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom