Kusiwe na Sare za Vyama vya Siasa

Mambo ya sare ndio yamekuwa kichocheo cha vurugu na migawanyiko katika jamii yetu!
Nchi nyingi hazina sare wala bendera za vyama, wanatumia alama za kitaifa.
 
Itapunguza matusi na kuondosha uhasama,kutishana kila mmoja atakua huru, hili sio suala la kusubiriwa katiba mpya ni msajili wa vyama kuzungumza na wanasiasa ili litolewe uwamuzi.

Pia nashangaa sana wale watoaji topic na wachangiaji mashuhuri humu jf sijawaona kuchangia topic hii muhimu kwa taifa hili linalozorota kiuchumi kila siku.nakupongeza sana GOODRICH kuleta topic kupitia kwako.
 
Kwani marekani wana sheria ya kukataza watu kuvaa sare za chama au imetokeaje wakawa hawatukuzi sare za chama au alama za chama? Uzalendo hautungiwi sheria, hata hapa nchini hatujakatazwa kutumia ishara za kitaifa au bendera ya taifa unapokuwa kwenye mikutano ya kisiasa hasa wakati wa chaguzi!
 
Ikipita hiyo kutokuvaa sare itakuwa nipigo kubwa sana kwa ccm .kwani hiyo ni sehemu yao kuu ya kutoa nguo kama rushwa kwalio wafanya maskini wa hali na akili .aita pita hii labda ccm wakiwa hawapo madarakani
 
WanaJf,

Salam za Xmas!

Zaidi ya mara tatu nimetumiwa msg hii na watu: "Je, umewahi kuiona picha ya Mwl. Nyerere akiwa ndani ya sare ya CCM? Tafuta popote duniani, ukiipata, kuna 1,000,000. Kama hakuna jiulize kwa nini?

Sijafanya uchunguzi kujua ukweli wa Mwl. kuvaaa au kutokuvaa sare ya CCM katika maisha yake. Waliyoiandaa msg hii, yamkini walifanya uchunguzi, walijiridhisha na kutoa msg hii tutafakari kwa kina. Mahusiano ya sare ya chama, uelewa wa siasa safi, na nafsi sahihi za watu ni vitu tofauti kabisa. Mengi yameongelewa namna Mwl alivyopenda kujipambanua kutokuwa mnafiki, na ndiyo maana aliwahi kusema: CCM si mama yangu!

Tunapoendelea na siasa zetu, ni wakati muafaka wa kuwaza kwa kina Uhuni wa Siasa na Sare za Vyama. Wananchi wa Tz hawahitaji sare, wanahitaji miongozo makini ya kuleta usatwi wa maisha yao. Watanzania hawahitaji sare za vyama, wanahitaji viongozi waliojipambanua kuwatumikia mpaka mwisho.

viongozi wa vyama vyetu wanajipambanua kwa yapi?

Salamu,

Perecy
Iringa
 
Nakujuza kama ni miongozo basi CCM inayo ya kutosha sana na yenye mwelekeo.

Shida ni utekelezaji wa miongozo hiyo. Huu si wakati wa kutunga sera wakati sera zilizopo zinashindwa kusimamiwa kwa maslahi ya wananchi.

Mwl alikuwa ni mtekelezaji na mtu wa popoyo au ubabaishaji.
 
Ilishajibiwa hilo kwamba ccm waliingia lini kwenye sare kama ilivyo kwa chadema ukitafuta ni wapi muasisi wao mzee mtei kavaa sare ya gwanda utapata,uzuri ni kwamba yupo hai kuna siku watanunua na kumvalisha,hizo ndizo mwelekeo wa hizi sare
 
Ilishajibiwa hilo kwamba ccm waliingia lini kwenye sare kama ilivyo kwa chadema ukitafuta ni wapi muasisi wao mzee mtei kavaa sare ya gwanda utapata,uzuri ni kwamba yupo hai kuna siku watanunua na kumvalisha,hizo ndizo mwelekeo wa hizi sare
Hilo ndio Jibu
Kwani hawa Viongozi wa Chama wangevaa suti ingekuwa ni mtafutano (kwani idadi / aina ya suti alizonazo Mbowe au Mtei ni nyingi na washabiki wasingeelewa Chama kipo ngazi gani)
Ndio maana mwasisi wa Magwanda tunajua ni Mbowe alikuwa akivaa rangi ya Khaki na sasa anavaa rangi nyeusi. Mimi naona ameamua kujiweka katika daraja la wote yaani la chini kwa yeyote mwenye uwezo huo
Ukivaa Khaki yoyote tayari wanakudhani wewe ni mlengo gani huu ni uzamani kama ule wa kuwa Shabiki wa OSCAR KAMBONA alipokuwa akichana nywele na kuweka njia (Way) ukifanya hivyo tayari wewe ni shabiki wa Kambona na mpinzani wa Nyerere (yaani umetoa ujumbe)
 
Back
Top Bottom