Kushukuru ni uungwana na kujali pia!

Kushukuru ni uungwana na kujali pia!

Nimefurahi.
Maaana wewe no kati ya ninaowaheshimu na kuwakubali Jf
 
nadhani umeroga mahali ili upate haka kacheko(joking,) anayway be blessed. usinisahau naililia nafasi ya undundami kwako
 
Huu ni mwaka wangu wa tisa hapa Jamvini. Kwahiyo naingia kwenye wakongwe wa kati wa JamiiForums.. Kama tukiamua kuvigawa vizazi vya JamiiForums basi tunaweza kufanya hivi kwa kipimo cha miaka kumi kumi

Kizazi cha kwanza 2000-2010.....
Hapo mnamo 2006 ndio JamiiForums ilizaliwa rasmi.. Hivyo kwa mpangilio wa vizazi.... Members wote wa kwanza mpaka 2010 hawa ndio kizazi cha kwanza cha JF... Pongezi nyingi kwao....

Kizazi cha pili 2011- 2020....
Hapa ndio nilipo mimi na wengine wengi sana... Sisi ni mapokeo ya kizazi anzilishi... Kizazi cha kwanza... Kwa jina lingine kizazi endelezi... Sura mpya nyingi na maboresho pamoja na mabadiliko mengi yamefanyika hapa... Pongezi kwa wote... Baada ya 2020 kitakuja kizazi cha tatu na cha nne na kuendelea....

Mfumo wa JamiiForums ni tofauti na mifumo ya mitandao mingine ya kijamii.. Hapa kuna mfumo wa kutambuliwa pia michango yako ndani ya forum hii.... Yani kuna madaraja kulingana na ukongwe pia... Mimi nilifikia daraja la SENIOR EXPERT MEMBER... yaani Mwanachama mkomavu mbobezi... Madaraja mengine ni junior member, member, na senior member (naweza kurekebishwa) madaraja haya ni bure.....

Aina nyingine ya madaraja ni yale ya kulipia yani kuna viwango tofauti vya tozo ambazo hukufanya upate daraja fulani... Haya sio ya bure... Na mojawapo ya madaraja hayo ni Gold member na platinum member... Nadhani ndio daraja la juu kabisa kwenye malipo

Wiki hii kuna mwanajamii mwenzetu bwana Mazigazi kwa kipekee kabisa aliguswa na mada na michango yangu hapa na kwa moyo wake mkuu wa upendo na bila shuruti akawiwa kuniombea kwa uongozi wa JamiiForums nipate daraja la PLATINUM bure bila kulipia.... Hisia zilikuwa tofauti kwenye hili toka kwa member wengine... Lakini alisimamia alichoamini

Kwa upendo wa dhati kabisa na kutoka moyoni... Uongozi uliridhia ombi la Mazigazi na nimetunukiwa rasmi daraja la PLATINUM Member bila kulipa chochote..

Nimefarijika sana na hili na napenda kuchukua nafasi hii kutoa shukrani za dhati kwa uongozi wa JamiiForums kupitia mwanzilishi wake Bwana Maxence Melo, Mazigazi aliyechagiza na kumshawishi pamoja na wana JF wote waliounga mkono na hata kupinga pia...

Nasema asanteni sana kwa heshima hii... Sitawaangusha....
CC : Maxence Melo, Paw, Invisible, Mhariri na moderators wote pamoja na wanajamii wote kwa ujumla wao... Itifaki imezingatiwa....

Jr[emoji769]
Hongera sana mkuu kwa heshma kubwa uliyopewa jf imekuwa sehem pekee ambayo naiheshimu sana tangu nilipojiunga mwaka 2013
 
Kwa mimi hata ungekuwa president trumph member ni sawa. Maana ukisoma post zako zote. Unachagua kuwa mchawi haswaa au kumtafuta Mola haswaa.
Hongera sana brother, hongera jf team kwa ujumla
 
Ongera sana kaka pongezi nyingi sana kwako,
Binafsi unastahili kwa aina ya Mada zako na aina ya Comment za huku kwa sasa kwani kuna kitu kimepungua Jf.

Unaustahimilivu wa hali ya juu sana,pamoja na Busara na ukomavu ,unajua kujibu mtu kwa kuzingatia Muhusika ,wakati na Mada husika pia kuwachukulia wanao kukwaza

Hakuna mtu ambaye hajajifunza kitu kutoka kwako ,kwangu mm member no 1 kwa ubora ni wewe.
Kifupi unastahili Sana, Congratulation
 
Sijaambiwa lolote nadhani sitalipia chochote mpaka mwisho wangu[emoji848][emoji848][emoji848][emoji849][emoji25][emoji144][emoji144][emoji144][emoji144]JF
Na sidhani kama unatakiwa ulipe Mshana Jr wewe ni moja ya watu ambao una contents nyingi na influence kwenye hili jukwaa. Na JamiiForums bila contents si lolote it's a win win kwenu wote kifupi mnategemeana.
 
Inakuwaje Mwaka wa Tisa wakati Umejiunga 2012?
 
Kweli wewe ndiyo ulifanya nijiunge rasmi Jf ,mada zako zilikuwa zinanivutia sana ila siyo zile za ndumba[emoji3][emoji3],nilikuwa wakusoma tu napita....

Hongera sana bro Mshana.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji120][emoji120][emoji123][emoji123][emoji120]
 
Back
Top Bottom