Habari zenu wandugu,
Kuna jambo nimekuwa nikitafakari kwa muda sasa baada ya kuona mara nyingi tumekuwa wepesi wa kulalamika na kulaumu kila wakati huku neno shukrani likiwa mbali na midomo yetu. Je ni kweli hata wale waliokukosea sana kwenye maisha yako awe mume/mke ,rafiki ,kingasti,jirani,mzazi hana jema hata moja alilotenda kwenye maisha yako ambalo linahitaji shukrani.
Je ni mara ngapi tumekuwa tukishukuru kwa yale ambayo Mungu ametubariki nayo kwenye maisha yetu?
Napenda kuwashukuru marafiki wote wa MMU kwa kutengeneza na kubadili mtazamo wangu kwenye suala zima la mahusiano .
MMENITOA MBALI MUNGU AWABARIKI.
Ameen Chauro,...mie sijui nisemeje nipate kueleweka,... Signature yangu inajielezea kila kitu, 'mwenye macho haambiwi tazama,'
...zaidi ya hapo...
Umenitoa mbali Mbu kuna wakati nikitaka kufanya jambo narejea post zako najikuta nimefanya maamuzi ya busara Be Blessed my brother.
Napenda kwa heshima na taadhima kutoa shukrani za pekee kwa rafiki yangu mpendwa Chauro kwa kunifanya nijisikie furaha kila wakati nionapo post/thread zake UBARIKIWE SANA MY DEAR ME LOVE YOU............................
Habari zenu wandugu,
Kuna jambo nimekuwa nikitafakari kwa muda sasa baada ya kuona mara nyingi tumekuwa wepesi wa kulalamika na kulaumu kila wakati huku neno shukrani likiwa mbali na midomo yetu. Je ni kweli hata wale waliokukosea sana kwenye maisha yako awe mume/mke ,rafiki ,kingasti,jirani,mzazi hana jema hata moja alilotenda kwenye maisha yako ambalo linahitaji shukrani.
Je ni mara ngapi tumekuwa tukishukuru kwa yale ambayo Mungu ametubariki nayo kwenye maisha yetu?
Napenda kuwashukuru marafiki wote wa MMU kwa kutengeneza na kubadili mtazamo wangu kwenye suala zima la mahusiano .
MMENITOA MBALI MUNGU AWABARIKI.
Sasas wewe Chauro umekaa ukafikiria nini hadi kuja na hii topic??
Nimeguswa sana na napenda kukupongeza kwa kufanya tafakuri kubwa namna hii.
Binafsi nakupongeza kwa michanga yako na kwa kweli wewe ni miongoni mwa watu wanaonifanya nijitahidi kutembelea uwanja huu wa MMU. Nakosa sana raha ninaposhindwa kutembelea hili jukwaa!!
Mbarikiwe sana..... wewe mwenyewe na wadau wote wa Uwanja huu wa MMU!!!
Hivi Chauro.........
Kati ya hao unaowashukuru, na mimi babu msema ovyo ODM Asprin wa ukaguzi nimo kwenye listi?
Ntashangaa!
Enenda na amani mjukuu wangu,Acha kabisa umejaza shukrani ndani ya moyo wangu kuliko unavofikiri,
siwezi kusahau hekima na busara za babu yangu.............
Mara ngapi?........E bwana sidanganyi siwezi kumbuka....Nna zaidi ya miaka kumi na huyu mrembo.Amina Babu,lakini embu niambie mara ngapi umekumbuka kusema asante angalabu kwa mama Matesha. .