Kushuka kwa shilingi ya Tanzania

Kushuka kwa shilingi ya Tanzania

Kakubi

Member
Joined
Apr 1, 2018
Posts
18
Reaction score
14
HISTORIA YA KUPOROMOKA KWA SHILINGI YETU DHIDI YA DOLA TANGU

1966-1972) 1USD = 5 TZS,
1973-1975) 1 USD =7 TZS,
1976 - 1 USD =12 TZS
1977 - 1 USD =12 TZS
1978-82 - 1 USD = 20TZS
1983 - 1 USD = 22 TZS
1984 - 1 USD = 23TZS
1985 - 1 USD = 102 TZS
1986 - 1 USD = 205 TZS
1987 - 1 USD = 207 TZS
1988 - 1 USD = 220 TZS
1989 - 1 USD = 226 TZS 1990 - 1 USD = 265 TZS
1991 - 1 USD = 300 TZS
1992 - 1 USD = 385 TZS 1993 - 1 USD = 434 TZS
1994 - 1 USD = 465 TZS
1995 - 1 USD = 500 TZS
1996 - 1 USD = 580 TZS
1997 - 1 USD = 665 TZS
1998 - 1 USD = 720 TZS
1999 - 1 USD = 800 TZS
2000 - 1 USD = 820 TZS
2001 - 1 USD = 880 TZS
2002 - 1 USD = 900 TZS
2003 - 1 USD = 900 TZS
2004 - 1 USD = 910 TZS
2005 - 1 USD = 1050 TZS
2006 - 1 USD = 1100 TZS
2007 - 1 USD = 1150 TZS
2008 - 1 USD = 1200 TZS
2009 - 1 USD = 1250 TZS
2010 - 1 USD = 1260 TZS
2011 - 1 USD = 1300 TZS
2012 - 1 USD =1450 TZS
2013 - 1 USD =1620 TZS
2014 - 1USD = 1650 TZS
2015 - 1USD = 2210TZS
2016 - 1 USD = 2200TZS
2019 - 1 USD = 2300TZS

Wakati tunaadhimisha Kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa ni juhudi zipi zifanyike ili kuirudisha shilingi yetu kama ilivyokuwa 1966-1972?
 
Serekali yetu ikae na wanauchumi wa zambia waone jinsi ya kufanya ikiwa ni pamoja na kubadili fedha zetu haya yote yaende kwa mpigo,ili hata wale walioficha magunia ya hela washindwe na walegee.
 
Hapo ni kujitahidi kupunguza uwiano mkubwa uliopo katika urari wa kibiashara kati ya nchi yetu na mataifa ya kigeni. Tujitahidi kupeleka bidhaa na huduma zaidi nje ya nchi kuliko kuingiza tu kwa wingi ili tupate ukwasi mkubwa wa fedha za kigeni na hii itapelekea shilingi yetu kuwa himilivu na yenye nguvu katika soko.

Halafu hizi kununua kwa cash hasa bidhaa au huduma zenye gharama kubwa napo kuangaliwe maana kunahusiana na kuivunja vunja fedha yetu ya ndani ili tupate sarafu ya nje kwa ajili ya kulipa/kununua. Sekta binafsi ipewe nguvu zaidi hasa katika uwekezaji mkubwa na kuwepo na PPP.

Vipaumbele vyetu viwe yakinifu, viwe vinaleta Matokeo chanya na jumuishi kwa Jamii kubwa kwa ujumla. Mazingira rafiki ya uwekezaji, sekta ya kilimo ibadilishwe kutoka kilimo cha mazoea na kujikimu kiwe kilimo cha kibiashara. Hii itachochea kasi kubwa ya Viwanda na ukuaji wa uchumi.
 
Nitakuja kujibu baadae ngoja kwanza nimfuatilie huyu msanii menina video zake chafuu
 
Tuna ndege 11 tume nunua cash na vituo 300 vya afya.


Nakupendaga na majibu yako...oh sorry i meant napendaga majibu yako 😂
Halafu ujue kuna kundi fulani hapa bongo wanaweza wakatumia hiyo sentensi kujibu zaidi ya hoja 100
 
Watakuambia mbona China na Japan ni nchi zenye uchumi mkubwa duniani, lakini fedha zao hazina thamani kihivyo mbele ya dola ya Marekani!

Kwa hiyo hilo siyo tatizo. Na hivyo tuendelee tu kufyatua watoto maana serikali inatoa zaidi ya bil.20 kila mwezi kugharamia elimu bure kuanzia shule za msingi mpaka sekondari.
 
Tuna ndege 11 tume nunua cash na vituo 300 vya afya.
Hapa kazi tu
Elimu bure, hospitali kila kijiji, mabalabala nchi nzima, ma fraiova, kuna ristandadigeji linajengwa, stigrajoji na yenyewe ishaanza kujengwa, mashure kira siku yanajengwa, pesa ya serikali haichezewi hovyo na wapiga diri kama zamani.
maendeleo hayana chama
 
HAPO KINA POLE POLE NA MAKONDO HAWAWEZI TIA NENO. JANGA LILIANZA RASMI 2015 NANDO MAANA JIWE ALIDAI BEI YA SUKARI ALIKUTA IPO JUU SANA,YEYE KAISHUSHA..
Ukitegemea ushauri wa mpango lazima ufeli.
 
Hapa kazi tu
Elimu bure, hospitali kila kijiji, mabalabala nchi nzima, ma fraiova, kuna ristandadigeji linajengwa, stigrajoji na yenyewe ishaanza kujengwa, mashure kira siku yanajengwa, pesa ya serikali haichezewi hovyo na wapiga diri kama zamani.
maendeleo hayana chama
Na korosho bado zimejaa kwenye maghala, hatutaki ujinga sisi
 
Afadhali wakati wa utawala ya Awamu ya tano shillingi imeimarika (stable) kuliko tawala zilizopita. Sasa hivi shillingi yetu inabadilishwa kwa 2300 kwa muda mrefu kama miezi saba kinyume na zamani.
 
Na korosho bado zimejaa kwenye maghala, hatutaki ujinga sisi
Kwenye kolosho hao wanaitwa sijui makambaga walikua wanawazulumu wakulima hakika serikali yetu sikivu inayowajali wananchi wake imekomesha unyonyaji kwa wakulima wetu.
 
Kwenye kolosho hao wanaitwa sijui makambaga walikua wanawazulumu wakulima hakika serikali yetu sikivu inayowajali wananchi wake imekomesha unyonyaji kwa wakulima wetu.
Tumeshindwa kupeleka watoto shule kangombacalikuwa mwokozi wetu
 
Back
Top Bottom