Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 34,059
- 79,414
Mpo salama!
Tunajua kabisa Iran inaonewa na kudhulumiwa lakini ndivyo mambo ya falme na tawala za dunia zilivyo. mdogo kumtii Mkubwa. Na kama mdogo akikaidi basi njia zozote hata zisizo halali hutumika.
Mwanadamu ni Mnyama aliyechangamka. Mifumo yake ya utawala haiko mbali na wanyama wa mwituni. Hiya ni nature.
Ingawaje kuna danganya toto kuwa haki za binadamu lakini ukifuatilia haki za binadamu ndizo haki hizohizo za wanyama wengine. Yakwamba Survival of fittest, na Mkubwa amle mdogo.
Matamanio yetu ni Dunia iwe ya Haki ya Usawa lakini hiyo ni ndoto za mchana. Kwa sababu dunia hii, nature haina haki sawa hasa kwenye Mkubwa na mdogo.
Wakubwa wa dunia hutumia propaganda ya haki za binadamu na usawa kama kiini macho kufikia maslahi yao ya kiutawala na kiuchumi.
Lakini kimsingi hakuna haki sawa kwenye huu ulimwengu.
Ulimwengu umedizainiwa katika ecosystems ya kutegemeana kwa namna ya kumuumiza mnyonge huku Nature ikimuabudu mwenye nguvu.
Dunia haina huruma!
Iran kushindwa Hilo wala halihitaji mjadala wala uwe na akili nyingi kuliona.
Iran ni kama Mbogo anayeshambuliwa na kundi la Simba. Tunajua atamalizwa.
Lakini nini tunajifunza katika kushindwa kwa Iran na ushindi wa Israel akisaidiana na mataifa ya Magharibi? Haya;
1. Know your position;
Popote uwapo tambua nafasi yako. Jua uwezo wako. Jua nguvu zako.
Kamwe usipambane na watu ambao wapo juu yako kinafasi, kiuwezo na kinguvu ambao unajua kabisa utashindwa.
Hapakuwa na namna yoyote ya Iran kushinda.
2. Usipambane na anayeweza kukuwekea vikwazo.
Kitendo cha wewe kuwekewa vikwazo kinaashiria moja kwa moja wewe umeshika Makali mwenzako kashika mpini.
Watu wanalalamika ooh! Iran kawekewa Vikwazo kwa zaidi ya miaka 30. Sijui kwa nini akili zao hawaziruhusu kujiuliza kwa nini Iran hamwekei vikwazo Marekani au nchi za Magharibi. Wanajua Iran hana uwezo wowote wa kumwekea vikwazo Marekani na washirika wake kwa sababu Iran ni taifa dogo, kashika Makali.
Kwa ngazi ya mtu binafsi, huwezi mwekea vikwazo Boss wako au mkubwa wako. Kwa sababu vikwazo vyako havitamuathiri pakubwa.
Alafu mwenzako anauwezo wa kutumia mabavu kukushinda.
3. Washirika wenye nguvu ni Muhimu Sana.
Watu wanalaumu Israel kuwa na ushirika na US na mataifa ya Magharibi. Huku wakisema Iran inachangiwa, na wanaitaka Israel ipambane pekeake.
Watu hao ni watu wajinga, hawajui kuwa kwenye utawala wowote ili uwe na nguvu lazima utumie mfumo wa Simba, team work.
Simba anapowinda hata kama mnyama no mdogo anayemmudu pekeake labda ni Swala, watamuwinda hata Simba watatu au wanne.
Washirika hurahisisha KAZI na kupunguza gharama ya vita.
Hii kwa level ya Mtu binafsi, unapata somo kuwa ni muhimu kuwa na network, connection, washirika ambao mtakuwa mnasaidiana kwenye baadhi ya ishu hasa ishu nyeti.
Mfano, Misiba na magonjwa.
Unapokuwa na wadau matatizo kama msiba mzigo unapungua.
Washirika lazima muwe mnashare common interest, ikiwezekana mnafanana Culture kwa kiasi kikubwa au mshirika anapenda culture yako.
Iran washirika wake wote wanatofautiana naye kiitikadi, na culture.
Utamaduni wa China na Urusi upo mbali Sana na utamaduni wa Iran.
Mrusi na mchina kufuata utamaduni wa Iran ni KAZI kubwa kuliko kufuata utamaduni wa US
Kumbuka Mrusi naye ni Mzungu.
4. Kuwa Low Key na ujijenge mpaka utakapokuwa the beast ndio uonyeshe chuki dhahiri kwa adui yako
Iran hajui kuwa Low Key, anakamdomo,
Pamoja na chokochoko za USA na wanamagharibi Iran hakupaswa kujitutumua kukabiliana na adui zake kwa mtindo wa vitavita kama kuanzisha magenge ya kivita katika mataifa mengine ili kupambana na US na wamagharibi.
Angefanya kama China, au India na baadhi ya Mataifa ambayo yanauchumi mkubwa na teknolojia kumzidi.
Kwa Mtu binafsi, Maisha yako ni yako. Hakuna ulazima wa kupambana na adui zako ukiwa haujajipanga, tumia muda mwingi kujiimarisha kuliko kupambana adui aliyekuzidi maradufu.
5. Ni muhimu kujenga na kuimarisha mahusiano na ndugu na Majirani itakusaidia kupambana na adui wa Mbali.
Ukishagombana na ndugu na majirani na kuwafanya kuwa adui zako, hakuna namna yoyote utakayofanya kumshinda adui wa mbali.
Iran hapatani na majirani na ndugu zake. Hakukuwa na uwezekano wa yeye kushinda.
Kitu pekee ambacho Siku zote USA na washirika zake ni mahiri ni kugombanisha adui zake na ndugu na majirani zake ili iwe rahisi kwake kukupiga siku akishaona wakati umefika.
Na hicho ndicho Urusi anahangaika nacho sasa hivi.
Huwezi kushinda mechi yoyote Ile ikiwa adui kashawateka ndugu na jirani zako.
Hii inatufundisha, kama unamke na watoto. Ni lazima Kwanza uwafanye Wawe kitu kimoja na wewe. Mpendane, upendo(uzalendo) uwe juu yenu.
Kisha boresha mahusiano yako na ndugu zako mliozaliwa wote, wazazi alafu majirani.
Unapokabiliana na adui wa mbali hata awe na nguvu gani hawezi kukushinda ikiwa Una familia yenye umoja yaani mkeo na watoto, ndugu na jamaa kuna nguvu.
Migogoro ya ndani ya kifamilia ni muhimu kuiondoa kwa haraka na kuishughulikia kwa tahadhari kubwa na upendo.
Majasusi wa Mosad huwatumia wananchi na Askari wa Iran wasiowaaminifu(wasio na maslahi na nchi yao).
Kukosa uaminifu huweza pia kuwa na tafsiri ya kukosa maslahi ya Jambo Fulani.
Usije ukasema Pesa pekeake zitakusaidia kuwashinda adui zako ikiwemo magonjwa.
Nope!
Pesa pekee haitoshi!
Mahusiano ndio msingi wa kushinda kwako katika vita yoyote. Kisha pesa ifuate.
China anatafuta pesa, utajiri na teknolojia, naamini kitakachofuata ni kutafuta mahusiano Bora.
Kumbuka Pesa na utajiri ni kichocheo kikubwa cha mahusiano Bora katika utawala na mamlaka.
Acha nipumzike!
Robert Heriel
Taikon Master
Kwa sasa Dar es salaam