Kushindwa kwa Heche kuongoza BAVICHA

Kushindwa kwa Heche kuongoza BAVICHA

Kwanini heche anatumia jina la kaka yake.!!!heche haitwi john heche...john heche ni jina la kaka yake ambaye amemaliza st.agustine mwanza
heche ametumia jina la kaka yake kupenya kwenye tundu la kupata uongozi.
Ndio maana kwenye hoja yangu ya awalo nimesema heche hatembelei chaso kwasababu anaogopa kuzungumza na wasomi??
 
Huu uzi umeshachangiwa sana na sijataka kusoma maoni ya wadau wengine wameandika nini. Nafahamu utakuwa umeshaambiwa ukweli wa kutosha lakini wacha nikomelee msumari juu ya misumari.

Huu ujinga wa kila siku mnakesha kwenye mitandao ya kijamii mkiwatukana na kuwadiscourage viongozi wetu watatu; Mh. Mbowe, Katibu Mkuu Dr. Slaa na Kamanda Heche hautawasaidia chochote zaidi ya kuwazika ninyi wenyewe kisiasa.

Vijana wanamiminika kujiunga na Chadema kwakuwa pamojja na mambo mengine wameridhikka na utendaji kazi wa mwenyekiti wa Bavicha chini ya uenyekiti wa Kamanda Heche. Kila mara tunashuhudia kwenye television, redio, magazeti na mitandao ya kijamii Heche akifanya mikutano maeneo mbalimbali. Ni juzijuzi tu ametoka kufanya mikutano mjini Sumbawanga, tena sasahivi Heche anaungwa mkono sana na watu wa rika zote.

Kamanda Heche amefanya mikutano ya hadhara na ya ndani mikoa kama ya Arusha, Morogoro, Rukwa, Katavi, Dar es salaam, Mara, Mwanza, Shinyanga, Ruvuma, Iringa, Mbeya, Tabora n.k. Sasa mtu unapokurupuka na kuja na allegations za kipuuzi kama hizi eti Heche anakaa ofisini tu ni zaidi ya kuwa na kichwa nazi. Hata viongozi wa ccm wa ngazi ya kitaifa hawawezi kukusanya watu wengi kama anao wakusanya Heche katika mikutano yake.

Kama mlitaka Heche awe anafanya kazi ambayo haina maslahi kwa chama bali kwa maslahi yenu waganga njaa ni haki yenu kumuona mbaya kwakuwa hakuchaguliwa kuwatumika waganga njaa wachache bali kukijenga Chadema hasa kushawishi vijana wa aina zote, wasomi na wasio wasomi kujiunga na Chadema. Leo hii ccm inahangaika kuwarubuni na kuwahonga vijana ili wabadilishe muelekeo na kuiunga mkono, si kutoka vyuo vikuu ama sekondari vijana wanamiminika kuingia Chadema, kama si kazi nzuri ya mwenyekiti wa Bavicha hao vijana wanoingia Chadema kila kukicha wanavutiwa na nani?

Badala ya kukesha mkipika majungu dhidi ya viongozi wetu ni muhimu mjitafutie shughuli halali za kuwainbgizia vipato vya kila siku ili muache kutumiwa na ccm kuwachafua viongozi wetu wakakamavu. Na Mungu mkubwa aliwapa busara wajumbe wa kamati kuu na kuweza jutambua hila mlizokuwa nazo wakati mnagombea uongozi Bavicha na hivyo kuenguliwa, vinginevyo leo hii tungekuwa tunalia na kusaga meno. Watu wa ajabu sana nyie mnaopewa vijisenti vya mlo wa siku mbili tu mnakubali kuwatukana na kuwakashifu viongozi wenu hata hamuoni aibu? hata mkiambiwa muwatukane baba zenu kwakuwa mnapewa hela na chemba bila shaka mtawatukana kwakuwa mmepoteza uwezo wa kufikiria na kuamua, mmeshikwa akili na hao wanaowatuma.
 
Kwanini heche anatumia jina la kaka yake.!!!heche haitwi john heche...john heche ni jina la kaka yake ambaye amemaliza st.agustine mwanza
heche ametumia jina la kaka yake kupenya kwenye tundu la kupata uongozi.
Ndio maana kwenye hoja yangu ya awalo nimesema heche hatembelei chaso kwasababu anaogopa kuzungumza na wasomi??

Kumbe anaitwa nani? Mbona husemi anaitwa nani?
Na huko chaso ndio wapi, na inakuwaje unataka atembelee maeneo unayoyataka wewe. Au ungependa awe anaku -consult kabla hajapanga wapi atembelee?
 
_zitto hana muda wa kupotea kabisa na huu upuuzi wako.
Muulize heche ni namna gani zitto kamsaidia ...kimsngi heche na zitto ni maswahba sana ndio maana zitto kamwachia gari heche la kufanyia kazi.
Kumhusisha zitto ni kupoteza muda wako bure...zitto sio type yako.
Kwahiyo ulikuwa unalitaka hilo gari wewe? nenda zako na gamba la mwisho wewe na leo sijui kama utaponea BAN na hiyo miID
 
Kwanini heche anatumia jina la kaka yake.!!!heche haitwi john heche...john heche ni jina la kaka yake ambaye amemaliza st.agustine mwanza
heche ametumia jina la kaka yake kupenya kwenye tundu la kupata uongozi.
Ndio maana kwenye hoja yangu ya awalo nimesema heche hatembelei chaso kwasababu anaogopa kuzungumza na wasomi??

Tuntemeke huna jipya kuhusu Heche.

Tangu nimeanza kusoma thread zako zinazozungumzia Bavicha ama kumtaja Heche mwenyewe muda wote umejitahidi kuonyesha kwamba Heche hajafanya kitu wala si msaada wowote kwa chama. Nataka nikuthibitishie kwamba miongoni mwa vijana wenye uwezo mkubwa sana wa kuzungumza na audience basi heche ni mmoja wao ndani ya Chadema na hata nje ya Chadema.

Mara kadhaa nimewahi kuwa nae katika jukwaa moja katika mikutano ,mbalimbali ya wazi(hadhara) na mikutano ya ndani. Usijaribu kudanganya watu Heche ni namba nyingine kabisa, hata kama sikufahamu lakini kwakuwa unajiita kijana wa Chadema sina sababu ya kutoamini kwamba huwezi kujilinganisha na Heche, amekuacha mbali sana kisiasa, ni vizuri kuukubali huo ukweli ili ujipange na kutafuta namna ya kufikia ngazi ya juu ya uongozi kuliko kutumia style ya majungu na uzushi.

Kwa mfano hilo la kutumia jina la kaka yake ni uzushi mwingine uliamua kuja nao, nadhani JK aliwalenga watu kama wewe, nawe una kiwanda cha uongo, unaachia mmoja baada ya mwingine kadri unavyojisikia. Kama kitu hukijui ni muhimu kuuliza ili uelezwe kuliko kujidhalilisha kwa maneno ya kutunga. Kama kweli una uhakika kwamba yeye si John bali kaka yake ndiye John, basi ungetueleza yeye jina lake ni nani na huyo kaka yake yuko wapi na anafanya nini.

John Heche Suguta aligombea udiwani kata ya Tarime mjini katika uchaguzi mdogo wa mwaka 2008 na kumshinda vibaya mjomba wangu Peter Zakaria wa ccm, wakati huo akisoma Saint Augustine University(SAUT) Mwanza, tena akiwa darasa moja na mpwa wangu halafu leo kiwanda cha uongo cha tuntemeke kinafyatua uongo hapa eti anatumia jina la kaka yake na kwamba hajawahi kukanyaga chuo kikuu? Hii comment yako imeonyesha kiwango chako cha juu cha uongo, uzushi, husda na wivu.
 
Kwanini heche anatumia jina la kaka yake.!!!heche haitwi john heche...john heche ni jina la kaka yake ambaye amemaliza st.agustine mwanza
heche ametumia jina la kaka yake kupenya kwenye tundu la kupata uongozi.
Ndio maana kwenye hoja yangu ya awalo nimesema heche hatembelei chaso kwasababu anaogopa kuzungumza na wasomi??

Mkuu
Kama wewe sio Mwanamke basi una element za kike (UMBEA)
Nini maana ya wasome kwetu sisi watanzania? ni level gani mtu akifika huhesabika kasoma?
Heche ana Elimu gani? na Hao wasome anaoogopa wana elimu Gani? (angalia kwenye wall ya heche alikuwa St Agtn anaongea na hao unaowaita wasome

Naomba soma hata kwenye wall yako ujue Heche kasoma wapi USIKARIRISHWE kwa chuki zenu za kimakundi za kijinga au Zile element zako za kike (WIVU)?
 
We fisadi,a.k.a gamba najua kuna wanaokutuma ulete umbea hapa cdm v
ijana tunamkubali sana kamanda wetu heche, ni mpiganaji wa nchi kavu ,na angani,,kingine cdm hai

endeshwi kwa majungu wanachama ndo tunaangalia utendaji wa viongozi wetu...jua hilo acha kazi za kike au uende salon ukachongee na wenzioo....kina mage fatuma.shame on you
 
Ukiona wanamagamba kama Ritz wanatoa ushauri juu ya chadema ujue panga na marungu ya heche yamewajeruhi,kifupi nilimkuta heche hapa iringa mjini akichapa kazi,sumbawanga na mpanda na pande zote za tanzania je mwanamagamba wewe unashinda wapi sijui mpakaunakuja uharo ha jf
 
Katika Viongozi ambao ninawaona sana kwenye ziara za kujenga chama na M4C ni Heche..! Sasa ninashangaa mleta uzi anasema Heche ni mtu wa kukaa oficini..! Unless kama kuna Heche wawili vinginevyo ninakubaliana na Kamanda Molemo kwamba mmekalia majungu wakati wenzenu wako busy kuleta mapinduzi ya fikra kwa wananchi wa Tanzania.. Hamna tofauti na walowezi wa Rhodesia ya zamani.. Cijui Albert Muzorewa wenu ni nani katika hilo kundi lenu la walowezi but tumewachoka..

Mkuu jamaa kama karukwa na akili vile!Anawasha tochi mchana kweupe na kuhadaa watu kuwa ni usiku wa manane
 
Mkuu jamaa kama karukwa na akili vile!Anawasha tochi mchana kweupe na kuhadaa watu kuwa ni usiku wa manane

Yaani kila kukicha ni kufungua threads mpya.. Mara Mbowe na kauli tata.. Mara Slaa cijui amefanya nini..! Hivi kwa kuongea au kuleta uzi kama huo yule mkulima wa korosho kule Mtwara inamsaidiaje apate hela zake kwa korosho ambazo hajalipwa mpaka leo..?
 
Kwanini heche anatumia jina la kaka yake.!!!heche haitwi john heche...john heche ni jina la kaka yake ambaye amemaliza st.agustine mwanza
heche ametumia jina la kaka yake kupenya kwenye tundu la kupata uongozi.
Ndio maana kwenye hoja yangu ya awalo nimesema heche hatembelei chaso kwasababu anaogopa kuzungumza na wasomi??
jina lake halisi ni nani?
 
Kuna haja ya kuanzisha jukwaa la wana Chadema ili mambo, ya ndani ya chama chao, kama haya wakayajadili wenyewe huko kwenye jukwaa lao.
 
TUNTEMEKE,

Huwa napingana sana na wewe ka hoja za kuhit persola zaidi lakini kwa hili nasema nipo pamoja na wewe hizi Organsations za CHASO zipo hoi sana kwnye vyuo ni kama vile hawan miongiozo zinajiendesha kwa uatashi watu binafsi ni vema kukawa na mapango endelevu wa kuzitambua na kuziwezesha kimikakati ili ziwe chanzo cha viongozi hodari hapo baadaye.

Hili la kuwanyima MIC naweza kulisema ni jambo la kujipanaga kama vinajan wanalao jambo ambalo wanataka kuliongea sidhani kama HENCHE anaweza kuwazuia na hata kama akiwazuia wanaweza kupeleka malalamiko yao mahali panapo husika.

Mwisho TUMTEMEKE jaribu kwa ukaribu wako wa chama kuwasaidia hao wanaonyimwa fursa jinsi ya kuadress changamoto zao mbele ya viongozi wetu tuliowachangua kuliko kujakilalamika hapa as if wewe si miongoni mwa wanachadema, Naamini kama utakuwa na ujasiri wa kuongea na viongozi wako face bt face matokeo ya lalama zako hapa zitapatiwa ufumbuzi.
 
Last edited by a moderator:
unataka mpaka atangaze maandamano ndo ujue kwamba jamaa yuko fito?
 
Kuna haja ya kuanzisha jukwaa la wana Chadema ili mambo, ya ndani ya chama chao, kama haya wakayajadili wenyewe huko kwenye jukwaa lao.
hutaki mambo ya chadema yawe wazi?ndo demokrasia hiyo bwana
 
tatizo lenu mnaongozwa na mahaba binafsi juu ya chama hamtaki kuambia ukweli kwa halii hii ya kutopenda kuambiwa ukweli hatuwezi kuendelea

Mkuu, tatizo lako ni kwamba, katika yote uliyoyaandika hujatoa hata chembe ya ushahidi kuwaaminisha na kuwathibitishia wana JF, kwamba Mhe. Heche kweli kashindwa kuiongoza BAVICHA!

Ndiyo maana unaambiwa ulicholeta hapa ni majungu tu, hamna zaidi.
 
Back
Top Bottom